Ndugu yetu alitaka kuwa tajiri kama Laizer kwa madini amefariki kazini

Ndugu yetu alitaka kuwa tajiri kama Laizer kwa madini amefariki kazini

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Afariki kwa kupondwa jiwe kichwani akichimba madini.

Mkazi wa Kijiji cha Masungura wilayani Meatu, Simiyu Michael Salum (30), amefariki dunia kwa kupondwa na jiwe kichwani wakati akichimba dhahabu ndani ya duara katika machimbo ya Mwakitolyo, wilayani Shinyanga.

Ofisa Madini Mkoa wa Shinyanga, Joseph Kumburu, akizungumza hivi karibuni na wachimbaji wadogo wa Mwakitolyo, alisema kuwa tukio hilo limetokea Julai 17, mwaka huu na kuwa ajali hiyo ilitokea katika kitalu cha wachimbaji wadogo wa namba 5.

Kumburu alisema ajali hiyo imetokea majira ya saa 6:00 mchana wakati wachimbaji zaidi ya watano walipokuwa wakitoka ndani ya duara baada ya kumaliza kazi.

Kumburu alisema, kwa mujibu wa Mtaalam wa afya aliyekuwa kwenye uchunguzi huo, mtu huyo alipasuka kichwani na kusababisha umauti kutokana na kuanguka kutoka umbali wa mita 20, baada ya kuteleza na jiwe kumponda kichwani na kusababisha kifo chake.

“Marehemu hakuwa na majeraha yoyote zaidi ya kupasuka kichwa, niwashauri tu ndugu zangu wachimbaji muhakikishe mnazingatia taratibu na sheria za uchimbaji mnazoelekezwa na wataalamu wenu ili kufanya shughuli hizo kwa hali ya usalama zaidi kwa kuwa chanzo cha tukio marehemu alikosa nguvu,” alisisitiza Kumburu.

Kutokana na ajali za mara kwa mara zinazotokea kwenye machimbo hayo, Ofisa Madini huyo alifunga eneo kulipotokea ajali kwa siku tatu kupisha ukaguzi.

Kumburu aliandaa timu ya wataalam kutoka Ofisi ya Madini, kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Salawe pamoja na Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Shinyanga ili kusimamia ukaguzi huku akishauri hatua za haraka za kuchukuliwa kwa maduara yote yatakayobainika kuhatarisha maisha ya watu.

Ofisa Madini Kumburu aliwataka wachimbaji hao kuzingatia Sheria za madini na maelekezo wanayopewa na wakaguzi kufukia mashimo yote ambayo yameachwa wazi ili kuepusha ajali.

Chanzo: Nipashe
 
Wanasema duara likiua ndio 'shimo linatema' madini ya kutosha
 
linakuwaje hilo duara kwa sisi tusiolijua na linatishaje?
1595231470558.png
 
linakuwaje hilo duara kwa sisi tusiolijua na linatishaje?
Mkuu nashindwa nikueleeze vipi ila inshort unazama kwanza kama kaburini, ngazi ni vipange vya magogo vilivyo kutani.

Kisha unapata horizontal tunnel ambapo nyingi hazina reinforcements hivyo mzigo ukishuka unashuka mazima

Nyingine ni ndefu sana kwenye chini na ni risky sana kwa kuwa wengi hawazingatii safety rules.

Picha hapi chini ndio tulikua tushazama sasa tuanze kwenye huko manta kuisakanya dhahabu
FB_IMG_1595231389558.jpg
 
Umetuhabarisha ahsante kilicho haribu ni kichwa cha habari.Huyu jamaa alikuwa mchimbaji kabla hata Laiser hajapata yale madini kilo nyingi kingine nikuambie usije dhani Laiser hizo bilioni saba ndio zimempa utajiri.Laiser ni tajiri siku nyingi ana hoteli ya kitalii na mifugo lukuki
 
machimbo ya Mwakitolyo ni zamani kinoma, ila yamewatoa vijana wengi tuu, mjini usione vijana wanaendesha ma -range sport, BMW x6 new model, kaa ukijua wame hustle kweli kweli………………..
 
Back
Top Bottom