Uchaguzi 2020 Ndugu yetu Tundu Lissu, KUBALI matokeo na ujipange safari ijayo

Uchaguzi 2020 Ndugu yetu Tundu Lissu, KUBALI matokeo na ujipange safari ijayo

Hakuna kitu kibaya kama kulazimisha furaha yani bora uhuzunike hatimaye utakua vizuri! Mleta mada hiyo #1 tu umeandika ila nafsi inakusuta achilia mbali yote yaliyofuatia! Ni mtoto aliyezaliwa 2015 tu ndio atashindwa kujua ccm hawaibi kura kwenye chaguzi ! Ila kila aliyeshuhudia chaguzi zote analijua hilo ila kwa wizi wa mwaka huu it was too much ! Hadi waliokuwa hawajui wamejua zaidi huwa zinaibwaje
 
Keyboard ya manufaa sio za kuchagua nchi kwankutaka umwagaji damu ili wao waje nchini Kwetu. Mfano USA, FB walipo minya na ilipoingilia uchaguzi wao 2018 Mtanzania gani alienda kuwahoji. Be realistic bana msiongee tu basi. Wazungu wakae kwao huko waje kutembea na kurudi makwao sio kututaka kuanzisha ushenzi nchini Kwetu.
Wazungu wengi wana mtizamo wao kuhusu Afrika; ambao ni hasi.
 
Keyboard ya manufaa sio za kuchagua nchi kwankutaka umwagaji damu ili wao waje nchini Kwetu. Mfano USA, FB walipo minya na ilipoingilia uchaguzi wao 2018 Mtanzania gani alienda kuwahoji. Be realistic bana msiongee tu basi. Wazungu wakae kwao huko waje kutembea na kurudi makwao sio kututaka kuanzisha ushenzi nchini Kwetu.
CCM wakienda ulaya America kuomba omba misaada hupiga magoti huwaita wazungu wafadhili wahisani lakini hao hao wazungu wakikataa ujinga upumbavu unyanyasaji uonevu mateso ya CCM kwa wapinzani ndipo CCM hugeuka na kuwaita wanaume wenzenu mabeberu utazani nyinyi CCM ni mbuzi jike
 
Hakuna uchaguzi Tanzania CCM imefanya vioja maigizo kuuhadaa ulimwengu kuwa kuna uchaguzi
Mh. Magufuli kitendo cha kuwaombea kura wabunge na madiwani ni ishara tosha ya kuwa he was prepared for this battle, narudia kusema hili ni jambo kujifunza na kufanyia kazi sio unaenda jukwaani unaanza kuimiza watu kugoma, kufanya fujo as I said Tanzanians aren't idiots Kama wengi mnvyofikiria hakuna mtu anashidwa kupredict kuwa Kiongozi flani wants this from me or us.
 
CCM wakienda ulaya America kuomba omba misaada hupiga magoti huwaita wazungu wafadhili wahisani lakini hao hao wazungu wakikataa ujinga upumbavu unyanyasaji uonevu mateso ya CCM kwa wapinzani ndipo CCM hugeuka na kuwaita wanaume wenzenu mabeberu utazani nyinyi CCM ni mbuzi jike
Msaada wengi wanaomba mbona, ila kumwaga damu aaaah bana embu kuwa kama mtanzania.
 
Ufalme unapatikana kwa nguvu, na wenye nguvu ndio wanaoupata. Hakuna wakati ccm itaondoka madarakani kwa uchaguzi. Huu ndio ujumbe ambao wameuletea upinzani wa Tanzania kwenye uchaguzi huu. Mkisema msubiri uchaguzi wa miaka 5 ijayo wataubaka kama huu. Haki haiombwi. Haki inanyakuliwa kwa nguvu. It's now or never. Huu ni wakati wenu muafaka wa kuchukua haki ya WaTz kuliko wakati mwingine wowote.
Kesho kutakuwa na press ya ACT/Chadema combined. Hakuna kulala kuanzia kesho. Ni ama za Uhai ana Kifo kuanzia kesho baada ya press.

Ukiogopa kuuliwa kwa risasi utauliwa kwa msongo wa mawazo ama njaa.
 
Kesho kutakuwa na press ya ACT/Chadema combined. Hakuna kulala kuanzia kesho. Ni ama za Uhai ana Kifo kuanzia kesho baada ya press.

