Ndugu zangu nisaidieni ujanja ili nitambue dhahabu halisi na feki

Ndugu zangu nisaidieni ujanja ili nitambue dhahabu halisi na feki

Morning Fam,

Kimsingi licha ya exposure katika mambo mengi tu yakiwamo mahusiano, magari, fashions na teknolojia nikiri tu kuna maswala mengine niko katika ujima.

Hivi karibuni nimekumbwa na kipengele, nataka nikanunue Gold jewelleries zikiwemo hereni, chain na pete ila sasa kimsingi sijui whats the difference between a real Gold and fake chain. Japo najua composition yake inapimwa kwa Karats kuanzia 12 mpaka 24.

Msaada kwa ambaye ni mzoefu wa haya mambo hasa warembo na washua wa humu JF! Maybe store ambayo ni genuine kwa kuuza hayo mavitu maana nimeenda City Mall pale nikakagua mali kwenye jewellery stores 2 ila still nna maseke.

Pia bei ya gold imesimamaje per gram sababu kuna ambao wanauza 175K per gram kwa 18 karats na wengine ni 190k kwa 21 karats. Katika story niliwahi kusikiaga gold ni 150k per gram.
Dah mkuu nikajua unataka kuja chunya tufanye biashara
 
Kuna kitu kimoja ambacho kinapandisha thamani ya gold nacho ni purity. Unaweza kuona gold ina ng'aa lakini purity ipo below 60% asilimia inayobaki ni copper, silver na iron.

Kama utaweza nenda kwenye duka ambalo wana purity machine, unanunua kitu kulingana na ubora wake. Inatakiwa iwe juu ya 85% gold.

Angalizo, purity machine inaweza kuchezewa.
Ila unajua huwezi tumia pure gold kutengeneza vito sababu pure gold ni soft na inatabia ya kulainika kwenye mazingira fulani na kuharibu umbile halisi la pete.

Ila ni lazima ichanganywe kidogo na madini mengine kuipa uimara unaotakiwa iweze kuwa imara na isipoteze umbile lake.
 
Back
Top Bottom