Ni watu wasio na fikra pana. Soko ama liwe stand hii ni miradi mikubwa na ndo miradi kichocheo, haijengwi na na wananchi bali serikali ikiamua.
Kama sahivi wameamua itajengwa na ndo kupeleka maendeleo kwa wananchi. Na si hayo tu,
Wanaweka RC wanajeshi kila siku ili iweje, mbona kwingine wanapeleka watu wa maana wenye CV zao na madegree yao wanaojua kupambanua mambo sasa iweje washika mitutu Kagera enzi zote as if kuna vita ama ni darful. Sasa wanataka wananchi ndo wateue RC, hilo ni jukumu lao kweli?
Vyuo na taasisi za serikali tunaziona kwa mikoa ya wengine ila Kagera ahaa! Sasa wananchi waache kujenga vibanda vyao vya kuishi wakajenge ofisi za serikali?
Kilimo ndo hicho, mkoa unategemea kilimo kwa 70% lakini eti leo ndo wanaanza kujikosha, wananchi wakulima ndo wangenunua kahawa yao wenyewe ama serikali ilitakiwa kutafuta wanunuzi kwa wakulima wake. Leo sasa aliyeleta bei mpya ni wakulima ama serikali, siku zote ilikuwa wapi na walitegemea nini
nini kwa mkoa?
Usafiri si waliua meli ikawa hamna kwa miaka zaidi ya 15, walitaka wananchi wamudu vipi maisha yao?
Nchi hii basi tu, wabaya zaidi ni hawa watu wa jf waliopita shule lakini hata kuchambua mambo hawawezi na bado daily wanajaza saver. Hii siyo sawa kabisa.