Uchaguzi 2020 Ndugu yetu Tundu Lissu, KUBALI matokeo na ujipange safari ijayo

Uchaguzi 2020 Ndugu yetu Tundu Lissu, KUBALI matokeo na ujipange safari ijayo

Hapo kwenye uchaguzi wa haki bora usipaongelee maana huku mtaani kuna wasimamizi wanaongea kila kitu, wanasema jinsi walivyolazimishwa kupenyeza kura feki
Uzushi mtupu, kura fake ziingie kutoka wapi?. Watanzania mbona mnapenda kula takataka?. Hakuna kura fake wala nini watanzania wakiamua yao wameamua.
 
NI SISI WANACHADEMA KANDA YA KASKAZINI
Sidhani kama umesema kweli kwamba wewe ni mwanachadema. Hapa chini kuna post yako ya mahali fulani

1604080350974.png
 
Kuukubali udhalimu mkubwa uliofanywa itakuwa ni kosa kubwa sana ambalo Lissu hawezi kulifanya. Penye udhalimu wa aina yoyote ile raia ni lazima wasimame kidete kuupinga udhalimu huo na hili jukumu si la Lissu pekee yake au Chadema pekee yake bali ni la Watanzania wote wapenda uhuru, haki na amani ya kweli.
Lini Chadema waliwahi kukubali Matokeo?. Kugaragazwa mmegaragazwa tu hakuna kisingizio hapa,kisingizio cha kuibiwa kura na bla bla ni upuuzi mtupu. Ingieni barabarani muipate dawa tamu. Mita kumi tu, mwisho.
 
Mwisho wa siku inabidi tujifunze from all we do, chama kinajisahau na kuwana plan za kizembe. Huwezi build up a strong house without a stronger foundation. Chama kimefocus kwa Rais instead kingejipa muda na kufocus Sana huku chini madiwani na wabunge kubuild up a very strong base ya kuja kupenya nayo. Mwisho wa siku wanasusiana na kusahau the foundation ya Kila kitu. So inabidi kujifunza kwani serikali sio presidential office tu bali MPs ndo mwanzo wa Kila kitu.
Ongelea yajayo kuhusu Tz ya kijani, ya chadema yaache tu maana kuna tatizo si dogo la miaka 5 bila ruzuku, ss ww unaongelea kujisahihisha sijui marekebisho nyakati hizi za kuwaza michango ya chama itakavyokuwa mingi?.
 
No opposition candidate has ever lost an election and graciously conceded. Not one, since 1995 when the first multiparty general election was held!
Wapo. Wale wanaozoa 1%-5% ya votes. Utawaona tu kwenye hafla fupi ya kumkabidhi cheti JPM.

Si ajabu na Membe nae akawepo mbele kabisa pale
 
30 OKTOBA 2020

Tumekuwa wafuatiliaji wakubwa wa kampeni zako tukiwa na matarajio ya kupata mengi mazuri baada ya kurudi kutoka Ubelgiji ukionyesha hali ya kushiriki vema katika kampeni zako.

Na kwa kweli ulianza vema ufunguzi wa kampeni zako kupitia CHADEMA yetu, ila tulianza kupata shaka baada ya kuona kauli zilizoanza kutoka muda mfupi baadaye ambazo zilitukumbusha msemo wa wahenga 'Asiyekubali kushindwa si mshindani.'

Hii ni kwa sababu ulituonyesha kuwa hukuja kushindana bali ulikuja kushinda kwa njia yoyote ile. Kauli zako zilionyesha hamasa za kuleta vurugu kati ya jamii na ndugu zetu Watanzania ili kuiangusha CCM hata kwa kumwaga damu ili wewe ukae katika kiti cha urais.

Leo tumesikiliza taarifa yako ya kukataa matokeo yanayoendelea kutolewa ukishinikiza jamii ya kimataifa kukataa uchaguzi huu. Tunadhani mshtuko mkubwa ulioupata wewe na viongozi wetu wa CHADEMA ni kuangushwa kwa Mgombea Freeman Mbowe ambaye amekuwa ni mbunge kwa miaka mingi na wabunge wengi mashuhuri hali ambayo hukufikiria.

Pengine ni kutoijua vizuri nchi yako kwa kipindi ulichokuwa ughaibuni. Ila tungependa kukujulisha yafuatayo kwa faida yako na viongozi wengine wa CHADEMA tukijibu mazungumzo yako ya leo.

1. UCHAGUZI NI HURU NA WA HAKI
Hakuna Mtanzania hata mmoja aliyekataliwa kupiga kura ikiwa na vigezo vinazohitajika. Mawakala wetu wa CHADEMA wametujulisha kuwa walikuwepo na wameshuhudia zoezi isipokuwa wanashangaa video zilizosambaa mtaani zikionyesha uzushi wa kutengeneza kuwa kura zimekamatwa.

