Uchaguzi 2020 NEC imecheza ngoma ya Tundu Lissu. Je, Wagombea walioenguliwa Ubunge Tume itawarudisha?

Uchaguzi 2020 NEC imecheza ngoma ya Tundu Lissu. Je, Wagombea walioenguliwa Ubunge Tume itawarudisha?

Tundu Lissu anatumia uwezo wake kinyume na matarajio ya wanasheria wengi; Katiba yetu ibara ya 74 inawataja Wakurugenzi wa Halmashauri kama sehemu ya TUME, n ndio maana wanawatangaza wabunge ba unapotakiwa wakusainie fomu za wadhamini,maana yake hao wapiga kura wapo kwenye maeneno yao'
Sheria ya Uchaguzi kifungu cha 35 na 37 kinawataja hao wakurugenzi wa TUME; yeye ashukuru Mungu kuwa NEC ilimstahi kuhakiki fomu zake, alipaswa kuenguliwa katika Ugombea wa Urais;
Sasa issue ya kuweka Picha nayo haina miguu ya kisheria maana sote tumeiona fomu ya Mgombea wa CCM na picha zake zote ni passport size;
Nafikiria Tundu Lissu atafute maeneo mengine ya kutoa elimu yake ya Kisheria na lazima aonekane kama mtu anayetaka kuwa STATEMAN hata kwa maneno na matendo yake; Usoni anaonekana kama mtu ambaye ana shari shari au uanaharakati uliopitiliza tu
 
Lisu ni muongo na mzushi
Mashabiki wake mnaplekwa kama wajingaView attachment 1549327View attachment 1549328
Trust me ndugu mahaba kwa mtu yanaweza kukufanya ukawa fala mkubwa sana....
Hawa wenzetu sahv akili zao hazifikiri kabisa nikama wameunganishwa kwenye ubongo wa lisu bongo zao hawazitumii kabisa
Swala ni kwamba form za jp zilikuwa na picha na tumeona form hizo
Pili fikii tu kwa akili ya ubinadamu verification ya wadhamini ingefanyika siku ya kurudisha form ile shughuli ingeisha ndo maana tume inawapa wakurugenz mikoani kufanya hilo jambo na sikwamba magu aliamua kama yy bali ni maelekezo ya tume kwa hyo yy angeihoji tume kwamba imekosea yenyewe si magu maana alikuwa anatekeleza maelekezo aliyopewa na tume
Wagombea wengine wote pia wadhamini walihakikiwa na wakurugenz mikoani kasoro yy na ndiyo sababu ya yy form yake kuchelewa kupokelewa...
Huyu jamaa anahulka ya kujiona he nows everything ndugu kuna vijana down here wanaijua sheria zaid ya anavyofikiria ila wako kimya maana hawajapata hiyo nafasi ya kuonekana na kujisifia na kusifiwa kizwazwa
 
Members, Tundu Lissu makusudi ameitega tume ya uchaguzi nayo imetegeka na kujiweka mahali penye maswali magumu na utata.

Kitendo cha tume kuyatupilia mbali mapingamizi ya Tundu Lissu juu ya wagombea urais wa CCM na CUF ni mtego mzito sana ambao Tundu Lissu alifanya kusudi kuwatega Tume ya uchaguzi.

Lengo la Tundu Lissu amefanikiwa kwa asilimia 100 kwani ameshapata msingi wa kuwaambia wananchi Tume ina ndimi mbili na hawazingatii sheria ya uchaguzi pale itakapotokea wagombea walioenguliwa hawajarudishwa na Tume ya uchaguzi.

Hoja za Tundu Lissu alizozitoa ni hoja za kisheria ambazo Tume ya uchaguzi wamejibu kwa kutofuata sheria bali kwa utashi binafsi,

Kitendo cha Tume ya uchaguzi kujibu hoja za mapingamizi mazito kisheria sasa rasmi wanaleta utata mitaani wa kisheria.

Kuokoa jahazi hapa na kujiondoa kwenye mtego huu na vurugu Tume lazima iwarudishe wagombea wote wa ubunge na udiwani walioengulia kijanja kijanja kwa utashi binafsi.

Hakika hoja za Tundu lisu za kisheria ambazo ni sheria za Tume ya Uchaguzi kuhusu mapingamizi zimeizamisha Tume ya uchaguzi yenyewe kwani Tume hawajaainisha vipengele vya sheria ya uchaguzi katika majibu yao ili kupinga hoja za Lissu.

Kuondoa sintofahamu hii sasa Tume ya uchaguzi Tundu lisu amewatega na nyinyi mmetegeka na kuingia mazima.

Ili mueleweke kwa wananchi na kuondoa utata mliofanya kwa mtego wa Tundu Lissu inawalazimu kuwarudisha wagombea wote wa udiwani na ubunge walioenguliwa na wakurugenzi.

Hoja za kisheria hupingwa kwa hoja za kisheria na vifungu vya kisheria.

Sheria tulizotunga wenyewe sasa zinageuka na kuwa msumari wa moto kwa Tume yenyewe ya uchaguzi.

