Ndugu wakulima na wafugaji sema changamoto yako kuhusu mazao yako na kila aina ya mifugo Ili wataalamu wakusaidie kutatua changamoto hiyo

Ndugu wakulima na wafugaji sema changamoto yako kuhusu mazao yako na kila aina ya mifugo Ili wataalamu wakusaidie kutatua changamoto hiyo

Napenda kujua shamba la Ekari 50 kabla hujapanda unatumia mbolea ya samadi au hata ya madukani inatosha...?

Kama ni samadi na eneo hilo hakuna ya samadi shamba linaweza kufanya vizuri wakuu...?
Mbolea ni mhimu mkuu samadi nzuri kwani inafaida nyingi kuliko hasara pia ina kaa muda mrefu. Mfano ukiweka ya kutosha na kwa usahihi hukaa kwa miaka3 ikifanya kazi yake vizuri.Ukikoswa ya samadi basi si mbaya ukatumia ya viwandani kulingana na uhitaji wa eneo lako.Kulima bila mbolea ni kujipunguzia uzalishaji kwa kiwango kikubwa.
Na pia, natakiwa kupitisha tractor na kuacha shamba litulie ndio nipande au naweza kupitisha tractor na kupanda kwa wakati mmoja ilhali mvua bado hazijaanza...?
Kama shamba ni safi na limelimwa vizuri mara moja tu inatosha. Unatakiwa upande ardhi ikiwa na unyevu wa kutosha ama uhakika wa mvua kama unamwagilia panda kisha mwagilia.
Na kama napitisha tractor then nasubiria lipoe ndio nipande, natumia tractor kupandia au nguvukazi...? Najua kuna plante ila inaweza ikaongeza gharama za uzalishaji, hapo imekaaje wadau...?
Nguvu ndo nzuri mkuu kani utapanda kwa usahihi zaidi.Kulisubiri lipoe ama kurudia kuklilima ni nzuri maana ardhi huchambuka vizuri na kulaini vizuri.Mambo haya yote hutgemea kipato na uchumi wako.

NB: Nimekujibu kulingana na uzoefu wangu na uelewa wangu subiri wengine watajazia ama kukosoa.
 
Nina maswali kadhaa nataka kufahamu chanjo zote nazotakiwa kumpa kuku kutokea kifaranga wa siku moja mpaka anapokuwa mtu mzima nataka kufahamu chanjo zinaaaply katika vipindi gani vya umri wa kuku anapoendelea kukua.Sijajua umebobea kufuga kuku wapi ila mimi nataka kudeal na sasso au kroiler
SWALI ZURI.

CHANJO ZA KUKU - RATIBA MAALUM​

1. SIKU 1.
Baada ya vifaranga kutotoleshwa ndani ya siku moja wapewe glucose kwa muda wa masaa mawili. Glucose huchanganywa katika maji na kupewa vifaranga hawa na baada ya hapo vifaranga wapewe mchanganyiko wa vitamins mfano ni AMINOVIT na OTC plus. Pia siku hiyoiyo ya kwanza kuku wapewe chanjo Marek's mara nyingi huwa haiandikwi maana dawa hii ni ghali kidogo na mara zote wauzaji wa vfaranga kampuni kubwa huwa chanja huko huko siku ya kwanza kabisa kabla hawajaanza ku-suply vifaranga.

Pia hii huchanganywa na maji. Vifaranga wawekwe katika eneo lenye joto wastani na safi. Baada ya hapo siku ya pili na kuendelea vifaranga wapewe
2. SIKU YA 7.
vifaranga wapatiwe chanjo ya NEWCASTLE (KIDERI). chanjo hii huchanganywa na maji safi katika eneo lenye kivuli kIsha kupewa vifaranga kwa muda wa masaa mawili kisha toa maji hayo na kuyamwaga mbali na eneo ambalo kuku wengine wanaweza kuyafikia,au kuyachimbia.baada ya hapo vifaranga wapewe maji yenye mchanganyiko wa vitamini
3. SIKU YA 14.
Wapewe chanjo ya GUMBORO(IBD). Chanjo hii pia huchanganywa katika maji na kupewa vifaranga kwa muda wa masaa mawili tu, baada ya hapo vifaranga wepewe mchanganyiko wa vitamin. Kuku waliokufa kwa ugonjwa huu unaweza kuwatambua kwa kuchana vifua vyao na hapo utaona vidoti vyekundu kama hapo pichani
4. Siku ya 21 (wiki ya tatu)
Rudia chanjo ya Newcastle (Kideri)
5. SIKU 28 (Mwezi)
Rudia chanjo ya GUMBORO IBD
6. SIKU 35 (Mwezi 1 na wiki 1)
Kipindi hiki kuku wapewe mchanganyiko wa vitamin ya kutosha.
7. WIKI YA 6-8
KUKU wapatiwe kinga ya Ndui (fowl pox).kinga hii sio rahisi kwa mfugaji asiye na utaalam kuwapa kuku, tafuta mtaalum wa mifugo kwa kazi hii au upate maeleze ya jinsi ya kuweka kinga hii.
8. WIKI YA 8
Kuku wapatiwe dawa ya minyoo kama Piperazzine na baada ya hapo unaweza kurudia chanjo ya Newcastle
 
