Ndugu zangu wakatoliki, mliwafanyaje wasabato? Malizeni tofauti zenu.

mcTobby

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2018
Posts
4,072
Reaction score
12,119
Kuna sehemu niliwahi kukaa jirani na kanisa la wasabato. Almost 80 % ya mahubiri niliyokuwa nayasikia ni kuwaponda wakatoliki. Kwamba wao ndio yule joka kuu, mara mwanamke yule kahaba mkuu aliyezini na wafalme wa dunia. Mara papa ni king wa freemason . Wakawa wanadai kwamba wakatoliki wanaabudu sanamu na mizimu (saints) . Yaani kila jambo baya kwenye hii dunia ,reference ni roman Catholic 🤔🤔

Huyu pasta wa kisabato alikuwa Anatoa references kwenye kitabu cha ufunuo wa yohana na baadhi ya vifungu fulani fulani ndani ya bible ili ku justify kile anachokisema dhidi ya wakatoliki. Na hii sio mara moja au mara mbili. Yaani ni kila siku ya ibada. Dear wasabato swali langu kwenu je, ibada haiwezi kukamilika pasipo kuwataja wakatoliki?
😊😊😊
Hata sisi walutheri tulijifanya tunajaribu ku temper na mamlaka ya pope enzi za kina Martin luther ,lakini tulichemka.🤣🤣🤣
NB: Tupendane na tuchukuliane kwa kila hali . Tusijivike koti la chuki za kidini.
 
Kukaa na kuanza kuponda dini ya mwenzako ni ushamba.

Usabato wangu, Usunni, Ushia, Ulutheran Ukatoliki unanisaidia nini kama nawatendea wengine vibaya?

Kwanini tusikae tukaanza kupondana kuhusu matendo yetu mabaya?

Hizi habari mnavyosali nyinyi sio sahihi inabidi mfanye hivi ni utapeli mkubwa sana.

Tunayaficha madhambi yetu kwenye kivuli cha dini.

WANAFIKI WAKUBWA WOTE WANAOABUDU DINO NA KUMUACHA MUNGU.
 
Religion is the opium of the people.

Dini inaweza kumfanya mtu akasahau reality ya maisha, ndio maana yupo tayari mtu kutafuta hata million moja ili akatafute muujiza kwa Mwamposa badala ya kuwekeza hiyo hela afanye biashara.
 
Dini ni kofia au kilemba kinachotumika kutawala watu waendelee kuwa kondoo na wasiwe huru. Dini ya kweli ni upendo (upendo wa kweli pasipo na mawaa wala hila). Hayo madhehebu yote yanarahisisha kuwagawa kondoo na wafuasi ili watawaliwe vizuri na kiulaini.

Ukiujua na ukiufahamu ukweli utakuwa huru.
 
Kukaa na kuanza kuponda dini ya mwenzako ni ushamba.

Usabato wangu, Usunni, Ushia, Ulutheran Ukatoliki unanisaidia nini kama nawatendea wengine vibaya?

Kwanini tusikae tukaanza kupondana kuhusu matendo yetu mabaya?

Hizi habari mnavyosali nyinyi sio sahihi inabidi mfanye hivi ni utapeli mkubwa sana.

Tunayaficha madhambi yetu kwenye kivuli cha dini.

WANAFIKI WAKUBWA WOTE WANAOABUDU DINO NA KUMUACHA MUNGU.
Badala ya kushindana kufanya kheri wao wanashindana ikitkadi zao.

Mashindano ya kusaidia mafukara , watoto yatima ndiyo mambo sahihi..
 
Kukaa na kuanza kuponda dini ya mwenzako ni ushamba.

Usabato wangu, Usunni, Ushia, Ulutheran Ukatoliki unanisaidia nini kama nawatendea wengine vibaya?

Kwanini tusikae tukaanza kupondana kuhusu matendo yetu mabaya?

Hizi habari mnavyosali nyinyi sio sahihi inabidi mfanye hivi ni utapeli mkubwa sana.

Tunayaficha madhambi yetu kwenye kivuli cha dini.

WANAFIKI WAKUBWA WOTE WANAOABUDU DINO NA KUMUACHA MUNGU.
Kkweli tupu...kwa tunaoamini...si ukatoliki wangu...au ulterior wako...au uislamu wako utakaokuingiza mbinguni au kukupa pepo

Dini ya kweli ni namna gani unaishi na wenzako
 
Ushamba wao tu alafu,ila katoliki ni zaidi ya kanisa yani ni taasisi iliyo kamilika.
Ni taasisi ambayo iPo well organised kwa kweli. Ni ngumu hata kusikia mgogoro baina yao.
 
Ukatoliki hauna ugomvi na madhehebu mengine Wala hauwezi kuta wakatoliki wakiwasema wengine vibaya
.Ni inferiority complex tu ya wasabato
 
Hiyo sio maana ya dini,dini zimekuwepo kwa ajili yakuleta utu,upendo,hekima..,msipotoshe maana ya dini,vitu hivyo vikikoseka inakuwa si dini.
 
Wasabato ni Wayahudi walioamua kumfata yesu.

Wasabato ndo waamini wanaosoma maandiko bila kujua kuyatafakari
 
Kuna sehemu niliwahi kukaa jirani na kanisa la wasabato. Almost 80 % ya mahubiri niliyokuwa nayasikia ni kuwaponda wakatoliki. Kwamba wao ndio yule joka kuu, mara mwanamke yule kahaba mkuu aliyezini na wafalme wa dunia. Mara papa ni king wa freemason . Wakawa wanadai kwamba wakatoliki wanaabudu sanamu na mizimu (saints) . Yaani kila jambo baya kwenye hii dunia ,reference ni roman Catholic 🤔🤔

Huyu pasta wa kisabato alikuwa Anatoa references kwenye kitabu cha ufunuo wa yohana na baadhi ya vifungu fulani fulani ndani ya bible ili ku justify kile anachokisema dhidi ya wakatoliki. Na hii sio mara moja au mara mbili. Yaani ni kila siku ya ibada. Dear wasabato swali langu kwenu je, ibada haiwezi kukamilika pasipo kuwataja wakatoliki?
😊😊😊
Hata sisi walutheri tulijifanya tunajaribu ku temper na mamlaka ya pope enzi za kina Martin luther ,lakini tulichemka.🤣🤣🤣
NB: Tupendane na tuchukuliane kwa kila hali . Tusijivike koti la chuki za kidini.
Uzuri wa sisi wakatoliki;
1. Ukituponda tunakusikiliza, ukimaliza tunaenda kwenye kitimoto na bia halafu nyumbani
2. Dominika tunakwenda kanisani kwenye misa kisha tunapitia baa na kwa ajili ya kitimoto na bia
3. Hatulazimishi mtu kuamini tunachokiamini. Ukiona unataka kujiunga nasi, wewe mwenyewe tafuta kanisa lilipo, uende ukasadiki basii..!!!
 
Hiyo sio maana ya dini,dini zimekuwepo kwa ajili yakuleta utu,upendo,hekima..,msipotoshe maana ya dini,vitu hivyo vikikoseka inakuwa si dini.
Upo sahihi . Je, kwanini sasa dini fulani inamponda dini nyingine kwamba haipo sawa ilihali na yenyewe ina makandokando mengi?
 
Religion is the opium of the people.

Dini inaweza kumfanya mtu akasahau reality ya maisha, ndio maana yupo tayari mtu kutafuta hata million moja ili akatafute muujiza kwa Mwamposa badala ya kuwekeza hiyo hela afanye biashara.
Kila kitu ni Imani hata biashara bila Imani utoboi
 
Back
Top Bottom