Uchaguzi 2020 Ndugu yetu Tundu Lissu, KUBALI matokeo na ujipange safari ijayo

Uchaguzi 2020 Ndugu yetu Tundu Lissu, KUBALI matokeo na ujipange safari ijayo

Lisu na Chadema msikubali udhalimu huu. Kama kuna njia yoyote ya kuudhibiti itumieni hata kama ina madhara kwa taifa letu. Liwalo na liwe!
Lissu anasepa zake Ubelgiji na tiketi anayo tayari,tafuta mwingine.
 
Mliamua kwa makusudi kabisa kumwaga ugali! Hivyo muacheni na Lissu naye amwage mboga.

Hakuna namna! Dawa ya moto ni moto tu. Mabeberu lazima wafahamu kila uovu mlio ufanya safari hii.

No opposition candidate has ever lost an election and graciously conceded. Not one, since 1995 when the first multiparty general election was held!
 
huku mtaani kuna wasimamizi wanaongea kila kitu, wanasema jinsi walivyolazimishwa kupenyeza kura feki
#Mitaani Wasimamizi Wanasema Kila kitu: Wewe ni shahidi muhimu sana katika hili unalodai na bahati nzuri IP yako inakusoma vizuri; Kama umeropoka kufurahisha jukwaa ni bora ukiri na kurekebisha.

Lakini kama una uhakika kuna msimamizi wa kura alikuthibitishia alilazimishwa kupokea kura ghushi akanyamaza kwa madai ya hofu yake, lakini baada ya kutoka akakutumia wewe kuropoka uzushi huu hapo ni kosa la jinai.

Hakuna msimamizi atakuja kwako kukuambia eti alilazimishwa kushiriki wizi wakati akijua aliapa na alikuwa na uwezo wa yeye akatumia feki ID akaweka ujumbe huo hapa jukwaani au kutoa taarifa kwenye tume.
 
Kuukubali udhalimu mkubwa uliofanywa na huyo anayejiita mwendawazimu ili kung’ang’ania madarakani itakuwa ni kosa kubwa sana ambalo Lissu hawezi kulifanya. Penye udhalimu wa aina yoyote ile raia ni lazima wasimame kidete kuupinga udhalimu huo na hili jukumu si la Lissu pekee yake au Chadema pekee yake bali ni la Watanzania wote wapenda uhuru, haki na amani ya kweli.

Mkuu utaandamana?
 
Lissu anasubiri mabwana zake Marekane watafanyaje, hana support ya umma watu wamemgomea kuingia barabarani, Mbowe na wengine bado wapo kwenye uchungu mkali kama wa uzazi hawataki hata kuziona camera, tuwape week moja denial stage ipite kwanza.😁
 
#Mitaani Wasimamizi Wanasema Kila kitu: Wewe ni shahidi muhimu sana katika hili unalodai na bahati nzuri IP yako inakusoma vizuri; Kama umeropoka kufurahisha jukwaa ni bora ukiri na kurekebisha. Lakini kama una uhakika kuna msimamizi wa kura alikuthibitishia alilazimishwa kupokea kura ghushi akanyamaza kwa madai ya hofu yake, lakini baada ya kutoka akakutumia wewe kuropoka uzushi huu hapo ni kosa la jinai. Hakuna msimamizi atakuja kwako kukuambia eti alilazimishwa kushiriki wizi wakati akijua aliapa na alikuwa na uwezo wa yeye akatumia feki ID akaweka ujumbe huo hapa jukwaani au kutoa taarifa kwenye tume.
Acha vitisho wewe! Eboo. Yaani kutishana tu kwenye hii nchi kuanzia juu mpaka vinyangalika wanaotumia id fake nao eti wanawatisha wenzao wenye id fake.

Dah nalog off kwa kweli. Nsije tukana
 
Acha nisome comments, maana kweli sijui kwa undani wake kilichotokea. Kura ni siri, na kura yangu ilikuwa moja tu kwa kila nafasi.
 