EvilSpirit NIMETOA HUMU HUMU JF UZI TOKA KWA jijayetu

1. Baada ya kuanguliwa , Chanjo ya Marek's na Dawa HVT, Namna: sindano
2. Siku ya 2 hadi 6 KINGA ya Pullorum, Dawa: Trimazine 30% plus Vitamin, Namna: Maji
3. Siku ya 7, Chanjo ya Mdondo/Kideri (Newcastle), Dawa: Newcastle vaccine [LASOTA] Namna: Maji
4. Siku ya 14, Chanjo ya Gumboro, Dawa: chanjo ya Gumboro, Namna: Maji
5. Siku ya 16 – 20, KINGA ya Koksidiosis (coccidiosis), Dawa: Trimazine 30% plus vitamin (Vitalyte itafaa), Namna: Maji
6. Siku ya 21, Chanjo ya Mdondo tena.. [Maelezo yapo kwa juu]
7. Siku ya 28 rudia chanjo ya gumboro,&Siku ya 30hadi 32, KINGA: kuimarisha kinga ya mwili, OTC 20% changanga na Amin'Total vitamin.
8. Siku ya 35 hadi 39
KINGA: Mafua, OTC 50% au CORDIX (ukiona kinyesi kina muharo kiasi) au Tylosine 75% changanya na Amin'Total.
9. Siku ya 56, Chanjo: Ndui. Hapa inabidi uangalie sasa kutokana na changamoto za magonjwa wape kati ya wiki ya 7 na kuendelea kutokana na kwamba ktk majumba yetu tuna kuku wakubwa na wadogo hivyo tafiti zinasema hivyo kwa sasa.
10. Siku ya 60 hadi 64 (Rudia namba 6 hapo juu)
11. Wiki ya 12 ( kati ya siku ya 64 hadi 70), Chanjo: Typhoid
12. Wiki ya 13 (kati ya siku 85 hadi 91), KINGA: minyoo
13. Wiki ya 15, Ukataji wa midomo
14. Wiki ya 16, KINGA ya kipindupindu, OTC 20 YA SINDANO, Sindano kwenye nyama ya kifua.
15. Wiki ya 17, KINGA ya mafua, Tylosine ya sindano, Sindano kwenye nyama ya kifua
16. Wiki ya 18, chajo ya Typhoid, Baada ya hapo, waache kuku.. Hakuna sindano tena...&Chanjo zinazobaki ni...
(A) Mdondo/Kideri(Newcastle Vaccine) aina ya LASOTA
(B) Minyoo &Hizi zote ni kila baada ya miezi mitatu mitatu....
 
Kwanza asante kwa mualiko huu mkuu.

Pili naomba nikiri kuwa siko vizuri sana kwenye kuelezea jambo au kumuelekeze mtu jambo kwa njia ya maandishi,hiyo ndio changamoto yangu.Hivyo endapo nitashindwa kueleweka nitakuwa tayari kurudia tena na tena.

Tatu KIOO umegusia mambo 3

Matumizi ya samadi Vs Mbolea za dukani.

Kulima na kupanda hapo hapo Vs kulima kwanza na kupumzisha shamba Kwa muda kisha ndio upande.

Kupanda kwa trekta Vs Nguvukazi.
Nafurahi kupata message yako natumai itanisaidia katika kupata mwangaza wa kile ninachohitaji kufahamu mkuu.

Ni kweli hayo ndio maswali niliyouliza kutaka kufahamu usahihi wake mkuu. Natanguliza shukran kwako.
 
KIOO
Uchaguzi wa aina gani ya mbolea ya kutumia shambani kwako, unategemea factors kama

Hali ya udongo
Aina ya udongo
Upatikanaji wa mbolea
Uchumi
Lengo la Kilimo
Kiwango cha rutuba n.k

Mbolea ya samadi ina faida na hasara zake.
Mbolea za madukani zina faida na hasara pia
Nimekuelewa vyema mkuu.

