Ndugu Polepole, nitajie kituo Cha mabasi cha Wilaya au mkoa chenye Hoteli yenye hadhi Kama hoteli binafsi zinazohusu abiria wa safari ndefu

Sasa kwa Ile stendi ya matope bukoba magari yasimame wap.

Mpaka makampuni mengine kama friends hayaitumii hiyo stendi mbovu na finyu
 
Kwa hiyo unataka kudhania kuwa wakiwa wanakaa stendi ili kupata chakula hawatakula bure? Tumia akili bro kabla ya kutetea upuuzi.
Nafikiri upuuzi mkubwa wa binaadamu tena mtu mzima ni kufikiria kuwa yeye atakula bure bila kutoa jasho, ni ushenzi uliopitiliza kuwalazimisha watu wazima wafanye kile unavyotaka hata kama ni cha kipuuzi hivyo watu au wasafiri hivi sasa ni wakati muafaka wa kuchagua ale nini na wapi
 
Hoja sio repeatedly,hoja ni kwa nini kaitoa polepole??mnafiki
 
wahamie stend tu kwa kweli italeta ushindan.nimesafir from dar to arusha pale korogwe tumeipita vuuu vuuu kwenda kusimama kwenye hoteli mbele.kuuliza sasa menu buffet wal maharag 10,000. chips elfu 10,000, andaz 1000 chai 1000 nikasafir mpkaa arusha bila kula kitu.zaid nikala mosh mjin tena parachich
 
kwanza washenz wao wakikubwagen kwenye hayo mahotel yao.wao sijui hawanaga haja ndogo.moja kwa moja mbio dereva na konda wake kuchkua hela na chakula.nyie wanawapa dk 10 za chakula na choo.anakula yeye haraka haraka unasikia mahoni sasa pippiiii piiii nachukiaga
 
muelimishe huyu.hajui tu.
 
Hakuna ndoto mkuu serikali ikiamua itakua tu,tena hao jamaa wa hovyo sana hawaruhusu hata watu kuingia na chakula ndani ya Bus. Pale ni udikteta mwanzo mwisho usipokula unakufa na njaa,bei ya chini chakula buku 8. Labda unywe chai au biskuti.
niliteseka safar moja asee.ndio mara ya kwanza kutumia njia ya arusha af nikapanda hio ngoma.ile tunashushwa hotelin kwao bajet yangu ikawa ndog.nilienda na njaa mpaka arusha
 

Hawa madereva ni wapumbafu na hawana ubinaadamu kabisa, kwanini wasiige kwa wenzao wanaosafirisha ng'ombe kutoka kanda ya ziwa kwenda dar wao wakifika maeneo ya morogoro dumila hushusha ng'ombe wote na kuwalisha kwa siku mzima kabla ya kuendelea na safari
 
Una hoteli nini? Au yawezekana haujawahi kukumbana na usumbufu huu.
 
Cha msingi hapo.

Kwa maoni yangu. Hayo mabasi yasimame kote.

Kwenye hotel na stend ili kuwasaidia na wale ambao hawana pesa ya kumudu kununua chakula hotelini.
Na ndivyo Waziri alivyosema wakati akiongea na Babu Pole Pole
 
Mnataka kutuletea migahawa ya NANGURUKURU huku kaskazini.? Bakini nayo huko huko njia ya Kusini. Kuna siku nilienda Mtwara magazine 2 yakasimama nangurukuru vyoo vya wanaume ilikuwa kwa foleni. Kuna mama alikuwa na visamaki kumi havikutosha kitu abiria wrote waliondoka na njaa zao. Chonde chonde tuacheni KASKAZINI na ustaarabu wetu
 
Sasa kwa Ile stendi ya matope bukoba magari yasimame wap.

Mpaka makampuni mengine kama friends hayaitumii hiyo stendi mbovu na finyu
Kunamajani ya migomba mengi sana wanaweza wakayatandika Bukoba yote na hapo kituoni, kama wahaya waliweza kubuni kufunga tai hilo la kutandika majani ya migomba litawashinda?
 
Watu najua solution ikitolewa na Mwana CCM itapingwa kwa sababu ya Uchama. Mimi nimeshawahi bus likasima sehemu flani ya kawaida sana chai kikombe kidogo ya rangi tsh 1,000 na chapati ya kawaida ambayo mtaani ni tsh 500 wao wanauza tsh 2,000. Sababu ni kuwa Bus ndo linasimama pale na ni huo Mgahawa mmoja upo peke yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…