Ndugu yangu amenipa sharti la kuacha kazi ya kuajiriwa ili anipe mtaji wa Tshs 200M nianze shughuli yangu mwenyewe lakini sijui nifanye shughuli gani!

Tumia akili, badala ufocus kwenye biashara yenye thamani ya 200m uhangaike na kazi ya 1.5m ambayo inakula zaidi ya masaa 8 ya siku nzima

Hakuna pesa inayoachwa kama uwezekano wa kuipata upo unless uwe limbukeni lenye mihemko likiona pesa.

M200 tayari unadharau m18 kwa mwaka?😂😂 Unadhani ni rahisi kuzungusha m200 ikupe faida ya m18 kwa mwaka? Wewe ndo tumia akili.

Mm nakushauri Kama kuna uwezekano wa kuwekeza m200 huku unapata hiyo 1.5m fanya hivyo ila kama ni lazima sana uiache hiyo 1.5m kaa chini tuliza akili sana.

Halafu kama inawezekana usifanye jambo jipya usilolijua.
 
hardware haimtupi mtu ikipata sehemu safi yenye wateja,
 
Bujibuji acha mzaha, this is serious, nategemea hekima zako![emoji1]

By the way, wife anapinga kabisa suala la kuacha kazi!
Weka TB za BOT za miaka 20 au 25 unavuna 2.7m kila mwezi hiyo unajibana unawekeza mdogo mdogo. Mambo yakikaa sawa yakisha materialize unauza kwenye secondary market then una re-invest elsewhere
 
Anzisha hata kiwanda cha mikate...
Jenga apartment au rent house fungua kibanda cha pesa..huduma za kifedha weka kijana.

by the way kumbe kuna watu wana hizi ela!
ukoo wetu mzima ukipata shida ya 500,000 hadi kuuza mbuzi
 
Kama hakupendi ataifuja tu biashara
 
Twende baa tukafanye icho kikao cha shughuli ya kufanya ukipewa izo ela....
 
Mkuu, kuacha kazi sio uamuzi wangu, ni sharti la sponsor! I give you USD 100,000 only if you are willing to quit your job and seriously pursue business, commit to it. You cant have both, your job and the USD 100,000.
Usd laki ni zaidi ya 200M mkuu mie ningetia bond yote halafu 23M ndio nifanyie biashara
 
Okay, ila kumbuka nikiichukua hiyo hela maanake sina kazi. Ila uzuri kuna hii nyingine ya mafao
Wee chukua hiyo bwana m200 kwanza bro. Tafuta kiwanja jenga apartment zako kadha tulizana.
Nyingine nunua tipa nenda kiranjeranje kilwa kuokota mawe ya gypsum
 
Dah hii Dunia hii duuuu!

Wewe nitafute kwa muda wako nikupe ufafanuzi wa namna ya kufanya haya nayotaka kukushauri. Lakini zaidi naomba partnership tupige kazi mimi ni skills za Biashara lakini sina financial power.

Mapendekezo:

1. Tafuta partner mzuri wa kufanya naye biashara (Mimi nafaa zaidi). Biashara inahitaji skills fulani fulani hv

2. Jaribu biashara yeyote unayoona inafaa ili u practice maana umesema hujawahi kufanya biashara. Soma mwelekeo wa hio Biashara, then ndo ukija kupata hizo pesa utaendeleza

3. Kuna aina kuu mbili za uzalishaji wa income: Active & Passive income. Mara nyingi passive income inahitaji mtaji mkubwa na unao tayari, kwa hio opt zaidi kufanya passive income kwa scale kubwa halafu active income fanya kwa scale ndogo ili uendelee kujifunza zaidi.

Kuhusu ni aina ipi ya active or passive kuna mjadala mkubwa zaidi kwa upande wa details.

Kimsingi, Fanya juu chini nitafute tuzungumze kwa kina zaidi
 
Kuna mtu alinipanga tufanye biashara pamoja mimi nitoe mtaji yeye atasimamia. Alinipa business idea very impressive nikazama benki nikampa Milioni 3 akachukue mzigo. Tangu 2012 hadi leo sijamuona. Kuwa makini na ushauri
 
Kuna tra mdau usisahau maana wanafilisi balaa wameshaliza wafanya biashara wengi wa mtaji kama wako.......

naona hili wengi wamesahau kukuambia
 
Bujibuji acha mzaha, this is serious, nategemea hekima zako![emoji1]

By the way, wife anapinga kabisa suala la kuacha kazi!

Kumbe mkeo ameshakushauri boss..!? Sasa unataka sisi huku tukuvunjie ndoa aiseeh!

Ama fanya hivi,acha kazi chukua mpunga! Siku hiyo hiyo unayochukua mpunga tengeneza mkeka wa odds 5, mechi tatu tu weka m100…
Utapata m500, chukua m200 mrudishie ndugu yako mwambia ahsante kwa kukuthamini, mpe mkeo m200 na wewe baki na m200, then wewe rudi kazini kesho yake, ama tafuta kazi sehemu nyingine!
Kisha mshtue Bujibuji akupeleke viwanja vikali na pisi kali uenjoy maisha!
 
Shee huyo ndugu yako hataki uwe mtumikishwa so mimi pia ni mwajiriwa lkini sipendi kuwa mtumwa ..dah natamani kijiajiri na kuajiri piaa sasa hapo boss 200ml nyingi saana..mimi nakushauri chukua kisha ingia mafinga hapo na 20ml tu.. kachukue mzigo wa mbao kauze bandari pale Tanga utakuja nishukuru..
 
Nimekuewlewa mkuu, ila sasa huo sio uamuzi wangu. Msimamo wake ni kwamba acha kazi, fanya biashara nitakupa mtaji. La sivyo endelea na kazi yako.
Kwa hii kauli inaonekana kazi unayofanya haijitoshelezi bado unakuwa unamsumbua sumbua kuomba baadhi ya mahitaji kwake thus why amekwambia hivo maana ameona kazi unayofanya haina faida..so cha kukushaur acha tu hiyo kazi.
 
Cha kufanya tafakari biashara gan unaweza fanya pia kuwa makin kuangalia location pia usiitumbukize yote katika biashara ingine weka fixed then ingne ndo iende kwenye biashara utakayokuwa umeona inafaa.
 
Kinachowafelisha wengi Ni kuingia kwenye biashara while hawana idea yoyote kuhusu biashara.

1.Biashara inahitaji uijue (uwe na uzoefu ) hata Kama hukuwahi kuifanya Basi uwe uliwahi kushirikishwa.

2.Biashara pia inahitaji uwe mjanja ( Simaanishi uwe tapeli au mwizi lah! ) hapa inatakiwa uwe na uwezo wa kuibadiri kuringana na nyakati.

Mtoa mada kama huna idea na uzoefu wowote kuhusu Nini utafanye mwambie jamaa Hali halisi then yeye atajua Nini afanye .
Kama kweli ana nia ya kukupa pesa atakupa tu, KUWA MUWAZ

Wastaafu wengi hufirisika wanapoanzisha biashara kutokana na hicho nilichokiandika hapo juu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…