Utawala mbovu sana wa CCM ndio umetufikisha huku.Aisee kama Taifa bila kujali itiladi zetu za siasa naona tunaelekea kibaya snaa.
Hii ni michezo ya hatari sana, bahati mbaya binadamu ni wagumu kujifunza kutokana na historia.Vijana wa mbwa mwitu wanalipwa na nani na kuongozwa na nani, usalama wa ukoje kwa kiongozi wa dini kujisifu kuwa na kundi la mbwa mwitu wenye mafunzo?.
Maoni yangu.
Kundi hili huenda kwa sasa likaonekana zuri kwa kuwa linaonekana kuisaidia Serikali lakini baade huko mwelekeo wao ukabadilika na kuwa hatari kwa jamii na tukawa tunaelekea kuwa Nigeria.
Vyama vya siasa vilizuiwa kuwa vikundi vya ulinzi sasa huyu amepewaje ruhusa ya kuunda vikundi vya kudhuru watu.?Kama mtamzania niliyeishi kwenye tawala zote tangu tupatie uhuru hadi Leo hii nashindwa kujua.
Kumekuwa na matukio mengi sana hapa nchini yanafanyika kila kukicha hasa ya kutisha kabisa na mtu kama huna moyo unaweza ukajifungia ndani ukijua nje tayari Kuna Vita.
Ebu msikilizeni huyu mtu maneno anayotamka na yanafika kwa jamii.
Je ni mtamzania kweli au anatumia teknelojia ya kisiasa maarufu kama A I?
View attachment 3612438
acha kusingizia vijana, wahuni ni Samia na CCM, hao ndio watekaji, wauaji na wezi wa kura wameharibu mifumo yote ya sheria, ni kama hatuna mahakama au chaguzi za viongozi, uhuni mtupuvijana wasicheze na amani