Unaposema hali ya udongo inamaanisha natakiwa nikapime maabara au najuaje mkuu...?

Upatikanaji wa mbolea kwa huku sidhani kama samadi inapatikana kuweza kutosha Ekari zote hizo ila kwa mbolea za madukani naweza nikapata Arusha mjini.

Uchumi, kwa kuwa Kilimo huwa kinaenda hatua kwa hatua natumai nitaweza kumudu gharama za mbolea, mbegu pamoja na madawa hilo hakuna shaka coz lengo la Kilimo ni Kilimo Biashara mkuu.

Kiwango cha rutuba nadhani hili suala ni kama hali ya udongo, kufahamu hilo natakiwa kupeleka maabara kupima au...?

Na mwisho, ni zipi faida na hasara kati ya mbolea ya samadi vs mbolea za madukani mkuu...?

Shukran sana.
 
Mbolea ni mhimu mkuu samadi nzuri kwani inafaida nyingi kuliko hasara pia ina kaa muda mrefu. Mfano ukiweka ya kutosha na kwa usahihi hukaa kwa miaka3 ikifanya kazi yake vizuri.Ukikoswa ya samadi basi si mbaya ukatumia ya viwandani kulingana na uhitaji wa eneo lako.Kulima bila mbolea ni kujipunguzia uzalishaji kwa kiwango kikubwa.

Kama shamba ni safi na limelimwa vizuri mara moja tu inatosha. Unatakiwa upande ardhi ikiwa na unyevu wa kutosha ama uhakika wa mvua kama unamwagilia panda kisha mwagilia.

Nguvu ndo nzuri mkuu kani utapanda kwa usahihi zaidi.Kulisubiri lipoe ama kurudia kuklilima ni nzuri maana ardhi huchambuka vizuri na kulaini vizuri.Mambo haya yote hutgemea kipato na uchumi wako.

NB: Nimekujibu kulingana na uzoefu wangu na uelewa wangu subiri wengine watajazia ama kukosoa.
Mkuu, nashkuru sana kwa mchango wako natumai utaleta tija na nitafanya hivyo kupitia ushauri huu, ngoja tusubirie na michango ya wadau tukusanye kwa pamoja ili tuifanyie kazi.

Nashkuru sana kiongozi.
 
Nimekuelewa vyema mkuu.

Unaposema hali ya udongo inamaanisha natakiwa nikapime maabara au najuaje mkuu...?

Upatikanaji wa mbolea kwa huku sidhani kama samadi inapatikana kuweza kutosha Ekari zote hizo ila kwa mbolea za madukani naweza nikapata Arusha mjini.

Uchumi, kwa kuwa Kilimo huwa kinaenda hatua kwa hatua natumai nitaweza kumudu gharama za mbolea, mbegu pamoja na madawa hilo hakuna shaka coz lengo la Kilimo ni Kilimo Biashara mkuu.

Kiwango cha rutuba nadhani hili suala ni kama hali ya udongo, kufahamu hilo natakiwa kupeleka maabara kupima au...?

Na mwisho, ni zipi faida na hasara kati ya mbolea ya samadi vs mbolea za madukani mkuu...?

Shukran sana.
Ili kupata uhakika na mbolea ya madin gani inahitajika kwa wingi ni vyema kwenda kupima MAABARA. Mimi sijawahi pima mkuu . Pia nakuomna nunua mbolea ya ruzuka badara ya kununua 150k+ wewe unalipia 60-70k kulingana aina ya mbolea.

Mkuu kwetu sisi wazoefu swala la kuianglia tu ardhi kwa macho huwa tunajua wazi kuwa hii ardhi ina rutuba hata nyasi za eneo hilo utaziona zilivyo stawi maabara huwa wanapeleka kuangalia ardhi ina upungufu gani ili mbolea sahihi itumike kwa wingi na kutokutumia mbolea kadhaa ambazo hazina ulazima kulingana udogo wako.

Madhara ya mbolea ya samadi na faida mkuu nitaleta somo kwa kina hapa hata nijkitaja faida sitatoa maelezo(nipo job) baki hapahapa nitaleta somo kwa kina na nita ku Quote
 
SWALI ZURI.

