Uchaguzi 2020 Ndugu zangu wanaCCM kweli tulikosea, tuchutame

Uchaguzi 2020 Ndugu zangu wanaCCM kweli tulikosea, tuchutame

Man Mvua

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2016
Posts
2,183
Reaction score
3,521
Habarini wanabodi,

Kwanza naomba nitamke wazi kwamba mimi ni mwanaccm kindakindaki na nimepanga 2025 kuonana na wajumbe.

Naomba niseme wazi kwamba ccm tulikosea kwenye vipaumbele vyetu, tuliegemea upande mmoja zaidi.( ujenzi wa miundombinu zaidi). Ni kweli Rais wetu kafanya mambo mengi sana mazuri na yenye tija kwa Taifa letu ila yote aliyofanya ilitakiwa yaendane na hali ya kiuchumi ya mtanzania mmoja mmoja. Rais wetu angekuwa Rais bora zaidi Duniani kama spidi yake ingeenda sambamba na yafuatayo:

1. Utoaji wa ajira kwa watanzania wanyonge (maskini) ambao wengi wao walisomeshwa na wazazi wao kwa shida kubwa na ndio wamejaa kwenye kada ya kilimo, Uvuvi, Ualimu na majeshi. RAIS ANAPOSEMA NI RAIS WA WANYONGE BILA KUFANYA HAYA ANAFIKIRISHA SANA kwa sababu hao wanyonge aliyofanya mengi hayawanufaishi kabisa ndio maana katika hili hatuna hoja.

Kuwaambia vijana wajiajiri ni kuwakosea sana mana Madaktari na maprofesa waliopo CCM wangekuwa mifano katika hili, pia wabunge wote baada ya kupokea 240M wangekuwa mifano mizuri sana katika hili, lakini wapiiii !! Wote wameenda majimboni kutafuta ajira kwa wananchi pamoja na kwamba wana mitaji.

Juzi Donard Trump alikuwa anajidai kwa kuzalisha ajira 1.5M ndani ya miezi miwili. Hili tunalizungumziaje wana CCM?

HOJA YA AJIRA TUKUBALI TUMEFELI VIBAYA SANA, tumefikia hatua kuwaambia wananchi wajitolee huku majukwaani tukijidai nchi ina pesa na ni tajiri. Vituko kwa kweliii

2. Mishahara kwa wanafanya kazi wa nchi hii. Hapa pia tukubali kwa miaka 5 hatukutenda haki kwa wafanyakazi, tuliwaongopea miaka yote minne labla tulidhani miaka 5 ni mingi sana. UKWELI MCHUNGU HAPA TUSHAUMIA SANA. WANACCM HAPA HATUNA HOJA, TUCHUTAME.

3. Vyeo na madaraja. Tumeshuhudia majeshi yetu yakipewa vyeo na kupanda madaraja kwa kipindi chote cha miaka 5 ila kada zingine tangu 2013/2014 watu hawajapanda madaraja kwa kuwa hakuna pesa, hapa tulikosea sana tungepandisha kidogo kidogo tangu 2015 sa hivi tungekuwa hili tatizo tushalimaliza kabisa. Kwenye kada ya Elimu hiki ni kilio kikuu.

4. HAKI, SHERIA NA WAJIBU, nadhani hatujui kutofautisha hivi vitu vitatu.

5. RUSHWA. Hapa napo CCM hamna kitu tumefeli pia. RUSHWA AKITOA MASKINI AU ASIYE NA JINA, AKITOA TAJIRI AU MWANACCM NI TAKRIMA.

6. Ule msemo wa wanaolalamika ni wezi au wamebanwa kwenye mambo yao ulikuwa wa KUPOTOSHA na kumpoteza Mh: Rais. Wanyonge wengi wa Mh.Rais walikuwa wakilalama hali ngumu WATEULE wake walikuwa wana mwambia hao ni wale MAFISADI uliowatumbua. WASAKATONGE MMETUHARIBIA CHAMA.

Mwisho

Wana CCM tujipange kisawasawa kutengua hoja za wapinzani wana hoja muhimu sana, kamwe huwezi kusifia ujenzi wa miundombinu wakati tumbo lipo tupu (wanufaika wa utawala huu kaeni pembeni kidogo tuokoe chama).

TUSIKOSEE TENA KWENYE ILANI YETU IJE KUMNUFAISHA MTANZANIA MMOJAMMOJA NA SIO PESA ZOTE KWENDA NJE KWENYE UNUNUZI WA NDEGE.

Mwisho kabisa

Tuombe msaada kutoka kwa comrade kinana, Nape na Makamba. Watusaidie mbinu maana tumeshikwa pabaya.

Ahsanteni sana.
 
Eti Meko utamsikia, "Tumenunua ndege" mara utamsikia "Tumejenga mafly over" kisha "Tumehamia Dodoma"

Hivi hata tukihamia Dodoma wakati mwananchi wa hapa Utegi anaishi kwa mlo mmoja, tunapata faida gani?

Au hata tukinunua ndege 800 wakati mwalimu wa kule Ng'ong'ona ana utitiri wa madeni yatokanayo na mahitaji ya kila siku ya nyumbani, tutakuwa tumenufaika au tumeathirika?

Magufuli asithubutu kujigamba kwa hivi vitu vyake wakati kampeni za uchaguzi zitakapoanza. Watu hawataki kuvisikia kwani haviwanufaishi walio wengi, badala yake vimesababisha waishi maisha ya kinyama.
 