Je sheria hizi zilitungwa ili kumtega nani? Tundu Lissu ametoa hoja kwa kufuata sheria za uchaguzi lakini Tume imetoa hoja kupinga mapingamizi kwa kuikwepa sheria yenyewe.
....hata picha halioni
 
Mmm kumbe ndo maana JK alisema bora agombee Slaaa kuliko Tundu! Wakati ule
 
Hawa wakupita bila kupingwa wanamatatizo sana wanatuwekea picha za mtu anakula mahindi kwenye form za kugombea uraisi wanata tusifie duh
Hata Kassim Majaliwa na Babu Tale wamepita bila kupingwa
 
Haya ndio mambo Socrates alikuwa apendi kwenye democracy ya kila mtu kuamua. Akatolea mfano wa tukio la mahakamani kuna siku raia waliochaguliwa kuamua kesi, baada kusikiliza ushahidi wa pande zote jamaa wakaamua mtuhumiwa apewe adhabu kifo. Kesho yake asubuhi watu wale wale wakakimbilia kwa hakimu wakidai walikosea maamuzi jamaa aachiwe.

Tatizo kwake hapo sio adhabu ya kifo au kuachiwa huru zilitolewa kwa mtuhumiwa isipokuwa namna maamuzi ya raia wa kawaida yanavyofikiwa. Hakuna reasonable arguments kwanini mtu auwawe au aachwe kutokana na ushahidi wa kesi husika, isipokuwa watu wachache wenye makelele wanaweza shawishi wengine namna ya kuamua. Democracy ya mtindo huo aifai.

Ndio CDM na Lissu yaani jamaa anaweza ongea upuuzi ambao auna maana kabisa kama MIGA au pingamizi lake la jana ni la ovyo kweli kisheria lakini CDM watashabikia huo upuuzi mpaka duh.

Rudi shule ukajifunze matumizi ya herufi h maana naona unatia aibu tu.
 
Nilishasema watendaji wa serikali ndio wanaosababisha matatizo kwa wananchi bali sio chama cha mapinduzi

Kwa style hii,Tume ilibidi watulie kwanza kabla ya kumjibu mtu huyo,Sasa wanaleta utata mpya kabisa kwenye uchaguzi huu

Sio kila jambo inabidi kulijibu,kuna mambo unachutama kwanza

Hawa watendaji wanakiharibia chama cha mapinduzi sana kwani wao hawako mstari wa mbele kwenye kutafuta kura

Kanuni za uchaguzi haziruhusiwi kwenda kinyume na Sheria mama ya uchaguzi haya si wanayajua Tume ya uchaguzi

Kitendo cha kumuweka Tundu lisu siku ile masaa zaidi ya saba nilitegemea haya yatajitokeza tu

Hivi Tume mngepokea fomu za jamaa haraka na kumuacha aondoke si mngekiweka chama chetu salama

Nina hakika huyu mtu hakuwaza kuja na mapingamizi bali kitendo cha kumuweka pale masaa kibao ndio madhara yake hayo

Mengi tunashauri hapa,Mfano tulishauri akija toka nje aachwe si aliachwa airport na hajatupunguzia kura na heshma kwa wananchi au nje

Mfano angesumbuliwa siku ile airport wangesema ni ccm imefanya na sio watendaji

Kwanini tunaharibu image ya chama?
Kuna mambo yanafanyika sio kwa maslahi ya chama hasa kwa watendaji
Hahaha !! Umenifurahisha tu kumbuka taasisi zote zipo chini ya serikali na serikal ni CCM ivo lazima lawama wapewe CCM maana ndio serikal mtu km polepole eti nae anatumia magal ya serikal kwel CCM ni serikal
 
Nandio maana nimeona tume jana waliwaonya waliojitangaza kupita bila kupingwa
 
Rudi shule ukajifunze matumizi ya herufi h maana naona unatia aibu tu.
Ukishindwa hoja mnaamia kwenye mambo madogo madogo au kuja na lugha zisizo na staha; we unadhani kwanini software zote za kuandikia zina spelling check ilhali watumiaji wake ni watu waliobobea kwenye lugha zao.
 
Yaani umeeleza maelezo marefu ambayo yanajirudia rudia halfu hayana substance yoyote. Kwa mfano, hukuelezea ni vifungu vipi vya sheria ambavyo Lissu amevitumia kuweka mapingamizi halafu havikujibiwa na Tume au imeenda kinyume chake.

Hujaeleza ni vifungu vipi vya sheria ambavyo Tume ilikiuka wakati wa kuwaeungua wagombea wengine ambapo sasa kwa hoja za Lissu itabidi iwarejeshe. Andiko lako lipo kama hadithi isiyo na mwanzo wala mwisho.
Kwa tunaofuatilia suala zima la uchaguzi tumemuelewa. Ameeleza vyema mno. Uko sahihi mtoa mada.
 
Yaani umeeleza maelezo marefu ambayo yanajirudia rudia halfu hayana substance yoyote. Kwa mfano, hukuelezea ni vifungu vipi vya sheria ambavyo Lissu amevitumia kuweka mapingamizi halafu havikujibiwa na Tume au imeenda kinyume chake.

Hujaeleza ni vifungu vipi vya sheria ambavyo Tume ilikiuka wakati wa kuwaeungua wagombea wengine ambapo sasa kwa hoja za Lissu itabidi iwarejeshe. Andiko lako lipo kama hadithi isiyo na mwanzo wala mwisho.

Zero brain. Kilangila.
 
Back
Top Bottom