Ndugu yangu amenipa sharti la kuacha kazi ya kuajiriwa ili anipe mtaji wa Tshs 200M nianze shughuli yangu mwenyewe lakini sijui nifanye shughuli gani!

Ndugu yangu amenipa sharti la kuacha kazi ya kuajiriwa ili anipe mtaji wa Tshs 200M nianze shughuli yangu mwenyewe lakini sijui nifanye shughuli gani!

Piga mahesabu utakapo tumikia hiyo ajira yako mpk kufika miaka 60 na hapo utakua umekua screpa utalipwa kiinua mgongo mil200 hapo ni ww kuchagua upate mil200 ukiwa kijana au upate mil 80 ukiwa mzee
 
Shukurani sana. Nimeongea sana na wife. Uzuri ana kazi yake japo hailipi sana. Hofu yake ni kwamba vipi tusipofanikiwa. Anaona ni bora nifanye kazi hadi umri wa kustaafu nitapata angalau 150m. Nmwambia sintakuwa na nguvu za kufanya biashara wakati huo, na nisipofanya kitu cha kuzalisha hazitatutosha.

Ila uzuri ni kwamba tayari tuna kibanda chetu, kwa hiyo hatukai nyumba ya kupanga.

Duh wote mmekutana waoga sana
Mungu awaongoze
 
Very good starting point, shukurani Mkuu. Kwa hiyo unasema nikubali kuacha kazi?

Acha kazi without a doubt
Lakini usikurupuke
Uwe na plan nini na nini utafanya na fanya utafiti wa kutosha
Pesa zigawe kwa mafungu
Ingekuwa mimi biashara zote ningetumia mtaji usizidi mil 30
Speaking from experience biashara zote nilianza na mtaji below 10M na nikakuza mtaji
Huwa nashauri hata kama mtu ana access na pesa nyingi asianze na pesa nyingi utajikuta umefanya vitu unnecessary
Unatakiwa uanze mdogo usome biashara ilivyo ndio uingize pesa zako sasa
So 200M ni nyingi sana inakupa nafasi ya kufanya kuanguka kujifunza na kufanya tena kwa ukweli
 
Huyo una ugomvi anataka kukuangamiza huku unacheka nae. Sasa ukiacha kazi asipokupa utapata wapi kazi?? Usikubali kutapeliwa kijana
 
Huyo una ugomvi anataka kukuangamiza huku unacheka nae. Sasa ukiacha kazi asipokupa utapata wapi kazi?? Usikubali kutapeliwa kijana
Mkuu, huyu sio rafiki, ni ndugu yangu ambae si mara ya kwanza anani-support. Kwake USD100,000 sio jambo kubwa.
 
Sawa huyo ni ndugu yako. Lakini huwezi jua anafikiria nini juu yako. Mwambie nimeacha kazi na nimefikiria kazi ya kufanya ya mazao. Ila utaacha kazi baada ya kupewa hiyo pesa.
 
Hujawahi fanya biashara ndio maana. Hapo una hofu kibao ya kushindwa. Sikuambii ni ipi. Nakushauri tafuta mtu aliyefanikiwa katika biashara na unaemumini awe mentor wako. Hela zipo katika biashara ndugu. Na hiyo biashara ni ile ambayo mwenyewe unashiriki sio ambao hujui chochote.

Safi
Kuongeza mentor ni mtu ambae sio tu unamuamini ila na yeye yupo tayari kukufungulia siri zote bila kuwa na uwivu na wewe
Isijekuwa wewe una hesabu mtu fulani ni mentor wako lakini yeye anakuona ni competitor wake
All in all kuwa na mentor ni muhimu haswa kwa mleta mada
 
watu wengi wanafikiri kujiajiri ni kazi rahisi sababu tuu wamepata hela. Hii ndo inawacost watu wengi sana kwenye kujiajiri. Ukishupaa na hizo 200M ukaacha kazi kiboyaboya unakuwa kichaa sio muda.
 
Mara nyingi nimetetea uraia pacha ili wana Diaspora wapewe nafasi za kuwekeza nchini. Sababu kubwa ya kufanya hivyo ni kwamba nina ndugu yangu huko nje alichukua uraia wa huko, na sasa anasema inakuwa vigumu kuwekeza Tanzania kwa kuwa yeye sio raia tena wa Tanzania.

