Ndugu yangu amenipa sharti la kuacha kazi ya kuajiriwa ili anipe mtaji wa Tshs 200M nianze shughuli yangu mwenyewe lakini sijui nifanye shughuli gani!

Ndugu yangu amenipa sharti la kuacha kazi ya kuajiriwa ili anipe mtaji wa Tshs 200M nianze shughuli yangu mwenyewe lakini sijui nifanye shughuli gani!

Sikushauri kuacha kazi, kama mtu unaamua kumpa mtu mtaji na huna mpango wa kumdai kwanini uweke sharti la kuacha kazi? Ukaanzishe biashara huna hada idea nayo unafanya pata potea. Akupe mtaji na kazi usiache.. anzisha biashara kwa kiasi kadhaa then uone biashara inakwendaje ukiwa stable na kuimudu ndo ufikirie kama uache kazi au laa
Anasema eti itanifanya niwe committed - lazima kuwe na fear ya risk ili nijihangaishe sana. Anasema bila kuwa na risk factor watu huwa hawafanikiwi hata siku moja, inakuwa come easy go easy. Anasema ndio maana watu wanaopata fedha kwa njia ya bahati nasibu huwa mara nyingi hawafanikiwi kimaisha - come easy go easy.
 
Anasema eti itanifanya niwe committed - lazima kuwe na fear yarisk ili nijihangaishe sana. Anasema bila kuwa na risk factor watu huwa hawafanikiwi hata siku moja, inakuwa come easy go easy

Kuna watu wameajiriwa na wana biashara zimesimama.. kwani wenye ajira hawana risk katika biashara zao? Akili za kuambiwa changanya na zako
 
Biashara NAYO ni kazi. 200 ml ni mtaji wa maana kabisa unaoweza kubadilisha maisha ya familia yako completely.

Kaa chini na mkeo, mwelimishe faida za kujiajiri .
Ukipata wazo LA biashara mshirikishe na umfanye kuwa partner in business, atakuamini na kuithamini biashara yenu
Shukurani sana. Nimeongea sana na wife. Uzuri ana kazi yake japo hailipi sana. Hofu yake ni kwamba vipi tusipofanikiwa. Anaona ni bora nifanye kazi hadi umri wa kustaafu nitapata angalau 150m. Nmwambia sintakuwa na nguvu za kufanya biashara wakati huo, na nisipofanya kitu cha kuzalisha hazitatutosha.

Ila uzuri ni kwamba tayari tuna kibanda chetu, kwa hiyo hatukai nyumba ya kupanga.
 
Nusu ya hela utayopewa usisahau kujenga nyumba (kama hauna nyumba yako bado), iliyobakia ndio upange hizo mambo za biashara unashauriwa hapa...

(Huu ni ushauri toka kwa mzee)
 
Mara nyingi nimetetea uraia pacha ili wana Diaspora wapewe nafasi za kuwekeza nchini. Sababu kubwa ya kufanya hivyo ni kwamba nina ndugu yangu huko nje alichukua uraia wa huko, na sasa anasema inakuwa vigumu kuwekeza Tanzania kwa kuwa yeye sio raia tena wa Tanzania.

Sasa juzi hapa kanishauri niachane na kazi za kuajiriwa (mshahara wangu ni kama Tshs 1.5m kwa kwenzi). Ananiambia yuko tayari kunipa mtaji wa Tshs 200m kwa shart moja tu, niachane na kazi ya kuajiriwa ili nijikite kwenye kuzitumia hizo Tshs 200m zizalishe. Kaniambia hatanipangia cha kufanya, ni juu yangu, na kwamba kama nikizipoteza pia ni juu yangu, wala hatanidai. Ila hataki anipe hizo hela huku naendelea na kazi ya kuajiriwa.

Naombeni ushauri - kwanza kama ni wazo zuri mie kuacha kazi kwa hiyo Tshs 200m, na kama ndivyo nikiacha kazi nizitumie kwenye biashara gani? Nikiacha kazi, nina mafao yangu ya kama Tshs 70m, kwa hiyo nitakuwa na jumla ya kama Tshs 270m, lakini bado sielewi nifanye shughuli gani. Kilimo? Daladala? Nyumba? Biashara ya mazao? Niziweke tu benki niwe nachukua interest? Au niendelee tu na kazi yangu ya kuajiriwa yenye uhakika wa mshahara kila mwezi?
Acha ubwege
 
Kuna watu wameajiriwa na wana biashara zimesimama.. kwani wenye ajira hawana risk katika biashara zao? Akili za kuambiwa changanya na zako
Nimekuewlewa mkuu, ila sasa huo sio uamuzi wangu. Msimamo wake ni kwamba acha kazi, fanya biashara nitakupa mtaji. La sivyo endelea na kazi yako.
 
Mkuu, sijawahi kufanya hata biashara ya juice au ice cream. Toka nimalize chuo mie mtu wa kuajiriwa tu!
1.Jipe muda (mwezi 1 hadi 3)ufikirie unapenda nini na unaweza nini...ikibidi test hilo wazo lako kbs unachukua likizo unajaribu uone..

2.jiandae na ulimbukeni siku ukipokea hio pesa

3.igawanye makundi hio hela
Mfano
i.Akiba,
ii.mtaji kwa kile utakachochagua na
iii.re-investment ingine nunua shares/bonds

4.fanya siri wakijua watu wengi watakuua
 
1.Jipe muda ufikirie unapenda nini na unaweza nini...

2.jiandae na ulimbukeni siku ukipokea hio pesa

3.igawanye makundi hio hela
Mfano
i.Akiba,
ii.mtaji kwa kile utakachochagua na
iii.re-investment ingine nunua shares/bonds

4.fanya siri wakijua watu wengi watakuua
Very good starting point, shukurani Mkuu. Kwa hiyo unasema nikubali kuacha kazi?
 
Nimekuewlewa mkuu, ila sasa huo sio uamuzi wangu. Msimamo wake ni kwamba acha kazi, fanya biashara nitakupa mtaji. La sivyo endelea na kazi yako.

Something is fishy kwenye huu msaada
 
Pesa bwana unaziona nyingi ukiwa hujazishika ila ukizishika sasa zinayeyuka hata hujui zimepotelea wapi.
 
Tumia akili, badala ufocus kwenye biashara yenye thamani ya 200m uhangaike na kazi ya 1.5m ambayo inakula zaidi ya masaa 8 ya siku nzima
Hicho kihunzi kimoja. Cha pili, niingie kwenye shughuli gani? Kuna mtu kaniambia Tshs 200m ni hela ndogo sana!

Mie mawazo yangu hao ilikuwa niingie kwenye Coaster, nianze na mbili.
 
Very good starting point, shukurani Mkuu. Kwa hiyo unasema nikubali kuacha kazi?
Jipe muda
Jiulize unafanya kazi kwa sababu gani
Hela?heshima?huna options?

And test each theory
Km usingekua na kazi ungefanya biashara gani ungeifanyaje?
Kwanini?unaipenda?utaiweza?
Vyote hivyo ni vitu tofauti

Kitu cha moyoni can go a long way

Jiulize why za kutosha!.,
 
Pesa bwana unaziona nyingi ukiwa hujazishika ila ukizishika sasa zinayeyuka hata hujui zimepotelea wapi.
Yaani kuna jamaa kaniambia exactly maneno haya. Kwamba Tshs 200 ni hela ndogo sana I have to be very careful nisi rush kuamua
 
Back
Top Bottom