Ndugu yangu Diamond Platinumz wekeza haraka sana, maisha ya wanamuziki wa Tanzania hugeuka shubiri haraka

Hivi punde

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2017
Posts
2,554
Reaction score
8,587
Diamond ndugu yangu. Hongera kwa kazi nzuri unazopata na network ya kimuziki unayoipata huko duniani Mungu akubariki sana.

Katika chenji zako unazopata kumbuka kuwekeza miradi mingine ya kiuchumi ili usiingie kwenye kasumba iliyozoeleka ya wasanii (hususani wanamuziki) wa kitanzania ambao huishiwa pumzi na kufulia haraka sana na kugeuka ombaomba mtaani.

Hatukuombei mabaya ila angalia tu wenzio(walio wengi) huko walikotoka na hali yao ya maisha kwa sasa. Wamechoka sana. Mfano ipo mingi sana.Na ndo maana kuna wasanii wanabadili gear angani mf Prof Jay Mr II Jokate Masanja nk.

Maana ukifulia na huo mdomo sijui utaonekanaje huko Mbagala.

Please nisiki mm kaka yako.
 
Kumbe wewe Me uandishi wako ulikuwa unanituma nikufikirie wewe Ke.
 
Sielewi unamuoneaje huruma mtu humjui hakujui mpaka unaamua kumpa ushauri ambao yeye tayari anautekeleza kwa miaka sasa.

Lebo ya wcb na wasanii walio chini ya hiyo lebo ni uwekezaji mkubwa kuliko karanga maana zilishapondwa kua zina chumvi nyingi na zipo tangu kitambo wala pafyumu iliyolaumiwa kua ni bei ghali.

Aisee kuna wadau mna moyo.
 
Diamond karanga , chibu perfume, wasafi.com kwa ajili ya kuuza nyimbo (uwekezaji mkubwa kama unajua maswala ya IT utaelewa) , wasafi label na studio, wasafi clothline , wasafi studio kwa ajili ya kupiga picha nk bado hapo yy mwenyewe balozi Coca, VODA, bellarie, GSM mall na partnership kati ya safaricom ya kenya na WCB nk, upande wa uwekezaji kafanikiwa sasa ww sijui unataka uwekezaji gani,. Huo ushauri wape wasanii wengine si diamond na mda si mrefu anaingiza bidhaa nyingine sokoni. Mimi ushauri wangu diamond platnumz ulikuwa ni kutoa album na naona mda si mrefu ataito album yake Boy from tandale.
 
nazani unaamini uwekezaji ni kujenga nyumba tu.. tena uwe unaziona..

diamond ana nyumba zaidi ya tano.. ana kampuni WCB.. ana share karanga.. amezaa na zari watoto wao tu ni biashara kubwa... unataka awekeze kwenye nini... au hadi anunue malori??
 
Mambo gani labda kwa mfano?
kila siku anatoa nyimbo zenye video expensive,unataka kuniambia hizo nyimbo zinampa return inayotakiwa? mimi nadhani diamond jina lake na music wake ni mkubwa kuliko hela anayoingiza. labda apige show tu na hela yenyewe ya show ina chawa kibao .mameneja watatu wapate mgao sio mchezo
 
Nyimbo zenye video si anauza lakini?

Unajuwa Michael Jackson aliwekeza kiasi gani kwenye video ya Thriller na unaona uwekezaji ule ulivyokuja kumlipa?
 
diamond anatoa video nyingi sababu ya hela za youtube ndio zinamtengenezea video.. akipiga views milion 10 kwa video moja.. tayari amesharudisha hela ya video... shows kwake inakuwa faida..

na hapo hapo akipiga show moja tu anarudisha hela... na wale mameneja diamond ni kawaajiri... sio kama wao wamemuajiri.. hata hela anawapangia yeye wapate bei gani

 
Nyimbo zenye video si anauza lakini?

Unajuwa Michael Jackson aliwekeza kiasi gani kwenye video ya Thriller na unaona uwekezaji ule ulivyokuja kumlipa?
kweli soko la enzi za michael jackson utalilinganisha na soko la kipindi hiki tena hapa bongo?
wenzetu mbele wana tabia ya kununua album za wasanii wao.hapa bongo nani ananunua zaidi ya kutumiana kwenye whatsup? wakikusaidia sana watacheki you tube na kukupa like moja.mimi nadhani mond anawekeza sana kukuza jina hila hapati return yoyote .watu wanamponda sana kiba ila nadhani jamaa ana akili sana akitoa wimbo mmoja anahakikisha umerudisha hela yake ndo anatoa mwingine.nadhani hyo ni good strategy maana music ndo kazi yake sio kufurahisha tu watu
 
view moja you tube analipwa sh ngapi?
 
Mara ngap sasa,
Kuna slogan innasema it begins with you, ni vyema ukajitathmin kwnz ww na hatua ya maisha ulofikia
 
view moja you tube analipwa sh ngapi?

kila views 1000 wanalipwa usd 2...

akipata views milion 10 mfano ambayo ndio average kwa video za diamond anazopataga.. analipwa na youtube usd 20,000 ambayo inatosha kabisa kutengeneza video south africa na chenji inabaki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…