Tetesi: Ndugu yetu Hasheem Thabeet anarejea NBA


I agree, mchezo umebadilika sana ingekuwa zaman ingekuwa vigumu mno kwa mtu kama Curry kuwa mvp, kinachoniumaga ni kwamba Hasheem yupo na physic kama ya kina KD, Bosh na the likes mbona kina KD wanaupiga mwingi sana, unajua mwingi mpaka unashangaa.....


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Alicheza dakika ngapi? Maana NBA nako unaweza kusajiliwa timu ukawa benchwarmer muda mrefu sana. Unasubiri mtu aumie, uwe kiraka, na mtu haumii.

Ni siku mingi sana 2011 kama sikosei ila nakumbuka ilikuwa game mbil ndio alicheza mkuu


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Wanaoijua game watakuelewa sana.
Siku hizi si zama za Shaq, Rashid Wallace, Yao n.k. Watu wanafanya yao nje ya arc. Center anatakiwa azuie lakini pia awe na uwezo wa ku-shoot kutoka popote si kuchutama chini ya ring.

Sifa moja ya Kobe ni uwezo wa ku-shoot akiwa ndani, nje ya arch au ku-attack ring kutokea popote. Uwezo huo anao KD, Curry, Westbrook, Haden, Kahwi na Anto. n.k.

Wachezaji wanabadilika sana si zama za Shaq kusubiri chini, siku hizi mchezaji anatimia idara zote. Kinyume cha hapo mchezaji atabaki kugawa maji katika bench halafu kupotezewa
 
Hapo kuna Basic na Extra skills. Ndugu yetu nathubutu kusema alikuwa na Basic Skills ambazo kila mchezaji kwa nafasi yake anayocheza alikuwa nazo. Saizi tunahitaji mtu mwenye both basic and extra skills. Watu kama akina KD, Giannis, Jokic licha ya kuwa na miili ya aina Ile, ila unaweza ukawachezesha kama Point Guards na bado ukapata matokeo unayoyataka.
 
Umenena vyema mkuu.
 
Siku hizi wanawafundisha hivyo tangu watoto wa miaka 7 naona nikienda kwenye mazoezi yao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Yaaah this is very true, ndugu yetu ndio ivyo yan, kawaida sana


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Tarehe 16/ 08/ 19 niliandika hivyo hapo juu wakati Hasheem Thabeet na Carmelo Anthony wanapenda kwenye workout Knicks na Bucks.

Rudia kusoma
 

kitu kilikuwa kinanikasirisha kuliko vyote ni kwamba Rajon Rondo na Yesaya Thomas wana stats kubwa kuliko Hasheem roho ilikuwa inauma kweli daaah noma kaka


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
kitu kilikuwa kinanikasirisha kuliko vyote ni kwamba Rajon Rondo na Yesaya Thomas wana stats kubwa kuliko Hasheem roho ilikuwa inauma kweli daaah noma kaka


Sent from my iPhone using JamiiForums
Haha ! Rajon Rondo alikuwa moto sana wakati wake. Ni watu waliofanya NBA iwe na msisimko kutokana na majonjo yake uwanjani. Naye kwa sasa kutokana na aina ya uchezaji wake as a Traditional Point Guard ambao kwa wakati ule walikuwa na jukumu moja tu la kuchezesha timu, amejikuta akizungumza timu kadhaa na hata kutokuwa chagua la kwanza kutokana na mapinduzi katka game yaliyoketwa na akina Steph Curry.


Isaiah Thomas, licha ya uandunje wake katika ligi, alikuwa na mambo kadha wa kadha aliyokusudia kuionesha dunia na bahati nzuri alifanikiwa kuyaonesha, japo majeraha yamemrudisha nyuma kwa sasa.

Hapa tunapata funzo kwamba, kimo chako kitakufungulia milango ya fursa, Ila what you bring at the table is what will build your legacy, something our fellow Tanzanian failed to deliver.
 

