Ndumba za hii timu ni hatari mno

Ndumba za hii timu ni hatari mno

Cashman

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2018
Posts
3,017
Reaction score
5,294
Ni nadra sana ukifanya vizuri kwenye hii timu kisha ukaondoka bado wanakuhitaji ukatoboa unakokwenda.Ndio maana wana jeuri ya kukutunia muda wowote unapodai haki yako.

Upo uwezekano kuwa huenda kuna nguvu ya ndumba huwa nyuma ya uchezaji bora wa wachezaji wao na makocha wao.

Angalia makocha wao waliofanya vizuri wanapoenda timu nyingine.Wengine walipachikwa majina ya ubobevu eti tu kwa kudhaniwa wana uwezo mkubwa sana,lakini huko waliko sasa,huo ubobevu umeyeyuka.

Wengine walipata ufungaji bora Afrika lakini sasa huko waliko wanasikitisha.

Kwa nyie mliopo sasa kwenye hii timu,msianze kuzingua maana huo ndio utakuwa mwisho wenu.Hamuwezi kwenda popote hadi viwango vyenu vishuke.Ondoeni ndoto za kwenda ulaya
 
Hakuna mchezaji mkubwa kuliko timu. Mimi sio shabiki wa hio timu na wala sipo hapa kutoa utetezi ila kuna mifano mikubwa tunaiona hata huko ulaya mchezaji akiondoka kwa kufosi huku timu ikiwa inahitaji huduma yake safari yake ya soka hua inakua ngumu.
Cheki mane coutinho eden hazard hao ni wachache
 
Hakuna mchezaji mkubwa kuliko timu. Mimi sio shabiki wa hio timu na wala sipo hapa kutoa utetezi ila kuna mifano mikubwa tunaiona hata huko ulaya mchezaji akiondoka kwa kufosi safari yake ya soka hua inakua ngumu.
Cheki mane coutinho eden hazard hao ni wachache
Hata makocha?
Sasa unataka mchezaji acheze kwa mapenzi wakati anatafuta kipato?
 
Kuwa bora kwenye timu fulani sio kigezo cha kuendelea kubaki kuwa bora hata ukibaki.
Ligi zimetofautiana mengi sana hasa uwezo wa wachezaji. Sijui n timu gani unaizungumzia hapa kwa kificho weka mambo hadharani mpira ni mchezo wa wazi
 
Ni nadra sana ukifanya vizuri kwenye hii timu kisha ukaondoka bado wanakuhitaji ukatoboa unakokwenda.Ndio maana wana jeuri ya kukutunia muda wowote unapodai haki yako.

Upo uwezekano kuwa huenda kuna nguvu ya ndumba huwa nyuma ya uchezaji bora wa wachezaji wao na makocha wao.

Angalia makocha wao waliofanya vizuri wanapoenda timu nyingine.Wengine walipachikwa majina ya ubobevu eti tu kwa kudhaniwa wana uwezo mkubwa sana,lakini huko waliko sasa,huo ubobevu umeyeyuka.

Wengine walipata ufungaji bora Afrika lakini sasa huko waliko wanasikitisha.

Kwa nyie mliopo sasa kwenye hii timu,msianze kuzingua maana huo ndio utakuwa mwisho wenu.Hamuwezi kwenda popote hadi viwango vyenu vishuke.Ondoeni ndoto za kwenda ulaya
Na nyie logeni kwenu
 
Okwi alienda huko akarudi Simba na bado alikuwa wa moto ,hivo hivo Morison naye alitoka huko akaja simba akiwa wa moto.

Hakuna dumba hapo,mchezaji anapoondoka anakutana na changamoto kipya either ang'ae zaidi au mfumo wa timu umkatae,vila vile hata kwa makocha,unakuta anaachiwa mikoba anaizoea timu hadi inafika mbali akiondoka siyo rahisi kuanzisha alipoishia kwenye timu mpya
 
Hata Luis alifanya vizuri alipoenda ndio maana leo yupo pale anapunguza kilo zake.
Hata yule mwingine yupo ligi daraja la pili ufaransa ajafanikiwa kucheza hata mechi moja na alichukua tuzo za mfungaji wa goli bora la cafcc.
Yupo mwingine alishindwa pale uarabuni wakisema ana kasi ya Kobe ila uku kwetu ndio mfalme zwazwaa..
 
Back
Top Bottom