Ndugu zangu Waislam mtaniwia radhi kidogo

Status
Not open for further replies.
Hapo vizuri
 
Kwamba Tabora hakuna Waislamu?
Shinyanga Kuna wapagani na Wakristo tu?
Singida yenyewe utasemaje?
Vipi kuhusu kigoma?
Mbeya?
Ruvuma?

Sasa utalingansha uduni na umasikini wa Bukoba na mikoa uliyotaja?
 
Punguza chuki haya yapo moyoni mwako na pia hauna exposure ,jaribu kuzunguka.

Yaani hilo limekukaa rohoni kabisa..!
 
This is ....umepigilia msumari. Nimesoma kile kinachoitwa tamko la BASUTA ni aibu tupu. Badala ya kujadili hoja kwenye mkataba wa bandari, wao wamekuja na malalamiko, kusuta na kulialia dhidi ya tamko la TEC. Kama kuna mikataba mibovu huko nyuma na haikukosolewa, wao walikuwa wapi kuikosoa? Au tuache ubovu uendelee kwasababu huko nyuma ulikuwepo?...ni mawazo mgando yanayo onyesha ufinyu wa akili za watu.

Badala ya kumsaidia Rais wanaempenda kisa tu katoka kwenye dini yao, bila kujua wanaendelea kumfitinisha na umma kwasababu ya udini wao. Sina hakika kama SSH huwa anazipitia hizi nyaraka za watu wake hawa na kutafakari repercussions yake uko mbeleni.
 
Safari hii mmeshikwa pabaya mzee unapuyanga mno hata iko cheo cha uboss naona tukuvue tu jiite hoe hae tu kwa sasa
 
Hivi vyombo si ndo vimegawa rasilimali zetu zote.. Kila kitu si wamegawiya wageni. Unaikumbuka gas na madini vilivyochukuliwa.
 
Mimi nkajua tunachambua mkataba
 
KKKT wangeweza kuja na hoja kama za TEC ila wakaja kivingine bila kushambulia waraka wa wenzao. BAKWATA nao kama watakuja juu waje na hoja za kisomi wasije na mihemko ya kidini, vinginevyo wakae kimya kama hawana uwezo wa kujenga na kupangua hoja za mkataba wa bandari wasije wakaaibika waonekane hawana elimu na ni wadini. Na wale akina CCT na CPTC bora wabaki kimya wasije wakaonekana ni majuha katika kujenga na kupangua hoja wakaonekana wanatumika kisiasa kuunga mkono mikataba ya hovyo.
 
.
Assalam alaykum, warahmatullahi wabarakatuh.
Bila shaka mu wazima, nami nashukuru Mungu. Mzima wa afya. Nimewiwa kuandika barua hii baada ya kuona picha ikisambaa mitandaoni kuonyesha Wanafunzi wa Sekondari wakiwa wamevalia sare za shule na kubeba mabango mbali mbali yenye kusomeka.

"Tutaongozwa na Kanisa Katoliki mpaka lini? "TAMSYA hatudanganyiki"
"Unyanyasaji wa Waislamu mashuleni ukomeshwe"

Na mengineyo kadhalika, yenye kuonyesha malalamiko ambayo yana mizizi ya chuki ndani yake.

Kama zilivyo nchi nyingine, ndivyo na nchi yetu imepitia katika vipindi tofauti vya Kihistoria, hivyo basi, vipindi hivyo ndivyo vimepelekea mifumo ya Kijamii, Kiuchumi na Kisiasa iliyopo sasa. Hatuwezi kubadili Historia ya vipindi hivyo, ila inawezekana kwa asilimia mia kubadili mifumo inayodhaniwa kuwepo leo hii, na kama haipo, basi inawezekana kubadili mitazamo iliyopo leo hii.

Kabla ya Tanzania, kulikuwapo na Tanganyika na Zanzibar, hizi zote ziliundwa na watu wa dini tofauti, dini ya Kiislamu ikitamalaki eneo la Zanzibar na Pwani ya Tanganyika na Ukristo ukiwa eneo la Nyanda za Kaskazini, Juu kusini, Kanda ya Ziwa na kwengineko. Hii haikumaanisha kuwa, eneo zima la Tanganyika halikuwa na Waumini wa dini ya Kiislamu, maeneo kama Ujiji-Kigoma na Tabora, zilikuwa nim ngome muhimu za Wafanyabiashara wa Kiarabu.

Ndugu zetu linapokuja suala la elimu, historia iliwaacha nyuma, na hii ni kwa sababu kuu mbili.

