Ndugu wakulima na wafugaji sema changamoto yako kuhusu mazao yako na kila aina ya mifugo Ili wataalamu wakusaidie kutatua changamoto hiyo

Ndugu wakulima na wafugaji sema changamoto yako kuhusu mazao yako na kila aina ya mifugo Ili wataalamu wakusaidie kutatua changamoto hiyo

Mkuu asante sana umekuja wakati muafaka kwa sababu namimi nina changamoto yangu.

Kuku wangu (Malawi Breed) wameshafikisha umri wa kuanza kutaga toka mwaka jana mwezi 11 lakini mpaka leo hawajaanza kutaga. Yan ukiingia bandani unaokota mayai hafiki 8. Kuku wap 150 na wanapata chakula na mboga za majani enye mchanganyiko safi na salama. Tatizo ni nini?
Ulianza nao toka vifaranga au ulinunua tayari wakubwa?
Mchanganyiko wako tuuone, ili tutoe ushauri.
 
Toka vifaranga.. sipo nyumbani ila nawachanganyia pumba ya mahindi, mahindi yaliyobarazwa, mashudu ya alizeti, DCP, GLP, chokaa, damu, unga wa dagaa, chumvi.
Huwa unachanganya wewe mwenyewe? kwa kawaida ulipaswa ununue starter hapo mwanzo na kama umewafuga ka nia ya mayai nashauri nunua chakula chao...pia huenda umemenua f2 (uzao wa pili ) watatanga tu ila speed itakuwa chini
 
MWAROBAINI HUTIBU......
Kuhara.
Kuzuia Kideri.
Typhoid.
Mafua.
Vidonda.

Mwarobaini unaweza tumia majani yake,magome na hata mizizi kipimo kadiria kulingana na kuku wako.

Na shauri utumie majani kwani ukiparua/kumegua magome amaukachimba mizizi uwezekano nimkubwa sana wa miti kukauka. Katika yote haya mizizi ndo inaufanisi sana hasa ukichemsha na kuwa nywesha kuku wagonjwa wastani wa mils10 kuku wakubwa wadogo mls5.
ANGALIZO USITUMIE MBEGU ZAKE.

Ahsante
 
Yaani Jana na juzi kuku wangu wengi wamekufa,walikuwa wanatoa kinyesi cheusi,kijani na cheupe.
Walikuwa wanakohoa au kutoa sauti kubwa ,wanatoa maji maji yanayovutika km kamasi.
Nikafikiri Ni mafua nikanunua dawa ya mafua,jamani jamani,wamekufa wa kutosha.
Sasa inabidi nitafute elimu sahihi ya ufugaji,Asante boss,naamini nitajifunza mengi humu
ulitumia dawa gani ndugu
 
Huwa unachanganya wewe mwenyewe? kwa kawaida ulipaswa ununue starter hapo mwanzo na kama umewafuga ka nia ya mayai nashauri nunua chakula chao...pia huenda umemenua f2 (uzao wa pili ) watatanga tu ila speed itakuwa chini
Walipokua wadogo niliwapa chakula chao kuanzia starter, grower mpaka finisher. Baadae nikaanza kuwapa chakula cha mchanganyiko. Nawafuga kienyeji asubuhi wanapata chakula then wanaanza kujitafutia wenyewe mchana kutwa hapo mida ya saa nane nawapa mamboga ya majani
 
Toka vifaranga.. sipo nyumbani ila nawachanganyia pumba ya mahindi, mahindi yaliyobarazwa, mashudu ya alizeti, DCP, GLP, chokaa, damu, unga wa dagaa, chumvi.
Ingekuwa vizuri ukadadavua...ni kwa uzani upi...mfn pumba kilo 2, shudu kilo XX....hapo ndio tunaweza shauri ila hii ya kuorodhesha tu....ni ngumu kutoa ushauri
 
Mbolea ni mhimu mkuu samadi nzuri kwani inafaida nyingi kuliko hasara pia ina kaa muda mrefu. Mfano ukiweka ya kutosha na kwa usahihi hukaa kwa miaka3 ikifanya kazi yake vizuri.Ukikoswa ya samadi basi si mbaya ukatumia ya viwandani kulingana na uhitaji wa eneo lako.Kulima bila mbolea ni kujipunguzia uzalishaji kwa kiwango kikubwa.

Kama shamba ni safi na limelimwa vizuri mara moja tu inatosha. Unatakiwa upande ardhi ikiwa na unyevu wa kutosha ama uhakika wa mvua kama unamwagilia panda kisha mwagilia.

Nguvu ndo nzuri mkuu kani utapanda kwa usahihi zaidi.Kulisubiri lipoe ama kurudia kuklilima ni nzuri maana ardhi huchambuka vizuri na kulaini vizuri.Mambo haya yote hutgemea kipato na uchumi wako.