CHANJO ZA KUKU - RATIBA MAALUM​

1. SIKU 1.
Baada ya vifaranga kutotoleshwa ndani ya siku moja wapewe glucose kwa muda wa masaa mawili. Glucose huchanganywa katika maji na kupewa vifaranga hawa na baada ya hapo vifaranga wapewe mchanganyiko wa vitamins mfano ni AMINOVIT na OTC plus. Pia siku hiyoiyo ya kwanza kuku wapewe chanjo Marek's mara nyingi huwa haiandikwi maana dawa hii ni ghali kidogo na mara zote wauzaji wa vfaranga kampuni kubwa huwa chanja huko huko siku ya kwanza kabisa kabla hawajaanza ku-suply vifaranga.

Pia hii huchanganywa na maji. Vifaranga wawekwe katika eneo lenye joto wastani na safi. Baada ya hapo siku ya pili na kuendelea vifaranga wapewe
2. SIKU YA 7.
vifaranga wapatiwe chanjo ya NEWCASTLE (KIDERI). chanjo hii huchanganywa na maji safi katika eneo lenye kivuli kIsha kupewa vifaranga kwa muda wa masaa mawili kisha toa maji hayo na kuyamwaga mbali na eneo ambalo kuku wengine wanaweza kuyafikia,au kuyachimbia.baada ya hapo vifaranga wapewe maji yenye mchanganyiko wa vitamini
3. SIKU YA 14.
Wapewe chanjo ya GUMBORO(IBD). Chanjo hii pia huchanganywa katika maji na kupewa vifaranga kwa muda wa masaa mawili tu, baada ya hapo vifaranga wepewe mchanganyiko wa vitamin. Kuku waliokufa kwa ugonjwa huu unaweza kuwatambua kwa kuchana vifua vyao na hapo utaona vidoti vyekundu kama hapo pichani
4. Siku ya 21 (wiki ya tatu)
Rudia chanjo ya Newcastle (Kideri)
5. SIKU 28 (Mwezi)
Rudia chanjo ya GUMBORO IBD
6. SIKU 35 (Mwezi 1 na wiki 1)
Kipindi hiki kuku wapewe mchanganyiko wa vitamin ya kutosha.
7. WIKI YA 6-8
KUKU wapatiwe kinga ya Ndui (fowl pox).kinga hii sio rahisi kwa mfugaji asiye na utaalam kuwapa kuku, tafuta mtaalum wa mifugo kwa kazi hii au upate maeleze ya jinsi ya kuweka kinga hii.
8. WIKI YA 8
Kuku wapatiwe dawa ya minyoo kama Piperazzine na baada ya hapo unaweza kurudia chanjo ya Newcastle
Nashukuru kwa muongozo
 
Ili kupata uhakika na mbolea ya madin gani inahitajika kwa wingi ni vyema kwenda kupima MAABARA. Mimi sijawahi pima mkuu . Pia nakuomna nunua mbolea ya ruzuka badara ya kununua 150k+ wewe unalipia 60-70k kulingana aina ya mbolea.

Mkuu kwetu sisi wazoefu swala la kuianglia tu ardhi kwa macho huwa tunajua wazi kuwa hii ardhi ina rutuba hata nyasi za eneo hilo utaziona zilivyo stawi maabara huwa wanapeleka kuangalia ardhi ina upungufu gani ili mbolea sahihi itumike kwa wingi na kutokutumia mbolea kadhaa ambazo hazina ulazima kulingana udogo wako.

Madhara ya mbolea ya samadi na faida mkuu nitaleta somo kwa kina hapa hata nijkitaja faida sitatoa maelezo(nipo job) baki hapahapa nitaleta somo kwa kina na nita ku Quote
Nitashkuru sana sana kiongozi nasubiria kwa shauku kubwa mkuu. Ahsante sana.
 
MTI WA PAPAI HUTIBU........

IMG_20240427_144503_583.jpg

Chemsha magao mawili ndani ya maji lita 6 hadi ubakie na lita 1. Poza kisha chuja.

Hutibu minyoo aina yote.
MBEGU ZAKE:Hutibu minyoo pia kusanya mbegu kiasi uwezavyo kisha kausha ziwe kavu kabisa weka sehemu salama hasa kwenye ndoo au mfuko usiopitisha maji/unyevu.
Chukua nusu kikombe cha chai changanya na kg5 za chakula chako kwa siku 4 tu hata kama hujaona dalili za minyoo zoea kuwapa tu kwani hutibu na kukinga magonjwa kadhaa.Pia wengine huweka kwenye maji lita3 kwa kijiko kimoja cha chakula.Kwenye minyoo pia ongeza na mbegu za mlonge punje tatu hadi5 zintosha kutibu maji lita 5 ya kunywa iwe binadamu au mifugo huwa nafanya hivyo mimi hasa kwenye mbuzi.
Mbegu za mlonge ukizisaga ni nzuri sana na maji huwa msafi kama umeweka shabu uchafu wote utaukuta chini.
MAJANI YA MPAPAI.
Hutibu kuharisha (Coccidiosis):
Mafua
Kipindupindu

Chukua majani ya mpapai matawi 3-5 ya ponde/twanga yawe kama kisamvu loweka kwenye maji lita6 kwa muda wa masaa2 chuja wape. makapi usitupe chnganya kwenye chakula chao.