Sasa juzi hapa kanishauri niachane na kazi za kuajiriwa (mshahara wangu ni kama Tshs 1.5m kwa kwenzi). Ananiambia yuko tayari kunipa mtaji wa Tshs 200m kwa shart moja tu, niachane na kazi ya kuajiriwa ili nijikite kwenye kuzitumia hizo Tshs 200m zizalishe. Kaniambia hatanipangia cha kufanya, ni juu yangu, na kwamba kama nikizipoteza pia ni juu yangu, wala hatanidai. Ila hataki anipe hizo hela huku naendelea na kazi ya kuajiriwa.

Naombeni ushauri - kwanza kama ni wazo zuri mie kuacha kazi kwa hiyo Tshs 200m, na kama ndivyo nikiacha kazi nizitumie kwenye biashara gani? Nikiacha kazi, nina mafao yangu ya kama Tshs 70m, kwa hiyo nitakuwa na jumla ya kama Tshs 270m, lakini bado sielewi nifanye shughuli gani. Kilimo? Daladala? Nyumba? Biashara ya mazao? Niziweke tu benki niwe nachukua interest? Au niendelee tu na kazi yangu ya kuajiriwa yenye uhakika wa mshahara kila mwe

Usithubutu; uje unishukuru baadae; bora 10,000 yako mwenyewe kuliko 1m ya mtu! I talk with experience!
 
Kumbe mkeo ameshakushauri boss..!? Sasa unataka sisi huku tukuvunjie ndoa aiseeh!
Mkuu, mke wangu anaelewa wazi kwamba pale asipokubaliana jambo na mimi haina maana lazima nifuate anachotaka yeye. Kuna wakati nafanya ninachotaka mimi tofauti na anachotaka yeye. Ndio kuna wakati nitafanya anachotaka yeye tofauti na ninachotaka, lakini sio siku zote. Kwa mfano, ingekuwa issue ni yeye kuacha kazi akapinga, nisingemlazimisha, lakini issue ni mimi kuacha kazi, hivyo sio lazima nifuate anachotaka. At the end of it all, mimi ndio captain wa familia.
 
Mkuu, huyu sio rafiki, ni ndugu yangu ambae si mara ya kwanza anani-support. Kwake USD100,000 sio jambo kubwa.
Kwaani ukimdanganya umeshaacha kazi ili aweke kabisa huo mzigo inawezekana?? Maana ukipata hiyo pesa humu ndani kuna wafanyabiashara wengi na wanayo mawazo mazuri ila wanakosa kuchangia maana wanaona unazingua.
 
Basi jitafakari
Unapenda au hupendi hio kazi?
Inakutesa ama haikutesi
Ina future nzuri au la?

Mkuu, lazima nikiri kwamba sifanyi kazi yangu kwa kuwa naipenda, bali kwa kuwa inaniwezesha kukidhi mahitaji ya familia ya kila siku - yaani inatosheleza kula, kuvaa na kulala, na pia naimudu vizuri. Kama ingekuwa suala lakufanya kazi ninayoipenda basi ningependa niwe pilot nirushe Dreamliner za ATCL!
 
Kwaani ukimdanganya umeshaacha kazi ili aweke kabisa huo mzigo inawezekana?? Maana ukipata hiyo pesa humu ndani kuna wafanyabiashara wengi na wanayo mawazo mazuri ila wanakosa kuchangia maana wanaona unazingua.
Nitamdanganya ndugu yangu ambae kila siku tuko pamoja kama jamaa moja? Na atakapojua nimemdanganya itakuwaje? Nadhani gharama ya uhusiano kati yangu na ndugu yangu ina thamani sana kuliko Tshs 200m. Nina principles Mkuu
 
Ni hela nzuri, ila salary yako pia ni nzuri.

Mwambie akupe hiyo hela ila kazi utaacha in one year.

Ufanye research kitu cha kufanya huku ukiwa kazini.

let's say,

ujenge chuo cha kufundisha nursing / medical assistants;

ujenge shule .a. level

ujenge hospital, private

Uwe na mtu wa kufuatilia vibali

Unless otherwise ... ukandarasi
 
Hapa ndo Tanzania bro
Mtengenezee fake papers..