Lissu anasepa zake Ubelgiji na tiketi anayo tayari,tafuta mwingine.
Anaenda kutibiwa tu halafu anarudi na hamtamfanya kitu. Atamfanyia kitu mbaya sana huyo mhutu wenu mpk hataamini macho yake. Chezea Lisu wewe!
 
Acha vitisho wewe! Eboo. Yaani kutishana tu kwenye hii nchi kuanzia juu mpaka vinyangalika wanaotumia id fake nao eti wanawatisha wenzao wenye id fake.
Dah nalog off kwa kweli. Nsije tukana
Hii inaitwa Jaribu kuingia Barabarani utatukuta walinda amani tunawasubiri ninyi msiopenda ugali

Mbona ni rahisi Sana, Ingia barabarani nasi tufanye yetu
 
Chama kilianza kampeini kwa kutembeza bakuli! Hakikiwa na wasaidizi kwenye ngazi za chini; unategemea kweli kitapata kura? Ingawa mimi bado ni mwanachadema mfu kwa sasa bado nisingekipigia kura hata kama ningekuwa active. Ubabaishaji mtupu!
 
Unaandika page ndefu kumbe utopolo mtupu uchaguzi umefanyika wapi hapa hakukuwa na uchaguzi watanzania siyo wajinga kihivo. Huo ni wizi wa aina gani kawe rahisi jumla ya kura za urais ni zaidi ya laki moja kulinganisha na jumla ya kura za ubunge na tume ilikataza watu kupiga kura za Rais sehemu nyingine nje ya walipojiandikisha isipokuwa mawakala wa tume ambao hawazidi 10 sasa hizo kura zaidi ya laki moja zimetoka wapi. Hivo tangu tupate uhuru zimewahi kutapakaa karatasi zilizopigwa kura mitaani kabla hata kura hazijaanza kuhesababi. Nchi yetu inapita aibu kubwa sana kwenye macho ya jumuia za kimataifa hadi wananchi tunaona aibu kwamba tunatoka Tanzania. Hii aibu ya karne
 
Let's udhibitisho, kura feki zipojee wale mawakala wakafanyaje, licha ya ivo kina majaribu unaambiwa uingize kura za Nini
Lipumba mwenyewe kasema uchaguzi huu ni kiboko kwa sababu ya kuiandika namba yako ya mpiga kura soo wanabaki nayo wewe unaenda kuweka karatasi yako ya kura kwenye boksi sasa mimi nashangaa wakala anaibiwaje na fundi wa kuyajua mambo ya Tanzania yule Bwana kigogo wa twitter hakujua yeye si anajua kila kitu.
Yani wamepigwa kihalali
 
Anaenda kutibiwa tu halafu anarudi na hamtamfanya kitu. Atamfanyia kitu mbaya sana huyo mhutu wenu mpk hataamini macho yake. Chezea Lisu wewe!
Aende akatibiwe,akirudi kuna kazinyingi sana serikalini kama vipi ata ubalozi utamuhusu.
akuna mkate mgumu mbele ya tea.
 
Aende akatibiwe,akirudi kuna kazinyingi sana serikalini kama vipi ata ubalozi utamuhusu.
akuna mkate mgumu mbele ya tea.
Mkiweza kumnunua chadema inakufa. Jambo ambalo ni gumu kama kufunika jua kwa shuka
 
Huu mnaoita uchaguzi unaelezea wazi aina ya mtawala tuliye naye ya kuwa ni muhuni kiasi gani. Very useless.
 
Mkiweza kumnunua chadema inakufa. Jambo ambalo ni gumu kama kufunika jua kwa shuka
Anunuliwi bali atapewa mustakbali wa taifa letu,na yeye kamayeye aonyeshe mchangowake kwenye ujenzi wa taifaletu pendwa.
akiitwa Ikulu ili kutengeneza maridhiano ya kitaifa ndo utaelewa.
kwani cha ajabu ni nini mpaka isiwezekane?
kesi zake zitaisha na ruzuku ya ajali yake ya kupigwa risasi na majambazi atapatiwa.
kwishaa,hii ndo Africa.
 
Back
Top Bottom