UTOMVU WA PAPAI
Hutibu vidonda kama kuku kajeruhiwa na kupata jeraha tumia utomvu wake ni vyema ukatumia na maji ya tunda la ndulele kwa matokeo mazuri zaidi.

NB:Ili upate mbegu za mapapai za kutosha panda mipapai angalu 10 ni nzuri sana hii tiba ya mpapai kama nilivyo orodhesha hapa. hii itakusaidia wewe kulamatunda yake na kuuza hata usipouza kuku ni wadau wazuri mno wa kula mapapai hasa bata ndo mahala pake.

AHSANTE.
 
Na mwisho, ni zipi faida na hasara kati ya mbolea ya samadi vs mbolea za madukani mkuu...?
1. Mbolea za asili

Mbolea aina ya Mboji na samadi (Mabaki ya Mazao). Mbolea hizi hutokana na vinyesi vyawanyama, mabaki ya mazao shambani,majivu na takataka nyingine ambazo nirafiki kwa mazao na udongo (takataka zisizo na madhara kwenye udongo).

1.Mbolea za asili zinafaa sana kutumika wakati wa kuandaa shamba/ mkulima anaweza kuchamganya mbolea ya asili na udongo wakati wa kulima aumkulima kuitumia mbolea ya asili kupandia mazao yake mfano mahindi,mharagwe, mboga mboga na mazao mengine.
Mbolea za asili hufanya kazi ya kuboresha hali ya udongo kufanya udongo uwe na uwezo wa kuhifadhi maji na hewa, vilevile mbolea za asili ufanya udogokuweza kutengeneza matundu mazuri ambayo husaidia mizizi ya mazao nahewa kupenya kwa urahisi.

FAIDAYA MBOLEA ZA ASILI(MBOJI NA SAMADI)
1.Gharama nafuu.
Huitaji kuwa na mtaji mkubwa wa kifedha ili kupata ainahii ya mbolea. Kikubwa zaidi pengine ni gharama za kusafirisha mbolea hiyo.

2.Mbolea ya asili huongeza, kujenga na kukuza mpangilio wa udongo. Hufanyahewa kupenya kwenye mchanga na husaidia utoaji maji shambani hasa kuzuia mmomonyoko wa udongo.
Mbolea hii hufanya mchanga kuwa na maji auunyevunyevu wakati wa Kiangazi. Kwa kutengeneza mpangilio wa mchanga,hufanya mimea kupata rutuba kwa urahisi na kukua kwa afya na kutoa mavuno mengi.

3.Kutunza ubora wa udongo, Mbolea ya asili hutunza ubora wa udongo kwakuongeza madini yanayohitajika na mimea. Hii inasaidia kuongeza mazao ya mimea.

4.Kupunguza wadudu wa mimea walioko mchangani, hivyo mimea kuwa na nguvu, afya na hustahimili magonjwa na wadudu waharibifu.

5.Haibebwi na mvua au kuhamishwa. Mbolea ya asili haibebwi na maji ya mvua kama ilivyo mbolea za kemikali, hivyo inaifanya kuwa na sifa ya kudumu kwa muda mrefu.

6.Kuondoa wadudu rafiki wa mmea. Hii ni tofauti na mbolea za kemikaliambazo huvutia wadudu waharibifu na kuondoa mazingira rafiki ya wadudu muhimu.

7.Huupatia mmea virutubisho vingi. Mbolea za viwandani zina virutubishobaadhi kwa kiasi fulani zaidi ya vingine. Lakini mbolea za asili zina utajiri wavirutubisho.

8.Huwezesha mizizi ya mmea kukua vizuri kuelekea kwenye virutubisho muhimu. Hii hufanyika kutokana na kuboreshwa kwa muundo wa udongo.Kama udongo ulikuwa umeshikamana, unapowekewa mbolea asili huwa laini,hivyo kurahisisha mizizi kupenya kwa urahisi.

9.Kuongeza ‘ph’ ya udongo. Moja ya matatizo yanayo punguza uzalishaji ni mkulima kuwa na udongo wenye ph ya chini dhidi ya mazao yake.Kwa kuweka mbolea ya asili, ph huongezeka hivyo kuuweka mmea katika halinzuri ya kuongeza uzalishaji.