NB: Nimekujibu kulingana na uzoefu wangu na uelewa wangu subiri wengine watajazia ama kukosoa.
Na samadi afanye kuiboresha kwa kuiongezea Phosphorus.
Hapa ataongeza Ndoo ndogo ya Majivu/ Lota 10( Jivu la pumba ya mpunga ama jivu lolote) kwa ndoo 2 kubwa mbolea.
Taratibu hii hutumiwa na watu wa Kenya kwa muda mrefu ma wanapata matokeo chanya pasi na kupoteza rutuba.
 
Yaani Jana na juzi kuku wangu wengi wamekufa,walikuwa wanatoa kinyesi cheusi,kijani na cheupe.
Walikuwa wanakohoa au kutoa sauti kubwa ,wanatoa maji maji yanayovutika km kamasi.
Nikafikiri Ni mafua nikanunua dawa ya mafua,jamani jamani,wamekufa wa kutosha.
Sasa inabidi nitafute elimu sahihi ya ufugaji,Asante boss,naamini nitajifunza mengi humu
Pole saana.....ulitumia dawa gani?
 
Na samadi afanye kuiboresha kwa kuiongezea Phosphorus.
Hapa ataongeza Ndoo ndogo ya Majivu/ Lota 10( Jivu la pumba ya mpunga ama jivu lolote) kwa ndoo 2 kubwa mbolea.
Taratibu hii hutumiwa na watu wa Kenya kwa muda mrefu ma wanapata matokeo chanya pasi na kupoteza rutuba.
Shukrani sana mkuu. Ukweli huwa nikizama youtube huwa naingia kujifunza ufugaji na kilimo kwa wakenya,uganda na mambele kama china israel nk naona kabisa wakenya tu hapa jirani wamepiga hatua sana kwenye kilimo /ufufgaji.

Umeongeza madini muhimu sana.
 
Walipokua wadogo niliwapa chakula chao kuanzia starter, grower mpaka finisher. Baadae nikaanza kuwapa chakula cha mchanganyiko. Nawafuga kienyeji asubuhi wanapata chakula then wanaanza kujitafutia wenyewe mchana kutwa hapo mida ya saa nane nawapa mamboga ya majani
Pumba debe 10, shudu debe 1, mahindi debe 2, unga wa dakaa nusu ndoo. Hivyo vingine kilo moja moja
Tumia vipimo vya mzani...achana na habari za debe!
Na mchanganyo wako :
Carbohadrate = 60%
Protini= 16-20%
Madini = 2.5%
Calcium= 10%
Vingine chezea 1-5%
Nasisitiza tumia vipimo vya mzani mkuu.

MIMI HUWA NAFANYA HIVI NA MATOKEO HUWA SI MABAYA

Mahindi kg50
Pumba mahindi kg15
Soya kg18 unaweza punguza kama huwafungii ndani
Mashudu alizeti pamba ama alizeti kg7
Dagaa/Uduvi/mabaki ya samaki kg4(dagaa zikaangwe huwa na wadudu nk)
Mifupa kg3
Chokaa kg2 au 1kama mifupa umeweka kg3 uhakika
Chumvi 0.5(gram 500)nusu kg
Vitamini kg2

Mkuu jaribu hii uone na usiache kuwapa majani

Ahsante sana
 
Na samadi afanye kuiboresha kwa kuiongezea Phosphorus.
Hapa ataongeza Ndoo ndogo ya Majivu/ Lota 10( Jivu la pumba ya mpunga ama jivu lolote) kwa ndoo 2 kubwa mbolea.
Taratibu hii hutumiwa na watu wa Kenya kwa muda mrefu ma wanapata matokeo chanya pasi na kupoteza rutuba.
Nashkuru sana kiongozi tatizo ni upatikanaji wa samadi kwa shamba kubwa ni changamoto sana, nikitumia mbolea za madukani pekee vipi zitaweza kufanya vizuri mkuu...? Shukran sana.
 
Mkuu sijawahi lima hili zao halafu kuna tofauti kubwa kati ya pilipili kali na pilipili kichaa watu huwa wanaunganisha tu in fact hata iliyopo hapo pichani sio kichaa ambayo sisi tumekua tukaikuta na sasa ni nadra sana kuipata (kama upo kanda ya ziwa wasukuma huita bhukoloja)

Soko la pilipili kichaa/kali lipo sana nje ya nchi hata rwanda tu hapa wanalao.

kuhusu mbegu zake labda ukusanye kidogokidogo ila pwani niliwahi ona kama heka moja ya pilipili kali wao wanaita kichaa.

Sifa ya pilipili kichaa ukiimenya tu ile harufu yake lazima ukohoe pia ukizidsha matumizi lazima uugue kifue huwa ni vidogo sana nikienda kijijini nikabahatika kupata nitapiga pia niweke hapa.
Ahsante, fanya ivyo Mkuu uzipige picha nione, maana wengi wanazichanganya,kuna moja nimepiga picha toka kwa jirani,nitaituma umu uione,mungu akipenda.
 
Back
Top Bottom