Ndugu zetu waislamu ifike muda mpunguze malalamiko na mjitafakari

Wakristo wa nchi hii ukipita mitandaoni unaweza dhani labda wanaishi maisha ya kiwango cha juu wakati nao wanaishi kwa kuunga unga kama watz wengine.
ndio muache udini
 
Asante sana , nilichokiona naona na mwenzangu umekiona

Kwenye suala la Gaza nitatofautiana na wewe kidogo, ikumbukwe kwamba Gaza ina wakristo pia (sio wengi lakini wapo) na wanateseka kama Wapalestina wengine tu
Ndugu yangu, hiyo vita imepakwa rangi ya Udini lakini ukiangalia ndani kuna maslahi ya kibepari ya nchi za kimagharibi (wapagani hawa) na nchi za kiarabu (mgogoro kati ya Iran na Saudi Arabia)
Kiufupi, Palestina ni kete kama kete nyingine zinazotumika katika vita za wazito katika eneo hilo la mashariki ya kati
Unaandika Vyema.

Lakini Vita vya Israel na Palestine vina Viashiria vya Dini na Race.

Israel ana uadui wa kihistoria na wapelestina na Anatafuta Namna ya kuwaua na kuwadhoofisha kwa ajiri ya usalama wake kama ambavyo wapalestina watalipiza kisasi kadri watakapo pata nafasi.

Marekani lazima waisaidie Israel kwa sababu ya manufaa anayopata kutoka Israel sio kutokana na vita bali kutokana na ushirikiano uliopo na utegemezi wa marekani kwa Israel hasa katika masuala ya technologia.

Iran anatumia mgongo wa Kuwasaidia wapalestina kwanza ili apate attention from muslims around the world kwamba yeye amesimama na wapelestina (japo sio kweli ana malengo yake mengine kabisa).

Pili iran inataka kushika udhibiti wa maeneo matukufu ya kiislamu ya kihistoria hiyo itakuwa hatua muhimu katika kukuza itikadi zao za Kishia zinazokwenda kinyume na zile za kisunni(zenye waislamu wengi)
 
Acheni wivu wakristo, nyinyi pia mna taasisi zenu mnawaajiri waislamu huko?
Kumbe roho inwauma muislamu kumuajiri muislamu, kwanza wengi wenu sio waaminifu nani atawaajiri. Waislamu pamoja na mapungufu yao ila ni waaminifu zaidi kuliko nyinyi

Unachanganya uvumilivu katika dhulma na uaminifu, utaendeleaje bila kujiongeza ikiwa bosi anakulipa mshahara wa laki na nusu kwa mwezi na una familia yenye watoto watatu? Na ikumbukwe upo kwa huyo muajiri wako Jumatatu mpaka ijumaa
 
Katika huu uzi siongelei ndugu zangu Waislamu hawa "secular" wa mjini ambao wanaingia msikitini mara tatu kwa mwaka, ndugu zangu hawa ambao tunashinda nao kwenye mabaa, ndugu zangu hawa ambao wanachanganywa na mwanamke anaitwa Rose anasali kwa Mwamposa.

Uzi huu unalenga Waislamu ambao aidha ni swala tano au Uislamu wao ni wa muhimu kuliko Utanzania wao.

Kila nikiingia kwenye majukwaa ya mijadala kama Jamii Forums, nakutana na hoja zinazochochea makasiriko kutoka kwa baadhi ya Waislamu dhidi ya Wakristo. Hoja hizi mara nyingi huonyesha chuki, lawama, na hata ubaguzi wa wazi. Kwa haraka, ninapochukua muda kutafakari, naona kana kwamba sisi Wakristo hatuna chuki wala ubaguzi wa moja kwa moja dhidi yao. Badala yake, lawama na makasiriko yote huonekana yakitoka upande mmoja. Ni kwa sababu hiyo nimeamua kuandika makala hii, nikiwaomba ndugu zangu Waislamu wafanye tathmini ya kina kuhusu mambo haya kwa nia ya kujenga mshikamano bora.

1. Ajira katika Taasisi za Kidini

Katika jamii yetu, taasisi za Kikristo zinaongoza kwa kuwa na uwazi wa ajira kwa watu wa imani tofauti. Waislamu wengi wameajiriwa kwenye hospitali za Kikristo, shule, na hata benki zinazomilikiwa na makanisa, lakini ni mara nadra sana, au labda haipo kabisa, kuona Mkristo akiajiriwa kwenye taasisi za Kiislamu.