Ukiogopa kuuliwa kwa risasi utauliwa kwa msongo wa mawazo ama njaa.
Nimeona tangazo, and this was all predicted as I said toka mwanzo Mh. Lissu was predicted toka mwanzo wa kampeni zake. Kinachoumiza zaidi hakuweka effort ya ziada kubadilisha kabisa his scheme na ndo maana hata hitimisho lake lilikua linajilikana and this is what was expected, I expected it kabisaaah so jiandaeni pia kumbiwa kuingia barabarani [emoji38][emoji38]. Lakini pia kwa ninavyoelewa watanzania wenzangu na huyu ndugu yangu minyoo ndo kwanza atakua amembonji[emoji23][emoji23][emoji23]. Kama vipi utatakuta kwenye VPN party ambayo watanzania washaandaa[emoji23][emoji23].
 
kuna kura zilishapigwa before na wao ilikuwa ni kuzichanganya na zinazopigwa siku ile, ukisema kithibitisho unamaanisha unataka nini?
CCM bila Polisiccm bila Tumeccm bila mahakamaccm bila wakurugenziccm bila Msajiliccm bila uchakachuaji bila wizi wa kura ni weupe sana
Sasa si ukafungue kesi mahakamani mkuu,maana inaelekea una ushahidi wa hatari?
 
Nimeona tangazo, and this was all predicted as I said toka mwanzo Mh. Lissu was predicted toka mwanzo wa kampeni zake. Kinachoumiza zaidi hakuweka effort ya ziada kubadilisha kabisa his scheme na ndo maana hata hitimisho lake lilikua linajilikana and this is what was expected, I expected it kabisaaah so jiandaeni pia kumbiwa kuingia barabarani [emoji38][emoji38]. Lakini pia kwa ninavyoelewa watanzania wenzangu na huyu ndugu yangu minyoo ndo kwanza atakua amembonji[emoji23][emoji23][emoji23]. Kama vipi utatakuta kwenye VPN party ambayo watanzania washaandaa[emoji23][emoji23].
Tupo tusio na chochote Cha kupoteza. Uhai wetu hauna maqna tena kwa maisha haya. Bora kufa napigania haki kuliko kufa nimechutama kuiomba haki.

Kesho nasikia harufu ya damu ikinukia puani mwangu halafu nafurahia kuuliwa kwma shujaa.
 
Napinga kabisa kwa nguvu zote wazo la kumtia moyo huyu 'mnanii' kusema eti ajipange kwa kipindi kijacho. Amemaliza zamu yake, amegalagazwa vibaya sana, aende zake.
Nakubaliana na wazo la chadema kujitafakari na kujipanga upya, kwa kujiondoa kabisa kwenye shombo ya lissu (kupinga kila kitu, kushogesha nchi, kuweka rehani madini, kutumiwa na kufadhiriwa na mabeberu, nk). Hakuna mgombea yeyote wa chadema atakayeweza kushinda bila kujivua hiyo harufu mbaya. Watanzania siyo wajinga kiasi hicho.
 
Mwisho wa siku inabidi tujifunze from all we do, chama kinajisahau na kuwana plan za kizembe. Huwezi build up a strong house without a stronger foundation. Chama kimefocus kwa Rais instead kingejipa muda na kufocus Sana huku chini madiwani na wabunge kubuild up a very strong base ya kuja kupenya nayo. Mwisho wa siku wanasusiana na kusahau the foundation ya Kila kitu. So inabidi kujifunza kwani serikali sio presidential office tu bali MPs ndo mwanzo wa Kila kitu.
Upo nchini wewe au unaropoka toka kwa mabeberu? Mmekwisha sahau kuwa Magu wenu alipiga marufuku shughuli za kisiasa za vyama vingine. CCM ilianza kampeni hii tangu Magu alivyoingia madarakani 2015 huku akiwakataza vyama vingine
 
Nifute kwaajili gani?, I do support JPM kwani naona na napenda what he has done with this country. If is was up to me ningemwongezea hata 20yrs Kama Mungu angempa uzima. That's my opinions sikuzuii kutoa zako kwani hii ni nchi huru.
Mjomba huu uzi umeandika ukijinasibisha wewe ni mwanachadema ilhali sio kweli tukifuatilia nyuz zako za nyuma
 
Namba 3 kiongozi gani anajinyima na kuijenga Nchi? Ujenzi upi? Kwani miradi yote mikubwa ina ufisadi mkubwa, ujenzi wa chato Airport kienyeji pasipo idhini ya bunge ni mojawapo ya mradi wa kifisadi, ununuzi wa Ndege ana 10% zake hakuna mradi asiojinufaisha binafsi na watu wake, kwa kifupi CCM ni ile ile ukoo wa panya baba mama watoto ni wezi
CAG Pr.Assad
 
Maoni yangu chadema wasikubali haya matokeo.. wasiende kwenye maandamano maana wananchi bado hawana ujasiri huo..

Wajipange namna ya kupambana nje ya uwanja.

Watumie zaidi mataifa ya nje kushinikiza uchaguzi kurudiwa.

Marekeni amesha sema uchaguzi ulikua sio huru.
Si Hamia huko marekan kila kitu marekani marekani khaa
 
30 OKTOBA 2020

Tumekuwa wafuatiliaji wakubwa wa kampeni zako tukiwa na matarajio ya kupata mengi mazuri baada ya kurudi kutoka Ubelgiji ukionyesha hali ya kushiriki vema katika kampeni zako.

