Ndugu yangu nimemtafutia kazi mshahara laki 3, anaikwepa, nimefowadiwa meseji zake anadai ninamnyanyasa. Nifanye nini?

Cry baby huyo , a. K. a mtoto wa mama atakusumbua sana .. kuishi na watu ni kazi mnooo
 
Kamaliza chuo mwaka juzi ila hadi sasa hana shughuli, alikuja hapa mjini pasaka mwaka jana ila nikamwambia abaki baki ajiskie huru hasa ukizingatia nyumbani kwangu kuna vyumba vya nje kwa hio haikuwa taabu kumuhifadhi. Sina ubaya wala hila, mimi kila wiki huwa nampa 50 kwajili ya matumizi, sifanyagi hivi kwa ndugu wengine ila kwa kuwa yeye mama yake alikuwa akinisaidia mara kwa mara kiuchumi nilipokuwa chuoni, basi huwa ni kama narudisha fadhila tu na hata hiyo 50 haijawahi kunipa mawazo kumpa.

Alikuwa ananiambia ana apply kazi serikalini lakini kwa hali ilivyo nilimwambia ajira zilekuwa ngumu hivyo nimtaftie, ni kama mara 2 hivi nilitaka kumsaidia mchongo ila alikuwa anakazia kwamba kuna interview anakaribia kuitwa.

Basi mimi nikaamua nimtaftie kazi sehemu ya mtu tunaejuana, tuna undugu kwa mbali, sehemu ile kazi huwa ni jumatatu hadi ijumaa saa 1 na nusu hadi saa 12 jioni.. na jumamosi huwa ni saa tatu hadi saa saba hivi.

Mshahara ni laki 3 na kitu ila haujazidi 350k, kila jumamosi kuna posho ya weekend, nadhani itakuwa kati ya elf 10 hadi 15

Sasa nilipompa hii habari ni kama hajaichukulia vizuri, alipoanza kuniambia nisubiri subiri kuna interview anaisikilizia nikamwambia wala asiwe na hofu, akiitwa kwenye interiew ataenda ila hii kazi inabidi aianze, kiukweli kwa jinsi alivyochukulia hisi suala ni wazi kabisa ni kama vile haitaki.

Jana ndio nimefowadiwa meseji screenshot analalamika kwamba namfanyia manyanyaso kwamba kazi ina muda kidogo wa kupumzika, malipo kidogo, n.k.
Hiyo 50 ya kila wiki isitishe.
 
Mm nina mdogo wangu kamaliza chuo mwaka juzi huwa simpi hata mia,namwambia akaze tyakko kutafuta pesa zake.

Hawa vijana wa dot com wanapenda maisha laini laini kwa hiyo na ww ukionesha kumjali kwa mambo yasiyo ya lazima wanabweteka sana.

Akili kichwani kwako usilee mtu mzima tena wa kiume asiye jiongeza.
 
Kamaliza chuo mwaka juzi ila hadi sasa hana shughuli, alikuja hapa mjini pasaka mwaka jana ila nikamwambia abaki baki ajiskie huru hasa ukizingatia nyumbani kwangu kuna vyumba vya nje kwa hio haikuwa taabu kumuhifadhi. Sina ubaya wala hila, mimi kila wiki huwa nampa 50 kwajili ya matumizi, sifanyagi hivi kwa ndugu wengine ila kwa kuwa yeye mama yake alikuwa akinisaidia mara kwa mara kiuchumi nilipokuwa chuoni, basi huwa ni kama narudisha fadhila tu na hata hiyo 50 haijawahi kunipa mawazo kumpa.

Alikuwa ananiambia ana apply kazi serikalini lakini kwa hali ilivyo nilimwambia ajira zilekuwa ngumu hivyo nimtaftie, ni kama mara 2 hivi nilitaka kumsaidia mchongo ila alikuwa anakazia kwamba kuna interview anakaribia kuitwa.

Basi mimi nikaamua nimtaftie kazi sehemu ya mtu tunaejuana, tuna undugu kwa mbali, sehemu ile kazi huwa ni jumatatu hadi ijumaa saa 1 na nusu hadi saa 12 jioni.. na jumamosi huwa ni saa tatu hadi saa saba hivi.