Ubaguzi wa ajira: Taasisi za Kiislamu zinaonekana kushindwa kuwahusisha Wakristo hata kwa kazi za chini kama ulinzi. Hali hii inaleta picha ya ubaguzi na ukosefu wa kujiamini kwa taasisi hizo.

Athari kwa jamii: Kama Wakristo wangekuwa na mtazamo sawa, ndugu zetu Waislamu wengi wangepoteza chanzo cha mapato, jambo ambalo lingeharibu ustawi wa familia zao.

2. Mfumo wa Elimu: Ushirikiano na Changamoto​

Shule nyingi za Kikristo nchini zimekuwa mfano wa ukarimu kwa kupokea watoto wa Kiislamu na kuwaheshimu kwa kuhakikisha mahitaji yao ya kidini yanazingatiwa. Kwa upande mwingine, taasisi za elimu za Kiislamu mara nyingi hazikubali wanafunzi wa Kikristo, na hata pale inapowezekana, hazina mipango ya kuwasaidia kufanikisha mahitaji yao ya kidini.

Ubora wa elimu: Shule nyingi za Kiislamu zimekuwa zikishika nafasi za mwisho kwenye takwimu za kitaifa. Ukosefu wa uwekezaji wa kutosha na mtazamo finyu wa elimu unaweza kuchangia hali hii.

Hitaji la kujifunza kutoka kwa wenzao: Taasisi za Kikristo zimeonyesha mafanikio makubwa, si kwa sababu ya chuki au ubaguzi, bali kwa kuwa na mfumo wa wazi unaowajumuisha wote bila kujali tofauti za kidini.

3. Utegemezi wa Misaada

Taasisi nyingi za Kiislamu zinaonekana kutegemea misaada kutoka nchi za Kiarabu kwa kila jambo. Hii ni changamoto kubwa kwa maendeleo ya ndani ya jamii ya Kiislamu nchini.

Kulegalega kwa juhudi za ndani: Kutegemea misaada ya nje kunalemaza uwezo wa jamii ya Kiislamu kujitegemea na kujenga taasisi imara.

Ukosefu wa mshikamano wa kitaifa: Badala ya kushirikiana na jumuiya zingine nchini, utegemezi wa misaada ya nje huongeza mgawanyiko wa kijamii na kiuchumi.

4. Kuimarisha Umoja kwa Kujifunza

Badala ya kushindana kwa chuki, jamii ya Kiislamu inaweza kujifunza kutoka kwa Wakristo juu ya kujitegemea na kushirikiana kwa manufaa ya wote. Ushirikiano wa kidini unaweza kufanikisha maendeleo ya kijamii na kupunguza chuki zisizo na msingi.

Kujifunza kutokana na mafanikio ya wenzao: Mifano ya mafanikio ya Kikristo inaweza kuwa darasa bora kwa Waislamu. Hii inahusu jinsi ya kuanzisha miradi inayojitegemea na kupunguza utegemezi wa nje.

Kubadilisha wivu kuwa chachu ya maendeleo: Badala ya kutumia nguvu kwenye lawama, jumuiya ya Kiislamu inaweza kutumia wivu wa maendeleo kuchochea mabadiliko chanya ndani ya jamii yao.

Hitimisho

Ni muhimu kwa Waislamu kufanya tathmini ya kina juu ya changamoto zinazowakabili, si kwa lengo la kulaumu wengine, bali kwa nia ya kujifunza na kuimarisha jumuiya zao. Uhusiano wa Kikristo na Kiislamu nchini unaweza kuwa na nguvu zaidi kwa kushirikiana na kuondoa chuki zisizo za msingi. Umoja wa kitaifa ni msingi wa mafanikio ya wote, na kwa kufanya kazi pamoja, Tanzania inaweza kuwa mfano bora wa mshikamano wa kidini duniani.
Hao waislamu gani unaowazungumzia? Mimi swala tano na pia ni msomi pesa kwangu si haba usipende kugenelize we jamaa hivi pambana na ukoo wenu
 
Hiyo ni wewe binafsi , mimi naongelea kwa muktadha ya jumuiya ya kiislamu na Kikristo pana
 
UPENDO
Upendo ndio jambo muhimu sana hapa duniani, binadamu tunapaswa kua na upendo sio tu na muumba wetu bali sisi kwa sisi hapa duniani pasipo kujali tofauti zetu, na MUNGU ndio anapenda na kutarajia hivyo.

Lengo la dini kuwaanda watu kuwa watukufu... Sasa shida iliyopo sio dini bali wanadini wanapoingiza hisia hasi katika dini.