Jamii za kimataifa zimefika na kuangalia zoezi zima. Hivyo, unachosema ni kujaribu kutafuta sababu ikiwa hali halisi unaijua. Tukubali tu tulizoea ubabaishaji ila sasa hivi tujipange upya kwa ajili ya uchaguzi ujao. Pia suala la mawakala kutopewa nakala za matokeo ni uzushi kwani chama chetu hadi kufikia usiku wa tarehe 28/10/2020 tulishajua upepo si mzuri.

2. HATUKUONEWA
Wanachadema tunajiuliza swali; Kama mawakala walikuwepo na hakuna aliyetoa ushahidi wa kukataliwa kuingia kituoni kwa nini hatusikii malalamiko hayo toka kwa mawakala na matokeo yake malalamiko yapo kwa wagombea walioshindwa ukiwemo wewe?

Tulisimamisha wagombea 244 lakini hatukuwawezesha fedha wagombea wetu wa ubunge kutokana na ukata katika chama. Fedha zipo lakini mwenyekiti na sekretarieti yake walikataa kutoa fedha hizo ili zikatusaidie na badala yake zimeendelea kupelekwa kwenye miradi binafsi ya viongozi.

Wabunge wetu walichangishwa kwa muda wa miaka mitano kwa sababu ya kuandaa fedha za kampeni lakini muda ulipofika hawakurudishiwa fedha zile hivyo kushindwa kuzunguka na kuomba kura.

Tujitafakari Wanachadema na viongozi wetu wametuangusha. Tunaamini walijua hawawezi kushinda ndio sababu.

3. HATUKO TAYARI KUANDAMANA WALA KUGOMA

Kura tumepiga tukimchagua kiongozi ambaye kwa miaka mitano amejinyima na kukaa na sisi Watanzania kwa kuijenga nchi yetu iweze kujitegemea. Tukitegemea uje na sera nzuri za kuboresha maendeleo ya uchumi wa nchi yetu na kuendelea kupunguza utegemezi ila muda mwingi wa kampeni zako ulitumia kuisema CCM kwa kusema unataka maendeleo ya watu na si vitu ili kuenda kinyume na mengi makubwa yaliyofanywa na CCM kuboresha barabara, shule, zahanati. Hali hii ilitufanya tujiulize maswali mengi juu ya uwezo wako.

Pia ulitumia muda mwingi kueleza ulivyoshambuliwa lakini sisi wafuasi wako tulitaka kujua utafanya nini ukichaguawa au kwanini tukupe dhama ya uongozi wa nchi? Ulishindwa kujibu maswali hayo na badala yake ulitumia muda mwingi kuonyesha umma wa wanachadema na Watanzania kuwa unaonewa. KWA MAELEZO HAYA HATUWEZI KUANDAMANA KABISA KWA AJILI YAKO.

4. CHAMA HAKIKUJIANDAA KUHUSU WEWE
Sisi Wanachadema tumechoshwa na maandalizi duni ya chama hasa kipindi hiki cha uchaguzi. Pamoja na malalamiko ya kutokuwa na fedha. Zipo taarifa kuwa wewe haukuandaliwa kugombea na ujio wako hakukubalika katika chama hadi kufikia kukataa kutoa fedha kwa ajili ya kampeni zako.

Pia, ushirikiano wako na viongozi wa juu wa chama haukuwepo na hawakuonekana katika mikutano yako. Kwetu sisi kama wanachadema tuliona ni tatizo kubwa sana. Taarifa tulizopata zilionyesha kuna mgogoro mkubwa wa maslahi ndani ya chama na mwenyekiti hakukukubali ndio maana hakuweza kukusaidia kampeni zako.

5. UNATUMIKA NA MATAIFA MAKUBWA KUHATARISHA AMANI YA NCHI
Tunafahamu wewe ni mwanasheria mzuri wa kimataifa. Kwa nini umlete Robert Amsterdam aje kama mwanasheria wako? Je, kuna maslahi gani amekuja kuyasimamia? Tumekuwa tukipinga sana ushoga na zipo taarifa kuwa umedhaminiwa na mataifa makuwa ili ukipata uongozi uidhinishe ushoga na kuuza madini yetu nje ya nch na ukishindwa uanzishe hata vurugu kwa mgongo wa demokrasia ili kutufikisha kama Libya ambako wanapigana vita vya wenyewe kwa wenyewe hadi sasa. Leo, Robert Amsterdam yupo Uturuki akisubiri Watanzania tupigane kwa uchochezai aliouandaa kupitia wewe. Tunakushauri kaungane naye tu muendelee na maisha yenu.

HITIMISHO

Tanzania itabaki kuwa nchi ya amani na maendeleo yataletwa na sisi wenyewe kamwe hatutakubali kununuliwa kwa bei yeyote tupo macho.

NI SISI WANACHADEMA KANDA YA KASKAZINI
Kamanda, umemaliza kila kitu. Hakuna kuvuna bila kupanda. Watanzania wameishangaza dunia nzima. Kuanzia kwenye Corona mpaka uchaguzi mkuu.
 
MATAGA at work

Matokeo ya kura hayaendani na hali halisi japokuwa wapo wengi ambao hawajapiga kura.