Hasara za mbolea ya asili

1.Mbolea ya asili haiwezi kuokoa mmea unao kufa, kwa sababu huchukua muda mrefu kuchukuliwa na mmea. Wakati mbolea ya viwandani ikishaloanishwa tu haraka huchukuliwa na mmea. Mbolea ya asili inahitajikuoza zaidi na kuvunjwavunjwa.

2.Upatikanaji wake ni mgumu. wakulima wengi wanashindwa kupata mboleaya asili kwa haraka. Hii ni kutokana na wafugaji wa wanyama kama ngombekuwapo maeneo ya mbali.

3.Huhitajika kwa wingi. Kwa mfano, kwa ekari moja mkulima anaweza kuhitajikuanzia tani 12, kwa sababu mbolea asili inahitajika kuwekwa kwa wingi.Mathalani, katika kila shimo, utapaswa kuweka mbolea inayoweza kujaaviganja vya mikono miwili. Kama ni katika matuta huwekwa kuanzia toroli tatu kwenye tuta la urefu mita 9 na upana mita 5.

4.Huathiri mmea, inaweza kukausha mmea mara moja kama itawekwa bila kuzingatia hali ya mbolea hiyo. Kwa mfano, kama itawekwa ikiwa haijaozavyema inasababisha mmea kuungua na kukauka
Lakini pia ikiwekwa ikiwa mbichi inaweza kusababisha mmea kupata magonjwa ya fangasi na bakteria.

5.Ni ngumu kujua virutubisho unavyoongeza. Mbolea za kemikali huwa navirutubisho vikuu vitatu kwa ukuaji bora wa mmea wako.Hivyo wakati mkulima anaweka, hujua kabisa kiwango anachoweka chanaitrojeni, fosiforasi na potasiamu. Kwa mbolea ya asili, mkulima hawezi kujuaameweka kiasi gani cha virutubisho hivyo muhimu.

Msisitizo

Mbolea ya asili ni njia nzuri mno ya kulisha mimea kuliko kutumia mbolea yakemikali. Mbolea za kemikali japo hutoa rutuba kwa mimea, hazitengenezi mpangilio au hali ya mchanga.

FAIDA YA MBOLEA ZA KEMIKALI/VIWANDANI

1.Hufanya kazi kwa haraka.
Nirahisi mno kuokoa mmea kufa kutokana na ukosefu wa virutubisho.Virutumbisho vilivyomo kwenye mbolea hizi hufyonzwa kwa uharaka zaidi.

2.Upatikanaji ni rahisi

3.Hutumika kidogo tu

4.Ina virutubisho muhimu vinavyo hitajika katika mmea na mkulima hutambua aweke kwa kiasi gani.

MADHARA YA MBOLEA ZA KEMIKALI(VIWANDANI)

1.Gharama kubwa.

2.Kuondelewa virutubisho haraka.

3.Huathiri udongo.
Matumizi ya mbolea hizi muda mrefu huongeza chumvi ambayo badae huathiri udongo na mavuno kupungua

4.Ukiweka zaidi ya kiwango huunguza mimi kwa muda mfupi na mmea kufa.

5.Inahitaji elimu namna ya kutumia.

6.Athari za afya.
Mbolea hizi zinahitaji umakina namna ya kutumia kwani zinaweza leta madhara katika ngozi na mifumo ya upumuaji.

7.Huondoa wadudu muhimu katika ukuaji wa mmea.

MUHIMU:- Mbolea hizi ni nzuri kama itatumiwa kwa muda mfupi na siyo kwa muda mrefu kwani ina athiri kwenye rutuba ya udongo.
 
Duh, Ekari moja nahitajika kupata tani 12 za mbolea ina maana kwa shamba la Ekari 50 nahitajika kupata tani 600 za mbolea, mbona zoezi kubwa sana.

Nafkiri nitumie tu za kununua viwandani kuliko hizo tani 600 kuzipata kwake sio kazi ndogo bado uzisafirishe, inabidi uache kazi ufanye kazi mkuu.

Umenipa mchango mkubwa sana na pia ukipata dondoo zozote juu ya maswala niliyouliza usisite kunipa mchango wako kiongozi.

Nakushkuru sana sana sana mkuu. Ahsante sana.
 
