Na mwisho, ni zipi faida na hasara kati ya mbolea ya samadi vs mbolea za madukani mkuu...?
1. Mbolea za asili
Mbolea aina ya Mboji na samadi (Mabaki ya Mazao). Mbolea hizi hutokana na vinyesi vyawanyama, mabaki ya mazao shambani,majivu na takataka nyingine ambazo nirafiki kwa mazao na udongo (takataka zisizo na madhara kwenye udongo).
1.Mbolea za asili zinafaa sana kutumika wakati wa kuandaa shamba/ mkulima anaweza kuchamganya mbolea ya asili na udongo wakati wa kulima aumkulima kuitumia mbolea ya asili kupandia mazao yake mfano mahindi,mharagwe, mboga mboga na mazao mengine.
Mbolea za asili hufanya kazi ya kuboresha hali ya udongo kufanya udongo uwe na uwezo wa kuhifadhi maji na hewa, vilevile mbolea za asili ufanya udogokuweza kutengeneza matundu mazuri ambayo husaidia mizizi ya mazao nahewa kupenya kwa urahisi.
FAIDAYA MBOLEA ZA ASILI(MBOJI NA SAMADI)
1.Gharama nafuu.
Huitaji kuwa na mtaji mkubwa wa kifedha ili kupata ainahii ya mbolea. Kikubwa zaidi pengine ni gharama za kusafirisha mbolea hiyo.
2.Mbolea ya asili huongeza, kujenga na kukuza mpangilio wa udongo. Hufanyahewa kupenya kwenye mchanga na husaidia utoaji maji shambani hasa kuzuia mmomonyoko wa udongo.
Mbolea hii hufanya mchanga kuwa na maji auunyevunyevu wakati wa Kiangazi. Kwa kutengeneza mpangilio wa mchanga,hufanya mimea kupata rutuba kwa urahisi na kukua kwa afya na kutoa mavuno mengi.
3.Kutunza ubora wa udongo, Mbolea ya asili hutunza ubora wa udongo kwakuongeza madini yanayohitajika na mimea. Hii inasaidia kuongeza mazao ya mimea.
4.Kupunguza wadudu wa mimea walioko mchangani, hivyo mimea kuwa na nguvu, afya na hustahimili magonjwa na wadudu waharibifu.
5.Haibebwi na mvua au kuhamishwa. Mbolea ya asili haibebwi na maji ya mvua kama ilivyo mbolea za kemikali, hivyo inaifanya kuwa na sifa ya kudumu kwa muda mrefu.
6.Kuondoa wadudu rafiki wa mmea. Hii ni tofauti na mbolea za kemikaliambazo huvutia wadudu waharibifu na kuondoa mazingira rafiki ya wadudu muhimu.
7.Huupatia mmea virutubisho vingi. Mbolea za viwandani zina virutubishobaadhi kwa kiasi fulani zaidi ya vingine. Lakini mbolea za asili zina utajiri wavirutubisho.
8.Huwezesha mizizi ya mmea kukua vizuri kuelekea kwenye virutubisho muhimu. Hii hufanyika kutokana na kuboreshwa kwa muundo wa udongo.Kama udongo ulikuwa umeshikamana, unapowekewa mbolea asili huwa laini,hivyo kurahisisha mizizi kupenya kwa urahisi.
9.Kuongeza ‘ph’ ya udongo. Moja ya matatizo yanayo punguza uzalishaji ni mkulima kuwa na udongo wenye ph ya chini dhidi ya mazao yake.Kwa kuweka mbolea ya asili, ph huongezeka hivyo kuuweka mmea katika halinzuri ya kuongeza uzalishaji.
Hasara za mbolea ya asili
1.Mbolea ya asili haiwezi kuokoa mmea unao kufa, kwa sababu huchukua muda mrefu kuchukuliwa na mmea. Wakati mbolea ya viwandani ikishaloanishwa tu haraka huchukuliwa na mmea. Mbolea ya asili inahitajikuoza zaidi na kuvunjwavunjwa.
2.Upatikanaji wake ni mgumu. wakulima wengi wanashindwa kupata mboleaya asili kwa haraka. Hii ni kutokana na wafugaji wa wanyama kama ngombekuwapo maeneo ya mbali.
3.Huhitajika kwa wingi. Kwa mfano, kwa ekari moja mkulima anaweza kuhitajikuanzia tani 12, kwa sababu mbolea asili inahitajika kuwekwa kwa wingi.Mathalani, katika kila shimo, utapaswa kuweka mbolea inayoweza kujaaviganja vya mikono miwili. Kama ni katika matuta huwekwa kuanzia toroli tatu kwenye tuta la urefu mita 9 na upana mita 5.
4.Huathiri mmea, inaweza kukausha mmea mara moja kama itawekwa bila kuzingatia hali ya mbolea hiyo. Kwa mfano, kama itawekwa ikiwa haijaozavyema inasababisha mmea kuungua na kukauka
Lakini pia ikiwekwa ikiwa mbichi inaweza kusababisha mmea kupata magonjwa ya fangasi na bakteria.
5.Ni ngumu kujua virutubisho unavyoongeza. Mbolea za kemikali huwa navirutubisho vikuu vitatu kwa ukuaji bora wa mmea wako.Hivyo wakati mkulima anaweka, hujua kabisa kiwango anachoweka chanaitrojeni, fosiforasi na potasiamu. Kwa mbolea ya asili, mkulima hawezi kujuaameweka kiasi gani cha virutubisho hivyo muhimu.
Msisitizo
Mbolea ya asili ni njia nzuri mno ya kulisha mimea kuliko kutumia mbolea yakemikali. Mbolea za kemikali japo hutoa rutuba kwa mimea, hazitengenezi mpangilio au hali ya mchanga.
FAIDA YA MBOLEA ZA KEMIKALI/VIWANDANI
1.Hufanya kazi kwa haraka.
Nirahisi mno kuokoa mmea kufa kutokana na ukosefu wa virutubisho.Virutumbisho vilivyomo kwenye mbolea hizi hufyonzwa kwa uharaka zaidi.
2.Upatikanaji ni rahisi
3.Hutumika kidogo tu
4.Ina virutubisho muhimu vinavyo hitajika katika mmea na mkulima hutambua aweke kwa kiasi gani.
MADHARA YA MBOLEA ZA KEMIKALI(VIWANDANI)
1.Gharama kubwa.
2.Kuondelewa virutubisho haraka.
3.Huathiri udongo.
Matumizi ya mbolea hizi muda mrefu huongeza chumvi ambayo badae huathiri udongo na mavuno kupungua
4.Ukiweka zaidi ya kiwango huunguza mimi kwa muda mfupi na mmea kufa.
5.Inahitaji elimu namna ya kutumia.
6.Athari za afya.
Mbolea hizi zinahitaji umakina namna ya kutumia kwani zinaweza leta madhara katika ngozi na mifumo ya upumuaji.
7.Huondoa wadudu muhimu katika ukuaji wa mmea.
MUHIMU:- Mbolea hizi ni nzuri kama itatumiwa kwa muda mfupi na siyo kwa muda mrefu kwani ina athiri kwenye rutuba ya udongo.