Mshahara ni laki 3 na kitu ila haujazidi 350k, kila jumamosi kuna posho ya weekend, nadhani itakuwa kati ya elf 10 hadi 15

Sasa nilipompa hii habari ni kama hajaichukulia vizuri, alipoanza kuniambia nisubiri subiri kuna interview anaisikilizia nikamwambia wala asiwe na hofu, akiitwa kwenye interiew ataenda ila hii kazi inabidi aianze, kiukweli kwa jinsi alivyochukulia hisi suala ni wazi kabisa ni kama vile haitaki.

Jana ndio nimefowadiwa meseji screenshot analalamika kwamba namfanyia manyanyaso kwamba kazi ina muda kidogo wa kupumzika, malipo kidogo, n.k.
Ni bush comer au mtoto wa town?
 
Wala shida sio hiyo 50 unayompa. Huyo bado anajiona ni mdogo yaani anajiona anastahili kulishwa.Shida ni kichwani kwake. Hata husingekuwa unampa 50 angekataa pia kwa vile tu ana pa kulala na kula.
 
Kamaliza chuo mwaka juzi ila hadi sasa hana shughuli, alikuja hapa mjini pasaka mwaka jana ila nikamwambia abaki baki ajiskie huru hasa ukizingatia nyumbani kwangu kuna vyumba vya nje kwa hio haikuwa taabu kumuhifadhi. Sina ubaya wala hila, mimi kila wiki huwa nampa 50 kwajili ya matumizi, sifanyagi hivi kwa ndugu wengine ila kwa kuwa yeye mama yake alikuwa akinisaidia mara kwa mara kiuchumi nilipokuwa chuoni, basi huwa ni kama narudisha fadhila tu na hata hiyo 50 haijawahi kunipa mawazo kumpa.

Alikuwa ananiambia ana apply kazi serikalini lakini kwa hali ilivyo nilimwambia ajira zilekuwa ngumu hivyo nimtaftie, ni kama mara 2 hivi nilitaka kumsaidia mchongo ila alikuwa anakazia kwamba kuna interview anakaribia kuitwa.

Basi mimi nikaamua nimtaftie kazi sehemu ya mtu tunaejuana, tuna undugu kwa mbali, sehemu ile kazi huwa ni jumatatu hadi ijumaa saa 1 na nusu hadi saa 12 jioni.. na jumamosi huwa ni saa tatu hadi saa saba hivi.

Mshahara ni laki 3 na kitu ila haujazidi 350k, kila jumamosi kuna posho ya weekend, nadhani itakuwa kati ya elf 10 hadi 15

Sasa nilipompa hii habari ni kama hajaichukulia vizuri, alipoanza kuniambia nisubiri subiri kuna interview anaisikilizia nikamwambia wala asiwe na hofu, akiitwa kwenye interiew ataenda ila hii kazi inabidi aianze, kiukweli kwa jinsi alivyochukulia hisi suala ni wazi kabisa ni kama vile haitaki.

Jana ndio nimefowadiwa meseji screenshot analalamika kwamba namfanyia manyanyaso kwamba kazi ina muda kidogo wa kupumzika, malipo kidogo, n.k.
Mfukuze
 
Usimpe Tena hiyo 50k mtoto umleavyo ndivyo akuwavyo stop that token right away utanishukuru
 
Huyo anakuletea jeuri tu hana lolote, anakwepa kazi yako ili apate alaiyotafuta yeye ila baadae ajekusema ulimnyanyasa sana japo wazaz wake walikusaidia...

Samahan lakin naomba niseme unafanya upumbav kumpa 50k kila wiki kwa mtu jobless hiyo pesa ni nyingi sana, that's means una afford kumpa 200k kwa mwezi, si mshahara kabisa wa mtu anae nyonga tai yupo ofisini embu mpotezee kula kulala na kunya kwako inamtosha. Ukiacha kumpa hela 3 months yeye mwenyew atakuambia anataka kaz yoyote...
 
Ajabu ni kuwa anaetunga huu uzi hana kazi ila anamtafutia asie na kazi kama yeye alipo mda huu sebleni kwa kaka ake akiangalia tamthilia ya huba [emoji1][emoji1][emoji1]jamii forum kila mtu ana pesa dah [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom