Ndugu zetu wa Kagera kwanini mkoa wenu unaongoza kwa umasikini?

Ndio maana nikakuomba unitajie wewe ni tajiri unayetokea mkoa gani??!! Maana Ninachokiona hapa ni mihemko tu kwani viashiria vya umasikini ni vipi mkuu tajiri???
Watakuhangaisha Bure ukute mkoa anakozaliwa anaogopa hata kurudi tangu amepata bahati ya kuondoka. Wachagga huko kilimanjaro wamedumaa sasa hivi hata halmashauri zao kwenye mapato ya ndani hazina tofauti na kigoma [emoji23][emoji23]
 
Rweye umenena. Huu ndio uchambuzi wa kisomi.
Kagera imedumaa kwa sababu nyingi ikiwemo uwekezaji duni kutoka serikali kuu na kuwa na Ma RC wanajeshi mara kwa mara.

Alikuwepo RC Massawe alijitahidi sana kuendeleza mkoa wa Kagera. Alikuwa na mikakati ya kupambana na ugonjwa wa migomba wa mnyahuko. Alianza kujenga uzalendo wa kupenda mkoa wa Kagera kwa wananchi. Usafi ndani ya miji na vijiji ulikuwa unaanza kuwa tabia ndani ya jamii. Mh Masawe hakudumu.
 
ITV jana nao kwenye taarifa yao habari juu ya utaperi wa Qnet wilaya ya Ubungo wakamuonyesha mama wa Kihaya eti anashangaa "...eti na muhaya anatapeliwa na Qnet kweli?...muhaya huwa hatapeliwi kizembe..."
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…