Ndugu yako akifanya kazi hii "Mmempoteza"

The Boss

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2009
Posts
49,282
Reaction score
117,244
Sielewi shughuli zingine zina nini ..lakini
Mtu akijiingiza Tu huko na tabia inabadilika moja kwa moja ...harusi tena kuwa Yule wa zamani...

Hii kazi ya udalali hapa Dar ..mtu akishajiingiza Tu ..basi very soon anakuwa
'haaminiki'
'mpigaji'
"Utapeli"
"Usanii"..

Yaani hata Ndugu zake anawaingiza mjini. Nyumba za familia inabidi muwe macho ..mkimpa hati eti aende kulipa kodi manispaa ..usishangae akiuza. Kibaya zaidi hii kazi ya udalali mtu anaweza kuwafanyia udalali hata mashemeji zake au dada zake...

Kama dalali mwanamke ndo kabisa..
Anaweza kuuza hata mabinti zake....

Hizi kazi zingine sijui zina nini..
Ngumu Sana kukutana na dalali sio
Muongo.
Muaminifu
Ana maadili..

Wengi pesa mbele ..full usanii..
 
Sielewi shughuli zingine zina nini ..lakini
Mtu akijiingiza Tu huko na tabia inabadilika moja kwa moja ...harusi tena kuwa Yule wa zamani...
Ni kweli..ila ingekuwa vyema kama ukishea yaliyokukuta
 
Kazi nyingine ambayo vinasaba vya watendaji wake zinafanana na madalali ni mafundi (nguo, carpenter, waashi n.k)...

Wale wa njoo uchukue nguo yako kesho, au kabati lako kesho ni waongo waongo sana
 
Sielewi shughuli zingine zina nini ..lakini
Mtu akijiingiza Tu huko na tabia inabadilika moja kwa moja ...harusi tena kuwa Yule wa zamani...
Pia Madalali wengi wana network na Watu Wa madili ya hatari na Haramu, i.e majambazi, wauza madawa ya kulevya, Machangudoa n.k..
 
Kazi ni kazi kama kazi zingine endapo muhusika ataweka tamaa nyuma na kusimama kwenye misingi na maadili ya kazi yake......

Mimi nimefanya kazi na madalali wengi wanaojitambua na sijawahi kukumbana na kadhia ya aina yoyote kutoka kwao.....

Madalali wanaongoza kwa utapeli na uongo ni wale waliotanguliza tamaa mbele badala ya weledi wa kazi......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…