Tetesi: Ndugu yetu Hasheem Thabeet anarejea NBA

Tetesi: Ndugu yetu Hasheem Thabeet anarejea NBA

Usiposifia utaitwa mchawi kama vile anayesifiwa ni Malaika ambapo hawezi kuwa na kasoro zozote zile kibinadamu.
Wenye hekima walisema ukiwa nyota kiwango kilekile cha sifa unazopewa unapofanya vizuri kitakua Sawa na kiwango cha lawama/matusi ukivurunda.
Ila sisi waswahili tunataka kusifiana tuu hata kama hamna cha kusifu
 
Kwa wakwanza siotabu ,mwendelezo unakuaje.
Na hicho tu ndio kinachoonekana na haters .. juhudi zake zote za kupambana zilizomfanya kuwa Mtanzania wa kwanza kucheza NBA huwa hatuzioni na wala hatutaki kujifunza kupitia yeye ..
 
Ngoja tuone lakini jamaa alichezea shilingi chooni ikadumbukia,michezo kama hiyo inahitaji mazoezi sana sasa yeye mda mwingi alikuwa anashinda clubs TZ mara kapigana na TID,Kugegeda hovyo na kina jokate,mda mwingi anashinda kwenye vituo vya redio na TV,ajifunze ingawa nina imani alishafika Peak yake huyo mtu.
Kamgonga hadi jokate
 
Ndugu yako wewe na nani hanijui na wala simjui
Ataonekana tena akichezea Milwaukee Bucks.ndugu yetu bado anaendelea kupambana na wachambuzi wanasema yupo kwenye good shape ya kuweza kumudu mikiki mikiki ya NBA.

wabongo tuache unafiki wa kumbeza ndugu yetu huu mchezo alijifunzia ukubwani hatua hii aliyofikia sio ya kubeza hata kidogo na wachache sana wangeweza kufikia hapo alipofikia yeye

All the best Mtanzania mwenzetu. Uzalendo kwanza !
 
Ni kweli habari yenyewe imekaa kama imetengenezwa nyumbani,ok,nimeikuta sehemu hii hapa https://www.msn.com/en-us/sports/nba/hasheem-thabeet-to-work-out-for-bucks/ar-AAFDH8Q ...
Maana yake anakwenda kufanya majaribio na Bucks ila akikidhi mategemeo atachukuliwa alishindwa ataendelea na maisha yake. Tatizo linakuja hapa, Hasheem ni Bigman na sifa yake ni kuchukua rebounds na kupost. Mahitaji ya sasa ya NBA yanataka Bigmen wanaoweza ku shoot ndani na nje ya 'D'. Je Hasheem anaweza ku shoot 3 points? au hata ndani ya D? Yote haya yatajulikana next week kwenye hiyo workout.

Ila kwa matokeo yeyote Hasheem hakuitendea vizuri fursa aliyopata kuwa second pick ya mwaka 2009. Laiti angekuwa msikivu basi leo Tanzania ingekuwa ni mlango wa vijana kwenda NBA. Kiburi, dharau na kutoshaurika ndiyo kilichomharibu bila kusahau fedha nyingi za ghafla aliyopata baada ya mkataba wa kwanza na Memphis
 
Screenshot_20190816-133514.png
if yuh cyaan give a hand nah give a red eye" Homo habilis 2500,000 BC
 
Nani anambeza ? Hakuna mwenye moral authority ya kusema chochote kuhusu huyu Bwana hata kama angecheza game moja akaanza kuokota makopo..

Ingekuwa alikwenda kwa sponsorship au Kodi za wananchi hapo sawa..., yaani mwache kuwasema wabunge na viongozi wanaoishi kwa fedha zenu mmkamseme mtu ambaye anafight kivyake kwa ajili yake na akipenda familia yake (ingawa hata hio haina moral authority ya kumpangia).., Haya mambo ya ukifanikiwa ni mwenzetu uki-fail ni mwenyewe ni mambo ya kizamani

Ila kwa ushabiki lets regard him according to his performance not his Nationality..., akifanya vema tuseme akichemsha tuseme pia (as washabiki wa Kikapu) In conclusion washabiki wana moral authority ya kusema chochote kuhusu kiwango chake.., watanzania na utanzania hauna authority ya kumpangia afanye vizuri sababu ya utanzania wake...
 
Ataonekana tena akichezea Milwaukee Bucks ndugu yetu bado anaendelea kupambana na wachambuzi wanasema yupo kwenye good shape ya kuweza kumudu mikiki mikiki ya NBA.

wabongo tuache unafiki wa kumbeza ndugu yetu huu mchezo alijifunzia ukubwani hatua hii aliyofikia sio ya kubeza hata kidogo na wachache sana wangeweza kufikia hapo alipofikia yeye

All the best Mtanzania mwenzetu. Uzalendo kwanza !

Hizi huruma mnatafuta za nini?

Jamaa alipewa chance mara kibao anaenda na kurudi ila kiwango ni hovyo vile vile!

Kama mtu kiwango ni hovyo ni hovyo sio hovyo halafu unasema kiitwe bora sababu tu it happens mnatoka nae kipande cha ardhi kinaitwa nchi!
 
Maana yake anakwenda kufanya majaribio na Bucks ila akikidhi mategemeo atachukuliwa alishindwa ataendelea na maisha yake. Tatizo linakuja hapa, Hasheem ni Bigman na sifa yake ni kuchukua rebounds na kupost. Mahitaji ya sasa ya NBA yanataka Bigmen wanaoweza ku shoot ndani na nje ya 'D'. Je Hasheem anaweza ku shoot 3 points? au hata ndani ya D? Yote haya yatajulikana next week kwenye hiyo workout.
Ila kwa matokeo yeyote Hasheem hakuitendea vizuri fursa aliyopata kuwa second pick ya mwaka 2009. Laiti angekuwa msikivu basi leo Tanzania ingekuwa ni mlango wa vijana kwenda NBA. Kiburi, dharau na kutoshaurika ndiyo kilichomharibu bila kusahau fedha nyingi za ghafla aliyopata baada ya mkataba wa kwanza na Memphis

Kuna clip yake Nimeiona hivi karibuni ana shoot decent
 
Maybe the second time will be the charm ila aache utoto na ajitume. Watanzania wengi walikuwa wanampa ushauri wa maana tu wakati yuko chuo na baada ya kuingia NBA lakini kwa asilimia kubwa hakuufanyia kazi na anguko lake wengi walilitabiri.

amealikwa kwenye interview milwauke bucks next week.. tumuombee heri akafanye vizuri majaribio yake
 
Back
Top Bottom