Mkuu nadhani humjui vizuri Tundu Lissu.Kama unavichukulia vitu juu juu na kwa jinsi anavyopangilia maneno yake, unaweza ukaamini kile anachokiongea ni sahihi. Lissu ni Mwanasheria mbobezi anajua jinsi ya kucheza na maneno na vifungu vya sheria kama ilivyo mahakamani ili kuweza kamshawishi hakimu akubaliane na hoja zake. Mbinu hiyo hiyo ndo anaitumia pia kuwashawishi watu huku nje wasiopenda kutafakari ili waamini anachoongea.
Nimesikiliza hoja za Lissu vizuri sana, kwanza anasema JPM hawakuwasilisha fomu za uteuzi siku iliyotakiwa kisheria. Lakini sote tulimuona JPM siku ile ya tarehe 25 ambayo ni ya uteuzi akiwa na fomu zake, sasa jiulize alienda kufanya nini pale Tume.
Lakini Hoja yake hii anaijenga pia kwenye uhakiki wa wadhamini, kwamba kwann wasimamizi wa uchaguzi ndo wahakiki wadhamini (membe pia wadhamini wake wamehakikiwa na hao wasimamizi wa Jimbo lakini cha ajabu hakumwekea pingamizi). Anarudi tena kusema kwamba tume ndo iliyotoa maelekezo kwa hao wasimamizi kuhakiki wadhamini katika kila jimbo lakini hapo hapo anasema maelekezo hayo yanapingana na sheria. Lakini hafafanui kwamba sheria hiyo ndo inairuhusu Tume kukasimu madaraka yake kwa kadri itakavyoona inafaa kwa wasimamizi wa uchaguzi bila kusema ni madaraka gani. Kwahiyo mpaka hapo utaona tume haikuvunja sheria. Lakini hata kama tume ingekua imevunja sheria kwa kuwapa mamlaka wasimamizi wa uchaguzi, unawezaje kumlaumu/kumuwekea pingamizi mgombea ambae alifuata maelekezo ya Tume.
Infact, Tundu Lissu aliweka mapingamizi siyo kwa maana ya mtego bali kwa kujihami kwasbb toka mwanzo alihisi atakatwa na Tume (Tweet ya mbowe siku moja kabla ya uchaguzi inathibitisha hili) . Baada ya kuona tume haikufanya hivyo, akajua CCM au chama kingine kinaweza kutumiwa kumuwekea pingamizi baada ya uteuzi. Kwsbb anajua zilikuepo sababu nyingi sana za kumuengua isipokua watu waliamua iwe fair play wamuache agombee na ili uchaguzi uende kwa amani.