View attachment 2748393
"Niseme Tu kwamba uchaguzi wowote si uchaguzi mwepesi lakini Sisi kama wanasiasa mara nyingi tunafanya tathimini zako unaangalia endapo utagombea mapokeo ya wananchi yatakuwaje?
Mwaka 2020 uchaguzi ulikuwa mgumu (ulikuwa na ugumu wake) ikiwemo mazingira ambayo yalitokea matokeo ya uchaguzi Mkuu lakini pia na aina ya wagombea ambao tulikuwa tunakwenda kushindana nao. Kama utakumbuka 2020 nilikuwa Naibu Waziri wa Afya lakini nilitenguliwa mwezi Mmoja kabla ya Bunge kuvunjwa na Miezi miwili kabla ya kuelekea uchaguzi Mkuu. Ilileta changamoto kidogo.
Lakini pia nilikuwa nashindana na aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda nayo pia ilikuwa na changamoto zake kwa sababu wakati tulipokuwa tunaelekea kwenye michakato ile alikuwa akivaa kofia zote mbili za ukuu wa Mkoa na Mgombea nafasi ya ubunge. Ilileta changamoto.
Sambamba na hilo siku Mbili kabla ya uchaguzi nilimpotezea Mzee wangu (Baba Yangu). Nilipitia mapito magumu. Nawashukuru Sana wananchi wa Kigamboni Imani yao ilikuwa kubwa Sana kwangu" Dkt Faustine Ndugulile
@Faustine_ndugulile, Mbunge wa Jimbo la Kigamboni.
Pole sana Ndungulile, watapata taabu sana.
Wanabodi, kwenye bandiko hili
Ndugu, Jamaa na Marafiki, Njooni Tumtetee Makonda Dhidi ya Mapapa Wauza Unga Wanaomzushia... nilishauri
Wanabodi,
Hili ni bandiko la kuhamasisha a mass mobilization ya kupata kundi kubwa la watu, kuunga mkono kwa dhati, juhudi kubwa zinazofanywa na Mkuu Mhe. Paul Christian Makonda, katika vita mbalimbali,
Hivyo hili ni bandiko la wito kwa kuwaomba ndugu, jamaa na marafiki wa dhati, wanaomjua Makonda kwa karibu na kwa ukweli, njooni tujitokeze kwa wingi, kumtetea Makonda tunayemfahamu dhidi ya uongo na uzushi unaozushwa na kusambazwa na mapapa wauza unga
Ndugu, Jamaa na Marafiki, Tujitokeze Kwa Wingi Kumtetea Makonda
Paskali.
Hata baada ya kuteuliwa kuwa Mwenezi wa CCM, Paul Makonda bado anapigwa vita na wasiomtakia mema, wasioitakia mema CCM na wasio itakia mema Tanzania.
Japo Tanzania ni nchi ya vyama vingi, na kwa mujibu wa katiba ya Tanzania, mamlaka kuu ya nchi ni wananchi, kupitia katiba, serikali ya CCM ilifanya mabadiliko ya katiba kinyume cha katiba na kupoka ukuu wa mamlaka kuu ya wananchi, na kuikakabidhi kwa chama cha siasa, ambapo sasa mamlaka Kuu ya nchi ni chama tawala, CCM ndio imeshika hatamu kuongoza serikali, hivyo katika ukuu wa chama, CCM ndio kila kitu, hivyo Makonda kama msemaji wa CCM, kikao cha CCM kinaweza kumwagiza Rais wa JMT atekeleze jambo lolote lililoelekezwa kwenye ilani ya CCM, Katibu Mwenezi ndie msimamizi wa ilani ya CCM, ana mamlaka yote ya kumuamrisha hadi Rais wa JMT, atekeleze ilani ya uchaguzi ya CCM, hivyo Makonda yuko very right kumuamrisha Waziri Mkuu na kumpa ultimatum ya miezi 6 kumaliza migogoro yote ya ardhi ya nchi hii.
Na baada ya miezi 6, kama Waziri Mkuu, Majaliwa Kasim Majaliwa atashindwa kuitatua migogoro yote ya ardhi, atakuwa ni ameshindwa kazi, Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi, itakutana na kumuagiza Rais wa JMT, kumuondoa Waziri Mkuu, kwa kushindwa kazi na kumteua Waziri Mkuu mwingine mwenye uwezo.
Hata ikitokea Rais Samia ameshindwa kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM, chama kinaweza kumfuta uanachama na hivyo kupoteza urais!, hivyo Mwenezi wa CCM ni mtu mkubwa sana, kuliko serikali yote ya Tanzania, na hii ndio maana halisi ya Party Supremacy, CCM ndio imeshika hatamu za kuiongoza serikali ya Tanzania .
Hongera sana Mwenezi mpya wa CCM, Paul Makonda, kuiheshimisha CCM, endelea kutoa maagizo na ultimatum kwa viongozi wote kuhusiana na utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM, wewe ndiye msimamizi wa ilani ya CCM!.
Angalia ilani ya CCM imeelekeza nini kuhusu Bunge la JMT, toa maelekezo kwa Spika with ultimatums, Spika akishindwa kutekeleza Spika anaondolewa!, enzi za Spika Sitta, aliponea chupu chupu kuondolewa, kuna mtu mmoja very powerful ndani ya CCM aitwae "The King Maker" ndie alimuokoa Spika Sitta kwa kumpa maelekezo Mwenyekiti wa CCM, JK, na hii ndio salama yake!.
Makonda angalia ilani ya uchaguzi ya CCM inasema nini kuhusu mhimili wa Mahakama, toa maagizo with ultimatum kwa Jaji Mkuu atekeleze.
Angalia ilani ya uchaguzi inasema nini kuhusu majeshi, ulinzi na usalama, toa maelekezo with ultimatum kwa Amiri jeshi Mkuu na kwa Mkuu wa majeshi, IGP , etc.
Ila kwa nafasi ambazo sio za kichama kama Jaji Mkuu, Mkuu wa Majeshi, CAG, Mwenyekiti wa NEC, Msajili wa Vyama vya Siasa, Wakuu wa vyombo vya Ulinzi, Mwenyekiti wa Tume ya Utawala Bora na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma ambao ni wateule wa rais, Paul Makonda anaweza kuwapa maelekezo bila ultimatums kwasababu hawa chama hakiwezi kuwafanya chochote, na badala yake, chama kitampa maelekezo mamlaka yake ya uteuzi ambaye ni Rais wa JMT, awaondoe!.
Kiukweli ninamkubali sana Paul Makonda!, Tangu nilipoanza kumkubali
Nimemkubali Sana DC Makonda, anafaa kuwa Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam
He has never let me down!. Tena niliwahi kushauri
Baada ya Magufuli, 2025 Makonda atatufaa sana, kwasababu ana uthubutu kuliko hata JPM!. Apunguze... ushauri huu still stands, kwasababu miaka hii 4 ya Mama ni kumalizia awamu ya Magufuli, awamu ya baada ya Magufuli inaanza 2025, ila
Voices From Within: Japo 2025 Tumepanga Twende na Mwanamke, 2025 Mama Akabidhi Kwanza Mwanamume, Kisha 2030 Ndipo Aje Mwanamke hivyo you never know with politics, everything is possible!.
Paul Makonda kanyaga mwendo, chapa kazi, kazi iendelee!.
Paskali.