Na kwa kweli ulianza vema ufunguzi wa kampeni zako kupitia CHADEMA yetu, ila tulianza kupata shaka baada ya kuona kauli zilizoanza kutoka muda mfupi baadaye ambazo zilitukumbusha msemo wa wahenga 'Asiyekubali kushindwa si mshindani.'

Hii ni kwa sababu ulituonyesha kuwa hukuja kushindana bali ulikuja kushinda kwa njia yoyote ile. Kauli zako zilionyesha hamasa za kuleta vurugu kati ya jamii na ndugu zetu Watanzania ili kuiangusha CCM hata kwa kumwaga damu ili wewe ukae katika kiti cha urais.

Leo tumesikiliza taarifa yako ya kukataa matokeo yanayoendelea kutolewa ukishinikiza jamii ya kimataifa kukataa uchaguzi huu. Tunadhani mshtuko mkubwa ulioupata wewe na viongozi wetu wa CHADEMA ni kuangushwa kwa Mgombea Freeman Mbowe ambaye amekuwa ni mbunge kwa miaka mingi na wabunge wengi mashuhuri hali ambayo hukufikiria.

Pengine ni kutoijua vizuri nchi yako kwa kipindi ulichokuwa ughaibuni. Ila tungependa kukujulisha yafuatayo kwa faida yako na viongozi wengine wa CHADEMA tukijibu mazungumzo yako ya leo.

1. UCHAGUZI NI HURU NA WA HAKI
Hakuna Mtanzania hata mmoja aliyekataliwa kupiga kura ikiwa na vigezo vinazohitajika. Mawakala wetu wa CHADEMA wametujulisha kuwa walikuwepo na wameshuhudia zoezi isipokuwa wanashangaa video zilizosambaa mtaani zikionyesha uzushi wa kutengeneza kuwa kura zimekamatwa.

Jamii za kimataifa zimefika na kuangalia zoezi zima. Hivyo, unachosema ni kujaribu kutafuta sababu ikiwa hali halisi unaijua. Tukubali tu tulizoea ubabaishaji ila sasa hivi tujipange upya kwa ajili ya uchaguzi ujao. Pia suala la mawakala kutopewa nakala za matokeo ni uzushi kwani chama chetu hadi kufikia usiku wa tarehe 28/10/2020 tulishajua upepo si mzuri.

2. HATUKUONEWA
Wanachadema tunajiuliza swali; Kama mawakala walikuwepo na hakuna aliyetoa ushahidi wa kukataliwa kuingia kituoni kwa nini hatusikii malalamiko hayo toka kwa mawakala na matokeo yake malalamiko yapo kwa wagombea walioshindwa ukiwemo wewe?

Tulisimamisha wagombea 244 lakini hatukuwawezesha fedha wagombea wetu wa ubunge kutokana na ukata katika chama. Fedha zipo lakini mwenyekiti na sekretarieti yake walikataa kutoa fedha hizo ili zikatusaidie na badala yake zimeendelea kupelekwa kwenye miradi binafsi ya viongozi.

Wabunge wetu walichangishwa kwa muda wa miaka mitano kwa sababu ya kuandaa fedha za kampeni lakini muda ulipofika hawakurudishiwa fedha zile hivyo kushindwa kuzunguka na kuomba kura.

Tujitafakari Wanachadema na viongozi wetu wametuangusha. Tunaamini walijua hawawezi kushinda ndio sababu.

3. HATUKO TAYARI KUANDAMANA WALA KUGOMA

Kura tumepiga tukimchagua kiongozi ambaye kwa miaka mitano amejinyima na kukaa na sisi Watanzania kwa kuijenga nchi yetu iweze kujitegemea. Tukitegemea uje na sera nzuri za kuboresha maendeleo ya uchumi wa nchi yetu na kuendelea kupunguza utegemezi ila muda mwingi wa kampeni zako ulitumia kuisema CCM kwa kusema unataka maendeleo ya watu na si vitu ili kuenda kinyume na mengi makubwa yaliyofanywa na CCM kuboresha barabara, shule, zahanati. Hali hii ilitufanya tujiulize maswali mengi juu ya uwezo wako.

Pia ulitumia muda mwingi kueleza ulivyoshambuliwa lakini sisi wafuasi wako tulitaka kujua utafanya nini ukichaguawa au kwanini tukupe dhama ya uongozi wa nchi? Ulishindwa kujibu maswali hayo na badala yake ulitumia muda mwingi kuonyesha umma wa wanachadema na Watanzania kuwa unaonewa. KWA MAELEZO HAYA HATUWEZI KUANDAMANA KABISA KWA AJILI YAKO.