Nilikua kugundua uislamu hauna shida sana shida ilitokana na mitazamo ya walimu wao kuchanganja mafundisho ya kiimani na hisia za kibinadamu Kutokana na hali ya migogoro ya kimahusiano na jamii mbalimbali nyakati hizo hasa ukizingatia serikali ya nchi kutumia misingi ya imani ya dini kuongoza taifa.

Hivyo wakufunzi wa kiimani walifundisha imani huku wakitumia hisia kali za kibinadamu kwa watoto wadogo, hivyo mtoto anakua mkubwa akiwa na trauma (kaathiriwa kisaikolokjia) kwa kawaida jamii itakuona kama ni mtu mwenye imani kali na dhabiti dhidi ya watu wasio wa imani yako, kumbe ni tatizo la kisaikolokjia.(afya ya akili)

Hali hii imewaathili jamii nyingi za kiislamu hasa hasa afrika. Kutokana na wakufunzi kutokua na maadili/misingi/muungozo wa mafunzo kutoka juu... Hivyo madrassa zimefunguliwa popote tu pale.

Sasa changamoto hii haipo kwa waislamu tu hata kwa baadhi ya madhehebu ya kikristo kwa kiasi kidogo kijuona wao ndio bora na sahihi kuliko wengine na kuunza kutengeneza chuki.

UPENDO wa dhati usio wa kusukumwa ndio kitu muhimu kuliko hata dini bali dini ndio zilipaswa kua msitari wa mbele kuhubiri hili.
Umeandika vizuri sana
 
Katika huu uzi siongelei ndugu zangu Waislamu hawa "secular" wa mjini ambao wanaingia msikitini mara tatu kwa mwaka, ndugu zangu hawa ambao tunashinda nao kwenye mabaa, ndugu zangu hawa ambao wanachanganywa na mwanamke anaitwa Rose anasali kwa Mwamposa.
Hii paragraph imenikumbusha aya tukufu ya Qur'aan;

ayat 120 from Surah Al-Baqarah
﴿وَلَن تَرْضَىٰ عَنكَ الْيَهُودُ وَلَا النَّصَارَىٰ حَتَّىٰ تَتَّبِعَ مِلَّتَهُمْ ۗ قُلْ إِنَّ هُدَى اللَّهِ هُوَ الْهُدَىٰ ۗ وَلَئِنِ اتَّبَعْتَ أَهْوَاءَهُم بَعْدَ الَّذِي جَاءَكَ مِنَ الْعِلْمِ ۙ مَا لَكَ مِنَ اللَّهِ مِن وَلِيٍّ وَلَا نَصِيرٍ﴾
[ البقرة: 120]

Mayahudi hawawi radhi nawe, wala Wakristo, mpaka ufuate mila yao. Sema: Hakika uwongofu wa Mwenyezi Mungu ndio uwongofu. Na kama ukifuata matamanio yao baada ya ujuzi ulio kwisha kujia, hutapata mlinzi wala msaidizi kwa Mwenyezi Mungu.
 
  • Nzuri
Reactions: Tui
Katika huu uzi siongelei ndugu zangu Waislamu hawa "secular" wa mjini ambao wanaingia msikitini mara tatu kwa mwaka, ndugu zangu hawa ambao tunashinda nao kwenye mabaa, ndugu zangu hawa ambao wanachanganywa na mwanamke anaitwa Rose anasali kwa Mwamposa.

Uzi huu unalenga Waislamu ambao aidha ni swala tano au Uislamu wao ni wa muhimu kuliko Utanzania wao.

Kila nikiingia kwenye majukwaa ya mijadala kama Jamii Forums, nakutana na hoja zinazochochea makasiriko kutoka kwa baadhi ya Waislamu dhidi ya Wakristo. Hoja hizi mara nyingi huonyesha chuki, lawama, na hata ubaguzi wa wazi. Kwa haraka, ninapochukua muda kutafakari, naona kana kwamba sisi Wakristo hatuna chuki wala ubaguzi wa moja kwa moja dhidi yao. Badala yake, lawama na makasiriko yote huonekana yakitoka upande mmoja. Ni kwa sababu hiyo nimeamua kuandika makala hii, nikiwaomba ndugu zangu Waislamu wafanye tathmini ya kina kuhusu mambo haya kwa nia ya kujenga mshikamano bora.

1. Ajira katika Taasisi za Kidini

Katika jamii yetu, taasisi za Kikristo zinaongoza kwa kuwa na uwazi wa ajira kwa watu wa imani tofauti. Waislamu wengi wameajiriwa kwenye hospitali za Kikristo, shule, na hata benki zinazomilikiwa na makanisa, lakini ni mara nadra sana, au labda haipo kabisa, kuona Mkristo akiajiriwa kwenye taasisi za Kiislamu.

