Ndumba za hii timu ni hatari mno

Ingekuwa vizuri ukatutajia hiyo timu ili tuje na mifano kabisa, badala ya kuleta mafumbo hapa. Mimi wachezaji ninaowafahamu walioondoka Tanzania wakachemka huko walikoenda ni hawa wafuatao:
1. Makambo - Toka Yanga
2. Chama - Toka Simba
3. Miquison - Toka Simba
Haya tuendelee sasa kuwataja wengine walioathirika na ndumba za timu zao baada ya kuondoka.
 
Nadhani wanajielewa tu na utawaona hapa wanakuja wamepanic
 
Unazungumzia Simba ambao walikuwa na hawa baadhi ya watu

Kocha Sven, kocha Gomez, kocha Ausems waliifanya Simba ifike robo fainali michuano ya CAF na walipotoa Simba tu hawakuvuma tena.

Chama na Miquison walipoondoka Simba walipoenda timu mpya wameshindwa kutamba huko
 
Sisi ndio tunashangaa.Kocha anapewa sofa za ubobevu,je huu ubobevu unayeyukia wapi akihama timu?Kama si ndumba ni nini?
Huyo kocha mbobevu hakupatia mafanikio yake Yanga tu, mkoba wake una kombe la shirikisho alilochukua akiwa na As Leopard ya Congo, timu aliyoikuta ikiwa haina mafanikio yoyote ya mashindano ya Afrika...
Kushindwa kwake kwenda makundi hakumaanishi kwamba uwezo umeisha kutokana na hiyo imani yako potofu, hata alipokuja Yanga msimu wa kwanza alitolewa na Rivers, msimu wa pili akatolewa na Al Hilal na kuangukia shirikisho alikofika fainali...
Kumbuka Karma inafanya kazi, watu wakikupenda sana kisha ukavimba kichwa na kuwaacha kwa ubaya lazima yakukute, mfano mzuri ni Eden Hazard
 
Usisahau Uchebe na Da Rosa
 
Sasa hapo ndio ujue Simba ni timu nzuri yenye mifumo na mazingira mizuri ambayo wachezaji na makocha wanafanikiwa kirahisi, wakivimba kichwa na kujiona ni wakubwa kuliko timu inakula kwao

Hao makocha nawafananisha na mwalimu ambaye alikuwa anafaulisha vizuri wanafunzi akavimba kichwa akadhani ni uwezo wake binafsi tu bila kujua pia mazingira mazuri ya shule na wanafunzi bora wanaosajiliwa na shule vinachangia, akahama na kwenda shule za vichochoroni na kujuta

Hata wachezaji wanapaswa kutambua kuwa mwanafunzi kufanya vizuri mazingira ya shule yanachangia sana
 
Maisha ya mayele yanaendeleaje huko pyramids?
 
Ulisikia kuna profesa hapo?
 
Mane anakula bata uarabuni tena anaporomosha majumba ya kifahari kwako maybe hao wengine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…