Isaya nikimwangaliaga na zile injury namwonea huruma ila at least wao wamedumu kwenye game na walikuwa wanapafomu


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Isaya nikimwangaliaga na zile injury namwonea huruma ila at least wao wamedumu kwenye game na walikuwa wanapafomu


Sent from my iPhone using JamiiForums
Sema andunje mdomo nae unaigharimu Career yake. Tangu aondoke Boston hajawahi kukubaliana na hali kwamba timu aliyoitolea sadaka haikuwa na shukrani kwake ikaamua kumuuza, hivyo a-move on. Amekuwa akiishi kwenye mafanikio aliyoyapata kabla ya kuumia na hicho ndio kinapelekea kuwa msafiri saizi from Boston to Cleveland, from Cleveland to Lakers, from Lakers to Utah, from Utah to Washington.

Angeiga mfano wa akina Kawhi ambaye licha ya kadhia alizozipata kutokana na majeraha aliweza kurudi imara na hata kuiongiza timu yake kuchukua Ubingwa.
 
Angeiga mfano wa akina Kawhi ambaye licha ya kadhia alizozipata kutokana na majeraha aliweza kurudi imara na hata kuiongiza timu yake kuchukua Ubingwa.
Kawhi ana sifa tunazoongelea. Kwanza, ana umbo kubwa linalomasaidia katika kulinda. Pili, ana uwezo wa kuchezesha kama point guard. Tatu anapiga field goal iwe 2 au 3. Nne, ana shoot hivyo ukimfanyia foul unaumia tu.

Ukitaka kuona wachezaji waliobadili NBA mfano ni Lebron. Naye ni kama Kawhi kwa umbo na sifa za kuhodhi mpira au kuchezesha wenzake, anachukua rebounds na ana shoot vizuri sana.

Lakini maumbo si lazima yawe makubwa. Mtazame Curry, ana umbo dogo. Kinachomsaidia ni uwezo wa ku score akiwa nje, ndani ya ring au free throw. Curry anachezesha timu ni ngumu kujua kama anatoa pasi au anafunga mwenyewe.

Mfano wa Curry ni Lowry wa Raptor au Westbrook. Maumbo si makubwa lakini wanadungua kutoka popote halafu anaweza ku attack ring wakati huo huo wanalinda.

Russel Westbrook watu wana mu-over rate, si point guard kihivyo hata sasa anasafiri nyota ya Haden.Huyu alikuwa na KD, OKCna mara zote walishindwa kuchukua Ubingwa.

Kiranga watu wanausoma mchezo na wamebaini NBA si urefu wa akina Yao au Tim Duncan
Utaona wachezaji kama Pascal Siakam sasa wanatumia field goal badala ya kuvamia ring.
 
Ni kweli kabisa mkuu. Nilipotoa huo mfano wa Kawhi, nilikuwa nazungumzia kesi ya andunje Isaiah Thomas, ambaye tangu aumie akiwa Boston Celtics na kuuzwa na timu yake ni kama vile ameshindwa kuukubali ukweli na ku-move on, ameshindwa kutambua muda unaenda hivyo ajipange upya na aweze rejea kwa namna nyingine. Badala yake amekuwa ni muongeaji sana kuliko mtendaji, amekuwa akiishi kwenye mafanikio aliyoyapata kabla ya majeraha na kusahau kuishi wakati aliopo, hali inayofanya awe anabadili tu timu kila msimu, kutoka Boston kwenda Cleveland, Cleveland kwenda Lakers, kutoka Lakers kwenda Utah na Utah mpaka sasa Washington.

Kawhi aliweza baada ya kupata majeraha na kutocheza karibia msimu mzima alijipanga vizuri, ndipo baada ya kurudi aliiiongoza timu yake ya Toronto kwa wakati huo kuchukua Ubingwa pasipo kuwa muongeaji zaidi ya mtendaji na kutoishi kwenye mafanikio yake ya nyuma.
 

Kanaongea sana kajamaa kanagombana hadi na mamamba kama kina Rebron alafu hadi vitoto vyake vinamdomo kwene media me nliangaliaga documentary yake fulan ivi yan daah toka aondoke celtics alikasirika na akawa anatema shyt sasa mambo ya mpira hayapo ivyo


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Hasheem ni kama jamaa fulani somebody Nditi ( alikuwa Chelsea ) ana vijitabia fulani vya kiswahili, basi kazi yake ikawa ni kuvimba tu, kujiona ushamaliza.

Ubitozi na Starehe huku ukiendekeza ustar njaa ukirudi bongo. Ukipigwa chini ndio basi tena
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…