Man Mvua,

Kati ya makosa makubwa CCM watajilaumu kumuacha akazuia Shughuli za Vyama vya siasa na kudhulumu uchaguzi wa Serikali za mitaaa mwaka jana ndio matokeo yake tunayaona leo

WANANCHI KOTE NCHINI BARA NA VISIWANI WAMEKUA NA SHAUKU KUBWA SANA YA KUWASIKILIZA WAPINZANI KINYUME KABISA NA MAWAZO KUWA WANGEKATA TAMAA

Kiukweli kupitia hili CCM wajifunze ;ingekua wapinzani wanapata muda wa kusema miaka mitaano hii bila kunyanyaswa leo hawangekua na la kuwaambia watu

Binadamu huna jipya la kuwafanyia au kuwapa ; WAPE KILA KITU ILA USIWANYIME MDOMO KUSEMA NA MASIKIO KUSIKIA. Dola na Vyama vyenye Nguvu duniani zilifanya Maendeleo makubwa Lakini zilianguka kwa sababu tu waliziba watu midomo.

Leo CCM haipo kwa watu kabisa zaidi ya kwenye Dola tena kwenye dola sio wote bali wale wenye mamlaka

Wanamikakati wa CCM wamempotosha Sana Mwenyekiti

Mwaka Huu ni maeneo machache sana CCM inaweza kushinda kihalali Hii ni tofauti kabisa na miaka mitano nyuma Pamoja na kazi nzuri iliyofanywa.

SEKRETARIET ya CCM imeuwa Chama kwenye mioyo ya watu!

Baada ya uchaguzi Huu lazima mabadiliko makubwa yafanyike kwenye sekretariet ya CCM ile ya kina Kinana na Nape was far better kwakua ilikua na approach ya kutumia siasa zaidi kuliko kutegemea kubebwa na Dola nzima.
 
Siku hizi makamanda wa CHADEMA wanajigeuza na kuwa wanaCCM huku wakitoa eti ushauri na maoni yao!

Unatumia picha ya Marehemu aliyekuwa Mbunge wa Mafia, Abdulkarim Shah halafu unajiita mwanaCCM!

Hizi ni propaganda za kitoto sana!
Mnapenda kujimilikisha vitu na ubinafsi tu. Kwa hiyo mwana mbogamboga ni wewe tu?

Huko kwenu hakuna msemakweli ndio maana umemuita muandishi kuwa ni CHADEMA. Rudisheni CCM ya wakulima na wafanyakazi, CCM ya Mwalimu Julius Nyerere.

Hayati Mkapa alisema hakuna kujimilikisha chama, ooh CCM ya Magufuli, CCM ya MsemajiUkweli .

Acheni ubaguzi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siku hizi makamanda wa CHADEMA wanajigeuza na kuwa wanaCCM huku wakitoa eti ushauri na maoni yao!

Unatumia picha ya Marehemu aliyekuwa Mbunge wa Mafia, Abdulkarim Shah halafu unajiita mwanaCCM!

Hizi ni propaganda za kitoto sana!
Hivyo hivyo na jiwe alikuwaanaambiwa kuwa watu wanahali mbaya! yeye anawaita mafisadi! Mwana ccm mwenzio ametoa ushauri ili mnusulike na kifo Cha uchaguzi, wewe unaleta pumba! aliyosema sio kweli?
 
Siku hizi makamanda wa CHADEMA wanajigeuza na kuwa wanaCCM huku wakitoa eti ushauri na maoni yao!

Unatumia picha ya Marehemu aliyekuwa Mbunge wa Mafia, Abdulkarim Shah halafu unajiita mwanaCCM!

Hizi ni propaganda za kitoto sana!
Ndicho kitu kinachofanya CCM mzidi kupoteana na kuonekana kituko mbele ya raia. Mmeamua kuwa kila anayetetea wananchi wa kawaida ni mpinzani. Kama ni hivyo naomba niwapongeze sana wapinzani wa CCM.
 
Hoja kuntu hizi, hongera sana mleta mada huu ni ukweli mtupu.

Ongezea pia matendo ya kiuonevu kama kuvunjia watu nyumba zao wakati kuna zuio la mahakama

Pia Matendo ya wasiojulikana, kukumbatia viongozi wasio na nidhamu kama Makonda na kutojali hisia za wajanga wa majanga kama vile kauli zilizotolewa huko Kagera baada ya tetemeko ziliwafanya wananchi waione serikali hii siyo ya utu!
 
Magufuli ni mchoyo sana selfish vijana kila siku wanakulilia ajira wewe huwapi na ukitoa niza kiubaguzi.

1. [emoji117]Unaajiri walimu wa sayansi tu je hao wa art wao wafanye nini?

2. [emoji117]Unaajiri vijana wa jkt walio jenga jenga majengo tu je hao waliopo kwenye makambi au vikosini wakiendelea na shughuli za uzalishaji mali wao huwaoni?

3.[emoji117]Watu wa afya Unaajiri idadi isiyo kidhi mahitaji ilhali wapo wengi mtaani.

4.[emoji117]Kuna baadhi ya sekta na taasisi tangu uingie madarakani haujawahi kuajiri kabisa tatizo nini?

Kama upo humu ndani ukasoma hili bandiko basi lifanyie kazi kwa kuwakumbuka vijana na wao watakukumbuka daima. Maisha tunapita
 
Back
Top Bottom