Mojawapo ya sababu ya kutokupiga kura wapo wengi ambao hawana imani na electoral process na hii huwezi kuwalaumu wapinzani. Mtu haoni kama walio madarakani wanaweza kukubali kushindwa.

Wamekatishwa tamaa!
 
Ongelea yajayo kuhusu Tz ya kijani, ya chadema yaache tu maana kuna tatizo si dogo la miaka 5 bila ruzuku, ss ww unaongelea kujisahihisha sijui marekebisho nyakati hizi za kuwaza michango ya chama itakavyokuwa mingi?.
Namrekebisha huyo Ndugu yangu hapo anaposema Mimi sio mwanachadema kwani mtazamo wangu kuhusu Kiongozi flani hauna chama and that's me and my opinions. Na naamini kuwa next time watajifunza na kufanya vyema but amani yetu ni mpango mzima aiseeeh.
 
Wewe ni mpiga nduru tu wa CCM usojua lolote tuulize sie tulovaa fulana za chama
je wajua kura nyingi za Magufuli zilipigwa na wafu
je wajua wanafunzi kuanzia form one walipiga kura
na walio wengi wasoenda kituoni kupiga kura sie wasimamizi wa tume tuliwawakilisha
bado kulikuwa na marundo ya kura zilizopigwa tayari
mode futeni na hii post tena kwa maana mmeshaonyesha itikadi
 
MATAGA at work

Matokeo ya kura hayaendani na hali halisi japokuwa wapo wengi ambao hawajapiga kura.

Mojawapo ya sababu ya kutokupiga kura wapo wengi ambao hawana imani na electoral process na hii huwezi kuwalaumu wapinzani. Mtu haoni kama walio madarakani wanaweza kukubali kushindwa.

Wamekatishwa tamaa!
Hizo ni hoja fupi, walio piga kura wengi ni kinamama na watu wa makamo Kama wewe binafsi umepiga kura basi umehionea. Vijana wengi hawajapiga kura na sababu mojawapo kubwa hasa ni kutokua na makazi permanent in 5 yrs vijana wanamove Sana na mahala walipojiandikishia panakua mbali Sana na makazi yao mapya na hilo ndo tatizo kubwa kuliko yote na sio kutokua na imani na system. Mbona hawajaingia mtaani Kama wanavyoelekezwa kufanya vijana wa kitanzania sio wajinga kabisa.
 
Lissu na Chadema msikubali udhalimu huu. Kama kuna njia yoyote ya kuudhibiti itumieni hata kama ina madhara kwa taifa letu. Liwalo na liwe!
Ufalme unapatikana kwa nguvu, na wenye nguvu ndio wanaoupata. Hakuna wakati ccm itaondoka madarakani kwa uchaguzi. Huu ndio ujumbe ambao wameuletea upinzani wa Tanzania kwenye uchaguzi huu. Mkisema msubiri uchaguzi wa miaka 5 ijayo wataubaka kama huu. Haki haiombwi. Haki inanyakuliwa kwa nguvu. It's now or never. Huu ni wakati wenu muafaka wa kuchukua haki ya WaTz kuliko wakati mwingine wowote.
 
Wewe ni mpiga nduru tu wa CCM usojua lolote tuulize sie tulovaa fulana za chama
je wajua kura nyingi za Magufuli zilipigwa na wafu
je wajua wanafunzi kuanzia form one walipiga kura
na walio wengi wasoenda kituoni kupiga kura sie wasimamizi wa tume tuliwawakilisha
bado kulikuwa na marundo ya kura zilizopigwa tayari
mode futeni na hii post tena kwa maana mmeshaonyesha itikadi
Wewe ndo mpiga nduru na hujui husemalo kabisa. So you mean umehusika kabisa kwa Kila hali kuingiza hizo kura feki sio? Then wewe ni mjinga wa mwisho kwasaabu huwezi fanya upuyaya Kama huo afu unaposti sahiv hapa na Kama umefanya kwasaabu ya pesa basi wewe pia ni mshenzi wa kutupa na msaliti mkumbwa wa kutupa. Hizo propaganda ndo zinapandishwa pia kule twitter ili kupata sympathy ya mabeberu so as tuanzishe machafuko nchini Kwetu. Narudia kusema watanzania sio wajinga hata siku moja hatutokubali ujinga propaganda Kama hizo. Alafu Unaweza kuta ww hata kituoni hufika Wala kura hijapiga.
 
Namrekebisha huyo Ndugu yangu hapo anaposema Mimi sio mwanachadema kwani mtazamo wangu kuhusu Kiongozi flani hauna chama and that's me and my opinions. Na naamini kuwa next time watajifunza na kufanya vyema but amani yetu ni mpango mzima aiseeeh.
Amani itakuwepo. Wapinzani wametolewa mapema kwenye ligi. Wameumia ila wana amani. Maumivu yataisha soon na watakuwa wapenzi watazamaji. Mm nadhani wanaotakiwa kuwa na hofu ni waliopewa madaraka maana hawana wa kumpa lawama tena.
 
Back
Top Bottom