Man Mvua
JF-Expert Member
- Apr 12, 2016
- 2,183
- 3,521
Habarini wanabodi,
Kwanza naomba nitamke wazi kwamba mimi ni mwanaccm kindakindaki na nimepanga 2025 kuonana na wajumbe.
Naomba niseme wazi kwamba ccm tulikosea kwenye vipaumbele vyetu, tuliegemea upande mmoja zaidi.( ujenzi wa miundombinu zaidi). Ni kweli Rais wetu kafanya mambo mengi sana mazuri na yenye tija kwa Taifa letu ila yote aliyofanya ilitakiwa yaendane na hali ya kiuchumi ya mtanzania mmoja mmoja. Rais wetu angekuwa Rais bora zaidi Duniani kama spidi yake ingeenda sambamba na yafuatayo:
1. Utoaji wa ajira kwa watanzania wanyonge (maskini) ambao wengi wao walisomeshwa na wazazi wao kwa shida kubwa na ndio wamejaa kwenye kada ya kilimo, Uvuvi, Ualimu na majeshi. RAIS ANAPOSEMA NI RAIS WA WANYONGE BILA KUFANYA HAYA ANAFIKIRISHA SANA kwa sababu hao wanyonge aliyofanya mengi hayawanufaishi kabisa ndio maana katika hili hatuna hoja.
Kuwaambia vijana wajiajiri ni kuwakosea sana mana Madaktari na maprofesa waliopo CCM wangekuwa mifano katika hili, pia wabunge wote baada ya kupokea 240M wangekuwa mifano mizuri sana katika hili, lakini wapiiii !! Wote wameenda majimboni kutafuta ajira kwa wananchi pamoja na kwamba wana mitaji.
Juzi Donard Trump alikuwa anajidai kwa kuzalisha ajira 1.5M ndani ya miezi miwili. Hili tunalizungumziaje wana CCM?
HOJA YA AJIRA TUKUBALI TUMEFELI VIBAYA SANA, tumefikia hatua kuwaambia wananchi wajitolee huku majukwaani tukijidai nchi ina pesa na ni tajiri. Vituko kwa kweliii
2. Mishahara kwa wanafanya kazi wa nchi hii. Hapa pia tukubali kwa miaka 5 hatukutenda haki kwa wafanyakazi, tuliwaongopea miaka yote minne labla tulidhani miaka 5 ni mingi sana. UKWELI MCHUNGU HAPA TUSHAUMIA SANA. WANACCM HAPA HATUNA HOJA, TUCHUTAME.
3. Vyeo na madaraja. Tumeshuhudia majeshi yetu yakipewa vyeo na kupanda madaraja kwa kipindi chote cha miaka 5 ila kada zingine tangu 2013/2014 watu hawajapanda madaraja kwa kuwa hakuna pesa, hapa tulikosea sana tungepandisha kidogo kidogo tangu 2015 sa hivi tungekuwa hili tatizo tushalimaliza kabisa. Kwenye kada ya Elimu hiki ni kilio kikuu.
4. HAKI, SHERIA NA WAJIBU, nadhani hatujui kutofautisha hivi vitu vitatu.
5. RUSHWA. Hapa napo CCM hamna kitu tumefeli pia. RUSHWA AKITOA MASKINI AU ASIYE NA JINA, AKITOA TAJIRI AU MWANACCM NI TAKRIMA.
6. Ule msemo wa wanaolalamika ni wezi au wamebanwa kwenye mambo yao ulikuwa wa KUPOTOSHA na kumpoteza Mh: Rais. Wanyonge wengi wa Mh.Rais walikuwa wakilalama hali ngumu WATEULE wake walikuwa wana mwambia hao ni wale MAFISADI uliowatumbua. WASAKATONGE MMETUHARIBIA CHAMA.
Mwisho
Wana CCM tujipange kisawasawa kutengua hoja za wapinzani wana hoja muhimu sana, kamwe huwezi kusifia ujenzi wa miundombinu wakati tumbo lipo tupu (wanufaika wa utawala huu kaeni pembeni kidogo tuokoe chama).
TUSIKOSEE TENA KWENYE ILANI YETU IJE KUMNUFAISHA MTANZANIA MMOJAMMOJA NA SIO PESA ZOTE KWENDA NJE KWENYE UNUNUZI WA NDEGE.
Mwisho kabisa
Tuombe msaada kutoka kwa comrade kinana, Nape na Makamba. Watusaidie mbinu maana tumeshikwa pabaya.
Ahsanteni sana.