Uchaguzi 2020 Ndugu yetu Tundu Lissu, KUBALI matokeo na ujipange safari ijayo

Uchaguzi 2020 Ndugu yetu Tundu Lissu, KUBALI matokeo na ujipange safari ijayo

30 OKTOBA 2020

Tumekuwa wafuatiliaji wakubwa wa kampeni zako tukiwa na matarajio ya kupata mengi mazuri baada ya kurudi kutoka Ubelgiji ukionyesha hali ya kushiriki vema katika kampeni zako.

Na kwa kweli ulianza vema ufunguzi wa kampeni zako kupitia CHADEMA yetu, ila tulianza kupata shaka baada ya kuona kauli zilizoanza kutoka muda mfupi baadaye ambazo zilitukumbusha msemo wa wahenga 'Asiyekubali kushindwa si mshindani.'

Hii ni kwa sababu ulituonyesha kuwa hukuja kushindana bali ulikuja kushinda kwa njia yoyote ile. Kauli zako zilionyesha hamasa za kuleta vurugu kati ya jamii na ndugu zetu Watanzania ili kuiangusha CCM hata kwa kumwaga damu ili wewe ukae katika kiti cha urais.

Leo tumesikiliza taarifa yako ya kukataa matokeo yanayoendelea kutolewa ukishinikiza jamii ya kimataifa kukataa uchaguzi huu. Tunadhani mshtuko mkubwa ulioupata wewe na viongozi wetu wa CHADEMA ni kuangushwa kwa Mgombea Freeman Mbowe ambaye amekuwa ni mbunge kwa miaka mingi na wabunge wengi mashuhuri hali ambayo hukufikiria.

Pengine ni kutoijua vizuri nchi yako kwa kipindi ulichokuwa ughaibuni. Ila tungependa kukujulisha yafuatayo kwa faida yako na viongozi wengine wa CHADEMA tukijibu mazungumzo yako ya leo.

1. UCHAGUZI NI HURU NA WA HAKI
Hakuna Mtanzania hata mmoja aliyekataliwa kupiga kura ikiwa na vigezo vinazohitajika. Mawakala wetu wa CHADEMA wametujulisha kuwa walikuwepo na wameshuhudia zoezi isipokuwa wanashangaa video zilizosambaa mtaani zikionyesha uzushi wa kutengeneza kuwa kura zimekamatwa.

Jamii za kimataifa zimefika na kuangalia zoezi zima. Hivyo, unachosema ni kujaribu kutafuta sababu ikiwa hali halisi unaijua. Tukubali tu tulizoea ubabaishaji ila sasa hivi tujipange upya kwa ajili ya uchaguzi ujao. Pia suala la mawakala kutopewa nakala za matokeo ni uzushi kwani chama chetu hadi kufikia usiku wa tarehe 28/10/2020 tulishajua upepo si mzuri.

2. HATUKUONEWA
Wanachadema tunajiuliza swali; Kama mawakala walikuwepo na hakuna aliyetoa ushahidi wa kukataliwa kuingia kituoni kwa nini hatusikii malalamiko hayo toka kwa mawakala na matokeo yake malalamiko yapo kwa wagombea walioshindwa ukiwemo wewe?

Tulisimamisha wagombea 244 lakini hatukuwawezesha fedha wagombea wetu wa ubunge kutokana na ukata katika chama. Fedha zipo lakini mwenyekiti na sekretarieti yake walikataa kutoa fedha hizo ili zikatusaidie na badala yake zimeendelea kupelekwa kwenye miradi binafsi ya viongozi.

Wabunge wetu walichangishwa kwa muda wa miaka mitano kwa sababu ya kuandaa fedha za kampeni lakini muda ulipofika hawakurudishiwa fedha zile hivyo kushindwa kuzunguka na kuomba kura.

Tujitafakari Wanachadema na viongozi wetu wametuangusha. Tunaamini walijua hawawezi kushinda ndio sababu.

3. HATUKO TAYARI KUANDAMANA WALA KUGOMA
Kura tumepiga tukimchagua kiongozi ambaye kwa miaka mitano amejinyima na kukaa na sisi Watanzania kwa kuijenga nchi yetu iweze kujitegemea. Tukitegemea uje na sera nzuri za kuboresha maendeleo ya uchumi wa nchi yetu na kuendelea kupunguza utegemezi ila muda mwingi wa kampeni zako ulitumia kuisema CCM kwa kusema unataka maendeleo ya watu na si vitu ili kuenda kinyume na mengi makubwa yaliyofanywa na CCM kuboresha barabara, shule, zahanati. Hali hii ilitufanya tujiulize maswali mengi juu ya uwezo wako.

