Ndugu yangu amenipa sharti la kuacha kazi ya kuajiriwa ili anipe mtaji wa Tshs 200M nianze shughuli yangu mwenyewe lakini sijui nifanye shughuli gani!

Utakuwa Afisa Ardhi Mfawidhi wewe
 
Mkuu kwa ushauri Kama upo dodoma, tafuta sehemu nje kdgo ya mjini, watu wanajenga Sana, anzisha bonge la hardware plus timber apo apo uweke na mashine ya kuchana mbao,, nunua viwanja au kiwanja jenda lorge ya kisasa kiasi uweke bei nzuri. Uweke akiba dodoma watu wengi hua wanauza viwanja bei rahisi ila tuu ukae usome mchezo sio kuingia kichwa kichwa kupitia kwa madalali ukipata viwanja kwa bei nzuri uwezekano wa kuuza bei nzuri zaidi ni mkubwa Sana. Jitahidi kufanyia kazi mawazo yangu utakuja kunishukuru. Ela yako haiwezi kupotea mkuu
 
Usijaribu kufanya biashara hata kidogo kama hujawahi
Utateketeza huo mtaji
Anza Biashara kidogo kidogo ukiwa bado kwenye ajira uielewe
 
Mkuu Chukua 200m ..fanya shauri za wadau kuhusu bonds..Ila anglia inaonekn mkeo kakuweka sana kiganjani..

Do a Manly decision.
 
Yaani ningepata ml 50 tu ningeacha kazi. Ningenunua boda boda 20 na kuwapata vijana kwa mkataba wa mwaka mmoja then boda zinakuwa za kwao.
Then ningeanzisga duka la spea za boda boda kwa sharti bida boda wote 20 wanakuja kufanya repair kwangu. Hapo nina uhakika wa hesabu ya siku ya boda boda 20 na uhakika wa wateja 20 wa kufanya repair na kununua spair za boda boda kwenye duka langu.
Golini ningeajiri fundi mmoja na mm mwenyewe kukusanya hesabu. Eeeh Mungu nijalie mwaka huu niipate hiyo pesa maana baada ya miaka miwili nitakuwa na vijiwe kama hivyo vinnr.
 
Sio kirahisi hivyo kama unavyofikiri
Taarifa za ajali zitakuzidia huwajui Hawa jamaa wa bodaboda bado wewe
 
Sio kirahisi hivyo kama unavyofikiri
Taarifa za ajali zitakuzidia huwajui Hawa jamaa wa bodaboda bado wewe
Nina uzoefu. Ajali ni moja wapo ya risk. Ila boda akijua baada ya mda chombo kinakuwa chake anaweza maliza ddni hata kabla muda.
 
Nina uzoefu. Ajali ni moja wapo ya risk. Ila boda akijua baada ya mda chombo kinakuwa chake anaweza maliza ddni hata kabla muda.
Elewa sio rahisi kihivyo ninafanya hiyo biashara ya Toyo 3 elewa sio rahisi kihivyo
 
Mkuu milioni 50 bodaboda 20?
 
Elewa sio rahisi kihivyo ninafanya hiyo biashara ya Toyo 3 elewa sio rahisi kihivyo
Hicho ndicho kila mtu kaniambia. Kila biashara naaambiwa sio rahisi. Sasa kuna watu wanapata faida kweli kwenye biashara?
 
Elewa sio rahisi kihivyo ninafanya hiyo biashara ya Toyo 3 elewa sio rahisi kihivyo
Nimeshasimamia hiyo kitu zilikuwa 17. Ilikuwa bizness ya sistaangu. Inategemea maana usimamizi wa miradi nacho pia ni kipaji au kunshitaji shule na uzoefu pia. Kipaumbele kimojawapo cha kuingia mkataba ilikuwa kwa watu wenye familia zao.
 
Mkuu Chukua 200m ..fanya shauri za wadau kuhusu bonds..Ila anglia inaonekn mkeo kakuweka sana kiganjani..

Do a Manly decision.
Mkuu hujaoa wewe, au kama umeoa ni yale makabila mnasema mwanamke si mtu wa kuthaminiwa wala kusikilizwa. Badilikeni Mkuu, wafundisheni watoto wenu mtazamo tofauti.

Kuna jamaa yangu toka sehemu fulani kaskazini alikuwa shocked kuja nyumbani na kuona tunakaa meza moja na dada zangu wakati wa chakula! Anasema wanapaswa kulia chakula chao jikoni. Nilimwambia kila akija tukala pamoja yeye na mimi tutakaa pamoja na dada zangu mezani wakati wa kula, na akiona haiji basi aache kuja nyumbani kwetu
 
Hicho ndicho kila mtu kaniambia. Kila biashara naaambiwa sio rahisi. Sasa kuna watu wanapata faida kweli kwenye biashara?
Hajuna business rahisi na hakuna busness ambayo haina faida. Ndio mana sponsor anataka uache kuajiriwa ili uitumikie biashara yako kikamilifu.
 
Boxer mdogo wangu alinunua 3m kama miaka mitatu iliyopita
Wapi huko? Inategemea na cc, labda kama alichuku cc 150 ambazo zinachezea 2.7 mpaka 2.8. Ila hizi cc 125 max price ni 2.5 ml
 
Million 200 ni pesa nzuri sana. Tuliza kichwa upate biashara nzuri ya kufanya. Kuna faida kubwa sana kujiajiri kuliko kuajiriwa hasa ukiwa bado na nguvu.
 
Hajuna business rahisi na hakuna busness ambayo haina faida. Ndio mana sponsor anataka uache kuajiriwa ili uitumikie biashara yako kikamilifu.
Na hicho ndio anasisitiza. Anasema sio kwamba ananifanyia roho mbaya, bali biashara inahitaji total commitment ili ifanikiwe. Anasem siwezi kuwa nina devote 8 hrs kwa mwajiri kila siku halafu eti nifanikiwe kwenye biashara, yaani anasema hapo anajua hizo hela zitapotea tu.
 
Take 5 years unpaid leave kisha ingia kitaa pambana, ndani ya 5 years utakuwa umejifunza sana na kama itatokea umefilisika utarudi kazini.
200M ni ndogo sana Mkuu kwani watumishi kibao zinasoma katika akaunti zao.
Ingekuwa 5B basi ungeacha mazima maana hapo ungejikatia Bima ya Afya, chakula, na bill zingine na bado mtaji unao. Kitaa sio poa kabisa kwani utapoteza ndugu, jamaa na marafiki kwa ukata utakaokukuta.
Kupanga ni kuchagua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…