4. CHAMA HAKIKUJIANDAA KUHUSU WEWE
Sisi Wanachadema tumechoshwa na maandalizi duni ya chama hasa kipindi hiki cha uchaguzi. Pamoja na malalamiko ya kutokuwa na fedha. Zipo taarifa kuwa wewe haukuandaliwa kugombea na ujio wako hakukubalika katika chama hadi kufikia kukataa kutoa fedha kwa ajili ya kampeni zako.

Pia, ushirikiano wako na viongozi wa juu wa chama haukuwepo na hawakuonekana katika mikutano yako. Kwetu sisi kama wanachadema tuliona ni tatizo kubwa sana. Taarifa tulizopata zilionyesha kuna mgogoro mkubwa wa maslahi ndani ya chama na mwenyekiti hakukukubali ndio maana hakuweza kukusaidia kampeni zako.

5. UNATUMIKA NA MATAIFA MAKUBWA KUHATARISHA AMANI YA NCHI
Tunafahamu wewe ni mwanasheria mzuri wa kimataifa. Kwa nini umlete Robert Amsterdam aje kama mwanasheria wako? Je, kuna maslahi gani amekuja kuyasimamia? Tumekuwa tukipinga sana ushoga na zipo taarifa kuwa umedhaminiwa na mataifa makuwa ili ukipata uongozi uidhinishe ushoga na kuuza madini yetu nje ya nch na ukishindwa uanzishe hata vurugu kwa mgongo wa demokrasia ili kutufikisha kama Libya ambako wanapigana vita vya wenyewe kwa wenyewe hadi sasa. Leo, Robert Amsterdam yupo Uturuki akisubiri Watanzania tupigane kwa uchochezai aliouandaa kupitia wewe. Tunakushauri kaungane naye tu muendelee na maisha yenu.

HITIMISHO

Tanzania itabaki kuwa nchi ya amani na maendeleo yataletwa na sisi wenyewe kamwe hatutakubali kununuliwa kwa bei yeyote tupo macho.

NI SISI WANACHADEMA KANDA YA KASKAZINI
Andika namba yako ya simu hapa , umepata wilaya.
Subiri utapigiwa.
 
Keyboard ya manufaa sio za kuchagua nchi kwankutaka umwagaji damu ili wao waje nchini Kwetu. Mfano USA, FB walipo minya na ilipoingilia uchaguzi wao 2018 Mtanzania gani alienda kuwahoji. Be realistic bana msiongee tu basi. Wazungu wakae kwao huko waje kutembea na kurudi makwao sio kututaka kuanzisha ushenzi nchini Kwetu.
Hicho kiburi tungekuwa nacho kama tungekuwa tunajitegemea hasa kiuchumi.Lakini kwa sasa tusidanganyane wale jamaa walituachia Uhuru wa bendera tu kumbe walikusudia kutuletea ukoloni mbaya kuliko ule wa mijeredi(Ukoloni part II).Ndio maana mara tuwaite mabeberu mara nchi wahisani.Kauli mbili zinazokinzana kutoka katika kinywa kimoja.Na mbaya zaidi tunawaona watanzania wenzetu wenye mawazo mbadala kama maadui zetu badala ya kutafuta njia za kimkakati za kumkabili adui yetu halisi.Tanzania ni yetu sote na bahati mbaya Mungu katupa Tanzania moja tu,hakuna Tanzania nyingine.
 
Do you know kuwa Amsterdam ndio one of the sh**t pr**ks walio ifanya Congo kuwa katika state iliopo now? So watch out on what you support brother/ sister and be careful on what you pray and wish for. Tumempata Kiongozi aneweza kupmbana na Hawa watu let's support him sio kumwekea kiwingu kisichoku na manufaa yoyote.
Nilishawahi kuandika humu.Silaha (ulinzi) bora kabisa wa kiongozi yeyote hasa wa kiafrika ni raia wake.Ukishagundua una maadui wa nje si vema kutengeneza maadui wa ndani tena kwa makusudi.Naamini Gadafi angekuwa anawatreat raia wake kwa haki bila harufu yoyote ya ubaguzi basi hao tunaowaita mabeberu wangekosa pathway.Kiongozi kuonesha waziwazi kwamba kuna raia wako huwapendi na unawafanyia unyama wa aina moja au nyingine ni hatari.Sioni jema hapo.
 
Huu ujinga wenu wa kutengeneza propaganda za kishamba kijinga jinga mkizani watanzania ni wajinga kama nyinyi ndiyo umewakosesha kura mpaka mkaamua kuunajisi kuulawiti na kuubaka uchaguzi huu kwa njia haramu za kishetani, mifano yako ya SMG ni mifano ya kijuha ni mtu mbumbumbu zuzu kama wewe anaweza kukaa kuamini ujinga wako.
Ingia barabarani kama jeuri unayo
 
Back
Top Bottom