Pia ulitumia muda mwingi kueleza ulivyoshambuliwa lakini sisi wafuasi wako tulitaka kujua utafanya nini ukichaguawa au kwanini tukupe dhama ya uongozi wa nchi? Ulishindwa kujibu maswali hayo na badala yake ulitumia muda mwingi kuonyesha umma wa wanachadema na Watanzania kuwa unaonewa. KWA MAELEZO HAYA HATUWEZI KUANDAMANA KABISA KWA AJILI YAKO.

4. CHAMA HAKIKUJIANDAA KUHUSU WEWE
Sisi Wanachadema tumechoshwa na maandalizi duni ya chama hasa kipindi hiki cha uchaguzi. Pamoja na malalamiko ya kutokuwa na fedha. Zipo taarifa kuwa wewe haukuandaliwa kugombea na ujio wako hakukubalika katika chama hadi kufikia kukataa kutoa fedha kwa ajili ya kampeni zako.

Pia, ushirikiano wako na viongozi wa juu wa chama haukuwepo na hawakuonekana katika mikutano yako. Kwetu sisi kama wanachadema tuliona ni tatizo kubwa sana. Taarifa tulizopata zilionyesha kuna mgogoro mkubwa wa maslahi ndani ya chama na mwenyekiti hakukukubali ndio maana hakuweza kukusaidia kampeni zako.

5. UNATUMIKA NA MATAIFA MAKUBWA KUHATARISHA AMANI YA NCHI
Tunafahamu wewe ni mwanasheria mzuri wa kimataifa. Kwa nini umlete Robert Amsterdam aje kama mwanasheria wako? Je, kuna maslahi gani amekuja kuyasimamia? Tumekuwa tukipinga sana ushoga na zipo taarifa kuwa umedhaminiwa na mataifa makuwa ili ukipata uongozi uidhinishe ushoga na kuuza madini yetu nje ya nch na ukishindwa uanzishe hata vurugu kwa mgongo wa demokrasia ili kutufikisha kama Libya ambako wanapigana vita vya wenyewe kwa wenyewe hadi sasa. Leo, Robert Amsterdam yupo Uturuki akisubiri Watanzania tupigane kwa uchochezai aliouandaa kupitia wewe. Tunakushauri kaungane naye tu muendelee na maisha yenu.

HITIMISHO

Tanzania itabaki kuwa nchi ya amani na maendeleo yataletwa na sisi wenyewe kamwe hatutakubali kununuliwa kwa bei yeyote tupo macho.

NI SISI WANACHADEMA KANDA YA KASKAZINI

Utopolo mtupu.

Pichani, mama yule anatuwakilisha wengi mno. Hata jiwe anajua hilo:

IMG_20201031_015738_162.jpg
 
Kabisa, na kifika huko ndo atajua nini maana ya kuwa na amani nchini.
CCM wakienda kuomba omba misaada America huwapigia magoti na kuwaita wahisani wafadhili lakini hao hao wazungu wakikataa ujinga upumbavu unyanyasaji uonevu uovu mateso ya CCM kwa wapinzani ndipo CCM hugeuka na kuwaita wanaume wenzenu mabeberu utazani nyinyi CCM ni mbuzi jike
 
Nimeona tangazo, and this was all predicted as I said toka mwanzo Mh. Lissu was predicted toka mwanzo wa kampeni zake. Kinachoumiza zaidi hakuweka effort ya ziada kubadilisha kabisa his scheme na ndo maana hata hitimisho lake lilikua linajilikana and this is what was expected, I expected it kabisaaah so jiandaeni pia kumbiwa kuingia barabarani [emoji38][emoji38]. Lakini pia kwa ninavyoelewa watanzania wenzangu na huyu ndugu yangu minyoo ndo kwanza atakua amembonji[emoji23][emoji23][emoji23]. Kama vipi utatakuta kwenye VPN party ambayo watanzania washaandaa[emoji23][emoji23].
Tanzania hakuna uchaguzi umefanyika bali CCM imeulawiti umeunajisi kuubaka uchaguzi kwa njia haramu za kishetani tu
 
Uzushi mtupu, kura fake ziingie kutoka wapi?. Watanzania mbona mnapenda kula takataka?. Hakuna kura fake wala nini watanzania wakiamua yao wameamua.
huo upupu kadanganyeni vijijini ila sio mjini kwa watu wenye elimu zao na akili zao timamu, hata mahesabu yamewashinda kujumlisha, total ya wapiga kura za ubunge kwenye jimbo hazilingani na total namba za wapiga kura za uraisi kwenye jimbo hilohilo, na kwa taarifa yako hao wanafunzi wa vyuo,walimu,wafanyakazi wa sekta zingine serikalini wote walioshirikisha kwenye udhalimu ni ndugu zetu, marafiki zetu na wanaongea ukweli mtupu.
 