1. Eneo la Pwani ya Mashariki lililokuwa chini ya ustaarabu wa Kiarabu wenye imani ya dini ya Kiislamu. Hivyo basi, haikuwa rahisi kwa Wakoloni Wa Tanganyika, yaani Wajerumani na Waingereza baadae kuleta Ustaarabu mpya.

Ikumbukwe kwamba, Utamaduni wa Kimagharibi ulienezwa kupitia dini na Elimu. Eneo la Pwani halikutawalika kirahisi kiasi cha kupenyeza dini, na changamoto ni kuwa, hata Elimu yao ilipitia kwenye mikono ya Wamishionari wa dini ya Kikristo. Hata ingekuwa umekuja kutawala wewe, hili eneo ungelipa kipaumbele?

Wakati Wajerumani wanawasili Tanganyika, Makabila yaliyoanza kuonesha upinzani mkubwa ni ya maeneo ya Pwani, yakiongozwa na Wahafidhina wa dini kama Chifu Bwana Heri na Abushiri, kule pangani na Kilwa kwa sababu yenyewe hayakuwachukulia kama Wakoloni tu, bali maadui katika imani.

Wamisionari wengi walikufa eneo hili, wenye bahati waliishia kufukuzwa. Hivyo, hakuna namna elimu ya Kimagharibi yenye chembe za Ukristo ingeweza kustaarabisha eneo hili. Hapo ndipo mwanzo wa eneo hili la Pwani ya Tanganyika kuwa na kiwango kidogo cha kundi la watu walioelimika. Kuanzia kwa Wasambaa Tanga, mpaka kwa Wamakonde, Mtwara.

Makabila kama Wachaga, Wasukuma, Wanyakyusa na Wahaya walipata fursa ya kupata elimu kwa sababu waliwapokea Wazungu si tu kama Watawala wao, bali ndugu katika imani. Wao walianza kunufaika hapa.

2. Dini ya Kiislamu inatoa msisitizo sana kwa elimu ya dini tu, na kutia mkazo mdogo kwa elimu dunia. Jambo ambalo kwenye dini ya Ukristo linakinzana na fundisho la Mithali 4:13, linalosisitiza kuishika elimu bila kuacha iende zake. Hata baada ya uhuru, muamko wa elimu katika maeeno haya bado ni mdogo, na changamoto kubwa ni moja, popote ambapo Wamisionari walijenga Kanisa, waliambatanisha na huduma za kijamii kama Elimu na Afya. Ni nani asiyezihitaji? Ndio mwanzo wa kukusanya watu wengi, na kuongeza idadi ya waumini waliovutiwa na huduma hizi, jambo ambalo Wafanyabiashara wa Kiarabu hawakufanya.

Ikumbukwe pia, Waarabu hawakuja kama Wakoloni, bali Walowezi na Wafanyabiashara, hivyo suala la kujenga miundombinu kama hii halikuwa lao. Sasa, nani alaumiwe? Jukumu lililopo sasa ni kunyanyua elimu bila kujali ukanda, dini au kipato cha mtu, bali tu kuutazama Utanzania wake.

Ndugu zangu, sitaki nikizungumzie chama cha All Muslims National Union of Tanganyika (AMNUT) cha mwaka 1948, chama ambacho kilitaka Tanganyika isifikie uhuru wake mpaka Wakristo na Waislamu wafikie hadhi sawa ya Elimu na Madaraja ya Kijamii. Harakati zile zisingetufikisha kokote, kwa sababu kila kitu kwenye nchi hii kingepimwa kwa vigezo vya dini hizi mbili. Naomba niwakumbushe, wakati wa harakati za kupigania uhuru, watu wote walishirikiana kupigania mamlaka ya taifa hili bila kutazamana imani zao, bali utaifa wao. Hatimaye, mwaka 1961, Tanganyika na badae 1963 Zanzibar zikawa huru. Sitaki kuizungumzia Zanzibar yenye 99% Wakazi-waumini wa dini ya Kiislamu, ambapo sitaki kuangazia waumini wa dini nyingine wanaishi vipi, lakini baada ya uhuru, nimesikitika kusoma baadhi ya Historia na kukuta kuwa kuna kundi kubwa la Waislamu lilimtazama Mwl. Julius K. Nyerere kwa jicho la dini yake na haswa Ukatoliki wake.

Sikatai kwamba; kuna namna Fulani kubwa tu, Ukatoliki una ushawishi mkubwa katika mwenendo wa siasa za nchi hii, lakini sio dini wala dhehebu linaloongoza nchi, bali siasa yake inatokana na idadi ya waumini iliyonayo nchini, taasisi zake ambazo zilitaifishwa, kama Shule na Hospitali, lengo likiwa ni kutoa fursa kwa watu wote bila kujali jinsia zao wapate elimu na huduma ya afya.