Ubaguzi wa ajira: Taasisi za Kiislamu zinaonekana kushindwa kuwahusisha Wakristo hata kwa kazi za chini kama ulinzi. Hali hii inaleta picha ya ubaguzi na ukosefu wa kujiamini kwa taasisi hizo.

Athari kwa jamii: Kama Wakristo wangekuwa na mtazamo sawa, ndugu zetu Waislamu wengi wangepoteza chanzo cha mapato, jambo ambalo lingeharibu ustawi wa familia zao.

2. Mfumo wa Elimu: Ushirikiano na Changamoto​

Shule nyingi za Kikristo nchini zimekuwa mfano wa ukarimu kwa kupokea watoto wa Kiislamu na kuwaheshimu kwa kuhakikisha mahitaji yao ya kidini yanazingatiwa. Kwa upande mwingine, taasisi za elimu za Kiislamu mara nyingi hazikubali wanafunzi wa Kikristo, na hata pale inapowezekana, hazina mipango ya kuwasaidia kufanikisha mahitaji yao ya kidini.

Ubora wa elimu: Shule nyingi za Kiislamu zimekuwa zikishika nafasi za mwisho kwenye takwimu za kitaifa. Ukosefu wa uwekezaji wa kutosha na mtazamo finyu wa elimu unaweza kuchangia hali hii.

Hitaji la kujifunza kutoka kwa wenzao: Taasisi za Kikristo zimeonyesha mafanikio makubwa, si kwa sababu ya chuki au ubaguzi, bali kwa kuwa na mfumo wa wazi unaowajumuisha wote bila kujali tofauti za kidini.

3. Utegemezi wa Misaada

Taasisi nyingi za Kiislamu zinaonekana kutegemea misaada kutoka nchi za Kiarabu kwa kila jambo. Hii ni changamoto kubwa kwa maendeleo ya ndani ya jamii ya Kiislamu nchini.

Kulegalega kwa juhudi za ndani: Kutegemea misaada ya nje kunalemaza uwezo wa jamii ya Kiislamu kujitegemea na kujenga taasisi imara.

Ukosefu wa mshikamano wa kitaifa: Badala ya kushirikiana na jumuiya zingine nchini, utegemezi wa misaada ya nje huongeza mgawanyiko wa kijamii na kiuchumi.

4. Kuimarisha Umoja kwa Kujifunza

Badala ya kushindana kwa chuki, jamii ya Kiislamu inaweza kujifunza kutoka kwa Wakristo juu ya kujitegemea na kushirikiana kwa manufaa ya wote. Ushirikiano wa kidini unaweza kufanikisha maendeleo ya kijamii na kupunguza chuki zisizo na msingi.

Kujifunza kutokana na mafanikio ya wenzao: Mifano ya mafanikio ya Kikristo inaweza kuwa darasa bora kwa Waislamu. Hii inahusu jinsi ya kuanzisha miradi inayojitegemea na kupunguza utegemezi wa nje.

Kubadilisha wivu kuwa chachu ya maendeleo: Badala ya kutumia nguvu kwenye lawama, jumuiya ya Kiislamu inaweza kutumia wivu wa maendeleo kuchochea mabadiliko chanya ndani ya jamii yao.

Hitimisho

Ni muhimu kwa Waislamu kufanya tathmini ya kina juu ya changamoto zinazowakabili, si kwa lengo la kulaumu wengine, bali kwa nia ya kujifunza na kuimarisha jumuiya zao. Uhusiano wa Kikristo na Kiislamu nchini unaweza kuwa na nguvu zaidi kwa kushirikiana na kuondoa chuki zisizo za msingi. Umoja wa kitaifa ni msingi wa mafanikio ya wote, na kwa kufanya kazi pamoja, Tanzania inaweza kuwa mfano bora wa mshikamano wa kidini duniani.
Labda tukuulize mtoa mada... Waislamu wakiwa duni katika maendeleo wee inakuathiri wapi!?.

Kama ilikuwa ni kutoa mada kwa lengo la kujenga ungeshikilia hapo hapo badala ya kukashifu.

Umoja wa kitaifa haujengwi kwa kashfa ulizotoa.
 
Ukiona mtu ni mtu wa kulalamika lalamika sana ujue kichwani ni empty set....

An uwezi kuta mtu kichwani yupo smart alafu analalamika lalamika hovyo..

Pia udini sometimes ni umavi mavi tuu..
Mi kuna mwanangu tupo form four alikua analeta habari sijui mara huko necta wanafrlisha waislam mara sijui kazini mpaka hv mara vile...