Kabisa, na kifika huko ndo atajua nini maana ya kuwa na amani nchini.
Tanzania hakuna Amani bali Tanzania ni kisiwa cha Uvumilivu tu hakuna Amani kabsa cheki Zanzibar na baadhi ya sehemu za Tanganyika kuna Polisiccm wameua wamejeruhi watu ni uvunjifu wa Amani huo lakini watu wanaendelea kuvulia
 
[emoji23] wamekuonesha IDs zao kuwa ni wasimamizi? Pia unajua wale wanaoongelea Sana kuwa wameonewa ndo hao wa kwanza kufanya udanganyifu. Yale mabegi yote yalikua ya chadema kuimplant uvunjifu wa amani na kumaster mind one thing " kukataa matokeo" you all know that.
hao wanafunzi, walimu na wafanyakazi wengine wa serikali walioshiriki kwenye udhalimu ni ndugu zetu na marafiki zetu, wanaongea kila kitu,siku zote siri huwa ya mtu mmoja, ukishamshirikisha mtu wa pili sio siri tena,so kawadanganyeni vijijini ila sio mjini kwa watu wenye elimu zao na akili zao timamu, una bahati mods wanafuta maneno yangu mengine
 
Ile kauli ya kuwambia wakurugenzi kuwa nakuteuwa,nakulipa mshahara,nakupa na Gari. Alafu unamtangaza mpinzani mshindi.
IMEMPONZA SANA.
 
Thibitisha....wananchi hawajakubali madini yao kuwekwa rehani ndio kisa cha kumpigia kura za upendo na wivu mkubwa Rais Magufuli.

Hongera CCM

Congratulations in advance President Magufuli
CCM KWA MAENDELEO YA TANZANIA
huo upupu wataamini watu wa vijijini labda lakini sio mjini watu wenye elimu zao na akili zao, walioshiriki udhalimu ni ndugu zetu, marafiki zetu na wanaongea kila kitu, hakuna siri ya zaidi ya mtu mmoja chini ya jua, mkae mkijua maovu yenu yote yanajulikana na dunia nzima inajua mmetengeneza kura nyingi tu kabla ya uchaguzi wenyewe, hata mahesabu yamewashinda,idadi ya waliopiga kura za ubunge kwenye jimbo hazilingani na idadi ya wapiga kura za uraisi kwenye jimbo hilohilo, kwa hiyo mnataka kusema kuna watu wengi tu walipiga kura za uraisi ila hawakupiga za ubunge
 
Ushindi ni wa ccm, kwann usiwapongeze tu na kuongelea Tz mpya ya kijani itakavyokuwa bila kasoro za kupingwa na wapinzani?
Haitawezekana.maana halisi ya mpinzani ni MTU aliyejitambua,akaona mapungufu na kuyasemea,hivyo ndo maana ya upinzani.
Kwa hyo kwa miaka hii mitano ya chama kimoja itazalisha wapinzani wengi maradufu.
 
Haitawezekana.maana halisi ya mpinzani ni MTU aliyejitambua,akaona mapungufu na kuyasemea,hivyo ndo maana ya upinzani.
Kwa hyo kwa miaka hii mitano ya chama kimoja itazalisha wapinzani wengi maradufu.
Wapinzani wa ndani ya chama cha ccm?Embu fikiri tena boss.
 
Congo ilisababishwa na uonevu unyanyasaji uovu mateso kama haya ya sasa CCM kuwapiga risasi kuwabambikia kesi kesi manyanyaso kuwapora ushindi wapinzani kwa njia haramu za kishetani
Hiyo sio root cause hata kidogo.
 
huo upupu kadanganyeni vijijini ila sio mjini kwa watu wenye elimu zao na akili zao timamu, hata mahesabu yamewashinda kujumlisha, total ya wapiga kura za ubunge kwenye jimbo hazilingani na total namba za wapiga kura za uraisi kwenye jimbo hilohilo, na kwa taarifa yako hao wanafunzi wa vyuo,walimu,wafanyakazi wa sekta zingine serikalini wote walioshirikisha kwenye udhalimu ni ndugu zetu, marafiki zetu na wanaongea ukweli mtupu.
Kumbe ww msomi [emoji23][emoji23] Na mtoto wa mjini sio? Basi leta facts za kisomi na za kimjini ndugu acha kulalamika total za wabunge na presidential haziwezi lingana kwani kunawatu ambao tumevote for presidential post pekeake na kwasaabu mbalimbali nyingine inapelekea kutokea kitu Kama hicho.
 
Back
Top Bottom