Duh, Ekari moja nahitajika kupata tani 12 za mbolea ina maana kwa shamba la Ekari 50 nahitajika kupata tani 600 za mbolea, mbona zoezi kubwa sana.
Ninavyo jua hapa kwenye samadi na mboji unatakiwa uelewe kuna utofauti mkubwa mfano mboji unaweza izidisha na isilete madhara yoyote maadamu mvua ina nyesha ama kuna unyemvu wa kutosha.

Mfano usiokuwa wa kitaaramu ni kwamba ukichukua kg2 za mbolea ya mboji ukachanganya na mchanga kg1 ukipanda zao lako haitakuwa na shida bali litanawili mno.

Kwenye samadi nako imegawanyika katika sehemu kuu 2
1. Ni ile iliyoiva. ni mbolea iliyokaa muda mrefu ama pale kulikuwa na zizi mifugo ikahama kwa mwaka ama miaka2 mbolea iliyoachwa hapo itakuwa imeiva ama kuoza kabisa. Hii mara nyingi huwa nzito sana inakuwa kama mchanga kiasi kwamba ukichukua ndoo ya lita20 ukaijanza hiyo mbolea vilevile ukachukua ndoo ya lita20 ukaweka mbolea ya can ama urea uzito utakuwa tofauti mbali mno.

2.Nile ambayo haijaiva ama ni ile ya juu ipo kama vumbi ukienda mazizini hasa kiangazi utaona kuna mbolea juu juu na ni nyepesi mfano wa vumbi tu. hii ukichukua ndoo ya lita 20 ukaipima si ajabu ukapta kg4-5 tu wakati ile iliyooza unaweza pata kg23+ hadi hapo umepata picha.

Unapaswa kufahamu kuwa mbolea ya samadi/mboji humwagwa shamba lote bila kujali hapa utapanda ama hutapanda! hii lazima iende mbolea nyingi tofauti na mbolea za viwandani smbavyo mbolea hu wekwa moja kwa moja kwenye mmea/shina husika.

Chukulia mfano uchukue kg1 ya urea umwage chini pia chukua kg1 ya samadi mwaga pia bila shaka eneo halitatofautiana sana ndo picha halisi ilivyo.

Kwanini mbolea ya samadi inamwaga shamba lote? Kumbuka hapo mwanzo nilisema hukaa muda mrefu hadi zaidi ya miaka3 ikiwa inafanya kazi. hivyo hata usipoitumia kwa kipindi hiki ukija kulipa awamu ijayo utaikuta na itakuwa imeoza vizuri zaidi. Na ukweli uko hivyo awamu ya pili ndo huwa na matokeo mazuri zaidi,.
 
Habari za uzima wenu ndg zangu hongereni sana kwa mapambano.Na wapenda sana.

Nimeona nianzishe huu uzi uwe wa General kwa kutuma changamoto zetu zote tunazopitia katika mifugo yote. Hii namanisha kila aina ya kiumbe kinachofugwa unaweza kuuliza swali lolote kuhusu mifugo yako, kutoa ushauri wako pia ni mhimu sana, ku share nasi kipi unafanya/umefanya hadi kufikia hapo ulipo,Tuambie kuhusu magonjwa ya mifugo yako na namna unavyo pambana nayo. Ningeomba wadau ukaambanisha na picha/clip fupi watu wajifunze kwako.

Hali kadharika kwenye kilimo iwe vivyo hivyo kama nilivyo sema hapo juu kwenye mifugo.

Ifahamike wazi kuwa mimi sio mtaalamu na wala sijasomea kilimo wala mifugo ijapokuwa nina uzoefu japo natambua Elimu haina mwisho napenda sana kujifunza leo, kesho na kesho sijawahi acha.

Nita share nanyi vyote nivijuavyo kwenye ufugaji na kilimo na nipo tiyari kukosolewa kwa 100% pale ukiona nipo tofauti na unavyojua wewe lengo ni kuelimishana. Usiogope kutoa maarifa uliyo nayo kwani ukitoa hapa kichwa chako kitafunguka kupokea maarifa mapya zaidi trust me hii ndo kanuni.

Pia nawiwa sana kufahamiana (siyo lazima) kwa wale watapenda wafahamiane hasa maeneo jirani na wanakoishi mfano watu GEITA,KAHAMA,MWANZA,SHINYNGA wakafahamiana na ikiwezekana kutembeleana ili kujifunza kwa vitendo ingefaa pia(mawazo yangu)

Imani yangu ni kubwa sana kuwa humu kuna watu waliosomea hizi taaruma zote mbili.

Hapa itakuwa sehemu sahihi kwangu kuwapa tiba asili na hata ikiwezekana nitakuwa natuma video ninavyo andaa hasa kwenye kuku na mbuzi maana ndo mifugo ninayo fuga. kwa sasa sina kuku kutokana na chanagamoto kadhaa.