Nikaona kabisa huyu jamaa ana akili za kujibu mtihani tuu ila ukitoa hizo akili anabaki na nyaa au mavi...
Wee mtu badala upambane et anawaza kupendelewa ndo nini sasa
 
Labda tukuulize mtoa mada... Waislamu wakiwa duni katika maendeleo wee inakuathiri wapi!?.

Kama ilikuwa ni kutoa mada kwa lengo la kujenga ungeshikilia hapo hapo badala ya kukashifu.

Umoja wa kitaifa haujengwi kwa kashfa ulizotoa.

Sijatoa kashfa, nimetoa observation kwa kile ambacho nimekiona na kwa bahati mbaya baadhi ya watu katika uzi huu wametafsiri kile nilichokiona kama kashfa

Upendo haujengwi kwa kufumbia macho mambo ambayo mtu anaona yanachochea umaskini (ni adui yako pekee ndio utamuombea na kuridhika ukiona anaoga umaskini)

Ningekua nakashifu nisingetoa mapendekezo nini kifanyike
 
Sijaona mapendekezo Yako yoyote hpo zaidi ya kuona waislamu Hawana maendeleo kwasababu ya kulalamika.
Kwakua ni mtizamo wako ndo umefikia hpo , ngoja nami niishie hapa.
 
Sijaongelea kuhusu kuboresha taasisi kweli? Hujaona hilo?
 
Yaani kwanini uweke kashfa Kisha ndipo uweke mapendekezo!? , Japo hata hayo mapendekezo ya umoja wa kitaifa ulioulenga sijayaona.

Kama wakristo ndo wenye elimu nzuri, hawaombi ombi basi wao wajenge huo umoja wa kitaifa peke Yao, Kuna ulazima gani kujumuisha wengine.

Ukiweka mada sio vyema kuweka ulinganishi ( comparison).
 
Unatakiwa ujue haya yafuatayo.
1) Uislamu ndio dini inayoongoza kupigwa Vita Duniani na Jamii tofauti tofauti.

Hata wanaodai hawana Dini Chuki yao Juu ya Uislamu sio Sawa na Chuki yao Kwa Dini Nyengine.

Watu wa Dini zengine (wenye mafundisho tofauti) linapofika suala la Uislamu wapo tayari kuungana kuupiga Vita Mf Kinachoendelea pale Gaza Wanaofanya mauaji ya waislamu wa Gaza ni Wayahudi lakini utaona hadi wakristo nao wakiunga mkono kana kwana Uyahudi na Ukristo ni imani sawa.

KWAIYO SIO KWELI KUWA WAISLAMU NDIO WANA CHUKI ZAIDI JUU YA WATU WA IMANI NYENGINE.

2)Suala la waislamu kuwa na Taasisi Duni zilizokosa Ushindani. Ni jambo lipo kweli.

Na sababu ni Waislamu wengi hata viongozi wa juu wa hizo taasisi hawana Elimu rasmi ya Dini ya uislamu (wana uislamu wa mazoea). pia hawana Exposure na Elimu za Kimazingira.

Upande wa pili mfano RC wao padri lazima awe kichwa darasani alifauru vizuri A-level akapelekwa Italy kusoma Dini yao miaka 7 pia atasoma PhD ya Philosophy akija kukabidhiwa taasisi lazima itanyooka.

Sasa kwa sisi waislamu ni tofauti Mtu hajui misingi ya dini wala hana Hata Bachelor yoyote anapewa asimamie taasisi kubwa ya Dini lazima atavulunda.

KATIKA HILI WAISLAMU WANEHIMIZWA SANA SUALA LA KUSOMA NA DINI YA UISLAMU NI KUSOMA NA KUJUA MAMBO.

WACHUKULIWE VIJANA MAKINI DARASANI WAPELEKWE NJEE KAMA SAUDIA AU MISRI WAKAPEWE ELIMU YA DINI KWA MIAKA YA KUTOSHA KISHA WAPELEKWE UNIVERSITY WAKACHUKUE DEGREE ZA MAANA.

KISHA WACHUJWE WALE WATAKAOPITA WAPEWE TAASISI ZA DINI.

NAAMINI MAMBO YATABADILIKA.
Hauazungumzia ubaguz wa kua wanaajiri waisilamu tuu?
 
Mkichafuana huko kwenye màtaifa ya kiislam kwanini mnakimbilia kwa hao wanaowachukia? Wakimbizi wa Syria ulishawahi kusikia wanakimbilia Afghanistan? Uarabuni?
Tafakari.
 
Back
Top Bottom