Pili, Kanisa hili ni mlezi wa Wanasiasa wengi nchini, naam, wengi sana. Wingi wake haimaanishi wanalitumikia, bali wana heshima nalo, na hili linatokana na mchango ambao kanisa hili limefanya kwao, mchango wa malezi yao. Wapo Maraisi waliotawala kwenye nchi hii ambao si Wakatoliki, lakini kwa bahati mbaya pia si Walutheri, Wasabato, Wala Wapentekoste. Bali ni Waumini wa dini ya Kiislamu mfano mzuri ukiwa Rais wa sasa.

Malalamiko yenu ya siku zote ni kuwa nchi inaongozwa na Kanisa. Jambo ambalo halina mashiko, na bahati mbaya sasa mnalipeleka kwa watoto. Watoto wa dini hizi mbili, watatazamana vipi? Wakiingia katika mzozo wa kurithishwa chuki, na wakija kutambua kama walilishwa uongo wenye chuki ndani yake, nani alaumiwe? Watakuja kulilia na kupiga kaburi la nani?

Hata hivyo; ikiwa suala ni bandari basi nawashauri msisamie mnachokiamini, kwa sababu dini husimamia haki, kama mmeiona haki katika uwekezaji wa bandari, kuwapo na tamko kutoka kwenu na jamii na umma wa Kiislamu utawaheshimu, na si kuzijibu hoja za Baraza la Maaskofu Katoliki, kwa sababu, huu utakuwa ni mwanya kwa Wanasiasa kututawala kupitia dini. Ila, kwa kuwa tayari kuna utofauti, basi si kitu na wala si tatizo, ikiwa kila taasisi itasimamia msimamo wake kwa kulinda imani zote mbili ili kutoruhusu siasa kutugawa.

Zaidi ningependa kuwaomba suala hili liishie kwenye mikono yetu kama Walezi wa watoto, naomba nichukue nafasi hii kama Mwalimu, kuwalinda kundi hili lisilo na uelewa mpana juu ya masuala haya yanayoendelea, na ikiwa picha hii tajwa hapo juu ni ya muda mrefu, ila Kisiasa imesambazwa hivi sasa naomba uwajibishwaji wa wahusika ufikike.

Nawatakia utekelezaji Mwema wa Majukumu ya malezi ya Kiroho kwa umma wa Mwenyezi Mungu (SAW).

Mpendwa, Diwani
 

Wakoloni na wale waliokuwa wafanya biashara wakubwa wa watumwa wakiona huu uzi wanacheka sana.
 
Kichwa cha habari hakina mantiki....

Waumini wa dini hiyo ni wengi...


Nilitegemea kichwa kiwe "....kwa hao waliotoa hilo tamko"....

Leo unaleta hoja kwa waumini wote wa dini huku ukihanikiza KEDI ,DHARAU NA CHUSHO.... upumbavu huu.....

Kama ni kweli kilichosemwa na TAMSIYA wajibu wao na si waumini wote....

TAMSIYA ni sawa na taasisi nyinginezo za dini ambazo tumeona TEC ikipinga uwekezaji ,KKKT ikiunga mkono uwekezaji.....sasa hapa huwezi kuwasema WAKRISTO wote na kuwashambulia....huo utakuwa ni upumbavu mwingine.....

Mwisho wa yote ,sisi ni watanzania na taifa letu haliwezi kugawanywa kwa ukinzani wa hoja za makundi na taasisi......

#TanzaniaMojaMilele[emoji120]

#Hakuna Mwenye Misuli ya kuligawa taifa hili [emoji120]
 

Umeongea vizur ila lengo lako ni bandari na sio hao wanafunzi Wenye mabango "TUTAONGOZWA NA KANISA MPAKA LINI".

NA KUHUSU KUONGOZWA NA KANISA NI HAKI YAO WAMEJIPANGA, HATA MUNGU HUMPA ANAEHITAJI NA ANAEHITAJI NI YULE ANAEHITAJI KWA MATENDO SIO BLA BLA, KANISA LIMEFANIKIWA KWA HILO.KAMA WAISLAM TUTAHITAJI KUONGOZA KANISA PIA NI LAZIMA TUJIPANGE SIO VIBAYA.

UISLAM NI MSAFI SALAMA SHIDA IPO KWA WAISLAM WENYEW [emoji16]

NJE YA MADA HIVI NI KWANINI WANAOSUPPORT DP WORLD WANAONEKANA NI WAISLAM NA HAWANA AKILI?
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…