Nategemea watu watakuwa Serious midhaha isichukue nafasi sana hadi kututoa kwenye lengo.

Kwa sasa natumia divice ya kazini sina picha lakini by saa1 nitaweka picha hapa.

Karibuni sana..........

MLONGE KAMA DAWA YA KUKU/KANGA NA BATA.
View attachment 3195205

Mlonge una vitamini A na C. Chukua majani ujazo wa mikono miwili (gao mbili). Kisha yapondeponde
na kuyaweka katika lita 10 za maji na iache kwa masaa 12 chuja na wape kuku. Isiyotumika
mwaga na tengeneza nyingine.

Iwapo hutaweza kuloweka kwa masaa hayo 12 basi mimi huwa nafanya hivi

Nachukua magao kama4 au5 binafsi huwa nakadiria tu maana sijawahi ona madhara kwenye kuku kama nimezisha.

Baada ya kuyaponda ponda kwenye kinu nitaloweka kwa muda wa lisaa1 tu kisha nayachuja vizuri.Kisha yale makapi naya changanya na chakula chao. huwa nafanya hivi kwa siku3-4 tu na kushuhudia maendeleo mazuri sana. Siku 4 zikiisha kesho yake siku ya5 huwa nawapa mpapai nitakuja elezea kwa kina.

Mlonge hutibu:

Mafua.
Kideri - inyweshwe kabla kwa kukinga
Kipindupindu cha kuku (Fowl Cholera).
Kuongeza hamu ya kula
Homa ya matumbo
kuhara
Ini.

Huwa nashauri kila mfugaji awe na miti hii kwake
Alovera
Mpapai
Mwembe
Mwarobaini
Pilipili kichaa
Mkonge(katani)
Komfrey
kuna minyaa yenye majani mapana (Cactus)

Hii ni baadhi tu na Nitaileza kwa mti mmoja baada ya mwingine.

TUTAENDELEA*
Shukrani Sana mkuuu,somo zuri sana
 
Yaani Jana na juzi kuku wangu wengi wamekufa,walikuwa wanatoa kinyesi cheusi,kijani na cheupe.
Walikuwa wanakohoa au kutoa sauti kubwa ,wanatoa maji maji yanayovutika km kamasi.
Nikafikiri Ni mafua nikanunua dawa ya mafua,jamani jamani,wamekufa wa kutosha.
Sasa inabidi nitafute elimu sahihi ya ufugaji,Asante boss,naamini nitajifunza mengi humu
 
Sawa nitakurudia mkuu ukiona kimya ni quote tafadhari
 
Pilipili kichaa.

Pondaponda kiasi kisha changanya na maji na wawekee kuku wawe wanakunywa muda wowote

Hutibu na kukinga....

Hii ni Kinga ya kideri/mdondo.
Hutibu mafuta hasa ukichanya na bapa la mkonge likipondwa pondwa na kuchanganywa.
View attachment 3195232

Hizi ni Moja wapo ya aina ya pilipili kichaa lakini og ni vile vidogovidogo sana ukipata hivyo Kwa kwenye Lita Moja ya maji weka5 tu hizi weka Saba Hadi 10.
Naomba kujua mkuu ni wapi nawezapata pili pili kichaa,mbegu zake,na je kilimo chake kikoje? Na zipi changamoto zake?,ahsante niko kanda ya ziwa.
 
Naomba kujua mkuu ni wapi nawezapata pili pili kichaa,mbegu zake,na je kilimo chake kikoje? Na zipi changamoto zake?,ahsante niko kanda ya ziwa.
Mkuu sijawahi lima hili zao halafu kuna tofauti kubwa kati ya pilipili kali na pilipili kichaa watu huwa wanaunganisha tu in fact hata iliyopo hapo pichani sio kichaa ambayo sisi tumekua tukaikuta na sasa ni nadra sana kuipata (kama upo kanda ya ziwa wasukuma huita bhukoloja)

Soko la pilipili kichaa/kali lipo sana nje ya nchi hata rwanda tu hapa wanalao.

kuhusu mbegu zake labda ukusanye kidogokidogo ila pwani niliwahi ona kama heka moja ya pilipili kali wao wanaita kichaa.

Sifa ya pilipili kichaa ukiimenya tu ile harufu yake lazima ukohoe pia ukizidsha matumizi lazima uugue kifue huwa ni vidogo sana nikienda kijijini nikabahatika kupata nitapiga pia niweke hapa.
 
Back
Top Bottom