Akija unachuka likizo unakaa kwny ile biashara ndogo uloanzisha

Mfano mini supermarket...
Wenye uzoefu watasema
mkuu mbona unakosa uaminifu hata kwenye ideas?.uaminifu na ukweli ni kitu muhimu na cha kwanza kwenye kila kitu iwe biashara au ajira....wizi, utapeli, uongo-uongo hautakufikisha mbali..ni jambo la muda mfupi tu lenye hasara kubwa mbeleni.

Vijana wa Tz tujifunze kuwa honest kwa mafanikio sustainable na yenye baraka za Mungu.
 
Mara nyingi nimetetea uraia pacha ili wana Diaspora wapewe nafasi za kuwekeza nchini. Sababu kubwa ya kufanya hivyo ni kwamba nina ndugu yangu huko nje alichukua uraia wa huko, na sasa anasema inakuwa vigumu kuwekeza Tanzania kwa kuwa yeye sio raia tena wa Tanzania.

Sasa juzi hapa kanishauri niachane na kazi za kuajiriwa (mshahara wangu ni kama Tshs 1.5m kwa kwenzi). Ananiambia yuko tayari kunipa mtaji wa Tshs 200m kwa shart moja tu, niachane na kazi ya kuajiriwa ili nijikite kwenye kuzitumia hizo Tshs 200m zizalishe. Kaniambia hatanipangia cha kufanya, ni juu yangu, na kwamba kama nikizipoteza pia ni juu yangu, wala hatanidai. Ila hataki anipe hizo hela huku naendelea na kazi ya kuajiriwa.

Naombeni ushauri - kwanza kama ni wazo zuri mie kuacha kazi kwa hiyo Tshs 200m, na kama ndivyo nikiacha kazi nizitumie kwenye biashara gani? Nikiacha kazi, nina mafao yangu ya kama Tshs 70m, kwa hiyo nitakuwa na jumla ya kama Tshs 270m, lakini bado sielewi nifanye shughuli gani. Kilimo? Daladala? Nyumba? Biashara ya mazao? Niziweke tu benki niwe nachukua interest? Au niendelee tu na kazi yangu ya kuajiriwa yenye uhakika wa mshahara kila mwezi?
Usiache kazi. Natumaini unajua Hali ya biashara ilivyo tete na isiyoeleweka. Tshs 200M utasema ni nyingi, Ila laana iliyopi ndani ya nchi yetu, zitapukutika na usifanye lolote, hivyo kuwa muangalifu sana, na kama ni kuwekeza, fanya kidogo kidogo. Maeneo gani ya kuwekeza, Hilo ni la kufanya utafiti wa kina, maana sijaona biashara yoyote yenye uhakika Tz.
 
Kwa hiyo ndugu yako Mr. Synthesizer anaona hawezi kuwekeza Tanzania sababu yeye "siyo raia"!!
Sisi weusi Kuna mahali tunafurahisha. Wakati ngozi nyeupe wanamiminika hapa nchini wanafanya vitu vya kuishi miaka 100, mweusi anasema siyo raia.
Kuna Wanetherland wanalima mboga mboga miaka nenda rudi, Kuna Kaburu wanamiliki ranch miaka kibao mpaka Wana supply nyama, Kuna mwingereza anafuga ng'ombe, Kuna mwingereza analima Parachichi za kumwagilia, Kuna Kaburu wanamiliki misitu ya miti miaka kibao, Kuna Wachina wanamiliki viwanda vya marine fiber board, Kuna Wachina wanamiliki viwanda vya kukoboa mpunga. Mwaka Jana mwishoni Kuna raia ya Australia alikuja anahitaji hecta 2,000 akafuge ng'ombe.
Huyu hapa (kwenye picha) katoka Egypt anatafuta ardhi akalime, hapo nipo naye Kijijini ndanindani huko tunaongea na kamati ya ardhi ya Kijiji, halafu ngozi nyeusi anasemaje vile!!! Yeye siyo raia hawezi kuwekeza!!!
PhotoGrid_1641137411086.jpg
 
Back
Top Bottom