seedfarm
JF-Expert Member
- Feb 9, 2020
- 260
- 2,655
Members, Tundu Lissu makusudi ameitega tume ya uchaguzi nayo imetegeka na kujiweka mahali penye maswali magumu na utata.
Kitendo cha tume kuyatupilia mbali mapingamizi ya Tundu Lissu juu ya wagombea urais wa CCM na CUF ni mtego mzito sana ambao Tundu Lissu alifanya kusudi kuwatega Tume ya uchaguzi.
Lengo la Tundu Lissu amefanikiwa kwa asilimia 100 kwani ameshapata msingi wa kuwaambia wananchi Tume ina ndimi mbili na hawazingatii sheria ya uchaguzi pale itakapotokea wagombea walioenguliwa hawajarudishwa na Tume ya uchaguzi.
Hoja za Tundu Lissu alizozitoa ni hoja za kisheria ambazo Tume ya uchaguzi wamejibu kwa kutofuata sheria bali kwa utashi binafsi,
Kitendo cha Tume ya uchaguzi kujibu hoja za mapingamizi mazito kisheria sasa rasmi wanaleta utata mitaani wa kisheria.
Kuokoa jahazi hapa na kujiondoa kwenye mtego huu na vurugu Tume lazima iwarudishe wagombea wote wa ubunge na udiwani walioengulia kijanja kijanja kwa utashi binafsi.
Hakika hoja za Tundu lisu za kisheria ambazo ni sheria za Tume ya Uchaguzi kuhusu mapingamizi zimeizamisha Tume ya uchaguzi yenyewe kwani Tume hawajaainisha vipengele vya sheria ya uchaguzi katika majibu yao ili kupinga hoja za Lissu.
Kuondoa sintofahamu hii sasa Tume ya uchaguzi Tundu lisu amewatega na nyinyi mmetegeka na kuingia mazima.
Ili mueleweke kwa wananchi na kuondoa utata mliofanya kwa mtego wa Tundu Lissu inawalazimu kuwarudisha wagombea wote wa udiwani na ubunge walioenguliwa na wakurugenzi.
Hoja za kisheria hupingwa kwa hoja za kisheria na vifungu vya kisheria.
Sheria tulizotunga wenyewe sasa zinageuka na kuwa msumari wa moto kwa Tume yenyewe ya uchaguzi.
Je sheria hizi zilitungwa ili kumtega nani? Tundu Lissu ametoa hoja kwa kufuata sheria za uchaguzi lakini Tume imetoa hoja kupinga mapingamizi kwa kuikwepa sheria yenyewe.