Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 59,804
- 134,593
Naunga mkono hoja na hiki ndicho nilicho shauri , Polepole ajitoe ndani ya CCM awe huru kukosoa.Kumpinga Dr. Samia ni haki ya kila anayejisikia kufanya hivyo, kwasababu kila mtanzania anayo haki ya kumchagua mgombea anayemtaka.
Lakini mtanzania unapojinasibisha kuwa mwana CCM unapoteza haki ya kumpinga mgombea wa CCM badala yake unakuwa na wajibu wa kumtetea. Kumpinga mgombea wa CCM, ukiwa umevaa sare za CCM ni USALITI.
Ushauri wangu, kama mwana CCM, hukubaliani na mgombea aliyeteuliwa, mambo ya kufanya ni mawili. Moja, baki ndani ya chama ukiwa umenyamaza, Mbili, Ondoka kwenye chama ufanye kazi ya upinzani. Lakini kufanya upinzani ndani ya chama, hizo ni vurugu.
Mwanachama wa CCM ana haki kukosoa jambo lolote au kiongozi yoyote, au maamuzi yoyote ya CCM, lakini uamuzi wa Mkutano Mkuu wa CCM ni uamuzi wa mwisho final and conclusive, ukiisha pitishwa, huwezi tena kuupinga. Mgombea akipendekezwa na CCM, unaweza kumpinga, lakini akiisha teuliwa na Tume kuwa mgombea wa CCM, then huwezi kumpinga, kuendelea kumpinga ni usaliti!.Sio ni umri mkuu unakufanya ushindwe kuchambua na kuona
Anayevunja taratibu za chama na anayekwmea aliyevunja taratibu za chama nani msaliti
Hii tabia tunaiona kwenye nchi kiongozi anavunja taratibu za nchi tunanyamaza ili tusionekana wasaliti
Uzalendo sio kuilinda viongozi ni Kusimamia taratibu za nchi
Hizi ni siasa za kimang'aa mnataka kuleta kizazi cha wajinga.Mwanachama wa CCM ana haki kukosoa jambo lolote au kiongozi yoyote, au maamuzi yoyote ya CCM, lakini uamuzi wa Mkutano Mkuu wa CCM ni uamuzi wa mwisho final and conclusive, ukiisha pitishwa, huwezi tena kuupinga. Mgombea akipendekezwa na CCM, unaweza kumpinga, lakini akiisha teuliwa na Tume kuwa mgombea wa CCM, then huwezi kumpinga, kuendelea kumpinga ni usaliti!.
Hata mimi nilipinga kilichofanywa na CCM, Dada Mkubwa tunakupenda na tunakukubali, kama ni wewe, ni wewe tu, hakuna mwingine! Usiruhusu uhuni huu, fuata Katiba na the due process, utabarikiwa lakini baada ya kupitishwa na INEC, na kampeni kuanza, kumpinga mgombea urais wa CCM ni usaliti!.
P
It's true, Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere ni kweli alifanya usaliti kwa kutoa hoja CCM sio baba yangu, sio mama yangu, ikituletea ujinga, unaichukua CCM, unatupa kule!.Nyerere ndio msaliti wa kwanza kumkataa mgombea wa Ccm jimbo la Musoma vijijini na kumfanyia kampeni mgombea wa Nccr Mageuzi Balozi Paulo Ndobho na akashinda uchaguzi mgombea wa ccm akaangushwa.
Kwani ulitaka kusemaje wewe unaijuwa Ccm kuliko Nyerere?