Uchaguzi 2020 NEC imecheza ngoma ya Tundu Lissu. Je, Wagombea walioenguliwa Ubunge Tume itawarudisha?

Hivi inakuwaje kwa nchi yenye umri wa miaka 60 wagombea wa nafasi ya ubunge na udowani wanapita bila kupitwa?
 
Naam. Pingamizi za Chadema dhidhi ya wagombea urais wa ccm na cuf yana msingi wa kisheria lakini ni mambo madogo madogo yanayozungumzika. Tume iko sahihi kuyaweka kando. Sidhani kama mweka pingamizi aliamini kuwa yatapita. Bila shaka alitaka kuonyesha kuwa sisi ni binadamu tunaokosea na tusihukumiwe kwa makosa mengine ambayo ni madogo sana. Changamoto ni kwamba kule chini wagombea wa upinzani wameenguliwa kwa sababu hizo hizo; au nyepesi kuliko hizo na wakati mwingine kwa dhuluma iliyo wazi na inayoratibiwa na vyombo vya serikali. The ball is in NEC's court.
 
Lisu ni muongo na mzushi
Mashabiki wake mnaplekwa kama wajinga
20200827_083056.jpg
20200827_083113.jpg
 
Naam. Pingamizi za Chadema dhidhi ya wagombea urais wa ccm na cuf yana msingi wa kisheria lakini ni mambo madogo madogo yanayozungumzika. Tume iko sahihi kuyaweka kando. Sidhani kama mweka pingamizi aliamini kuwa yatapita. Bila shaka alitaka kuonyesha kuwa sisi ni binadamu tunaokosea na tusihukumiwe kwa makosa mengine ambayo ni madogo sana. Changamoto ni kwamba kule chini wagombea wa upinzani wameenguliwa kwa sababu hizo hizo; au nyepesi kuliko hizo na wakati mwingine kwa dhuluma iliyo wazi na inayoratibiwa na vyombo vya serikali. The ball is in NEC's court.
Lisu kawageuza mandondocha kabisa nyie
Hizi hapa siyo picha ama ni nini?
20200827_083056.jpg
20200827_083113.jpg
 
Mkuu nadhani humjui vizuri Tundu Lissu.Kama unavichukulia vitu juu juu na kwa jinsi anavyopangilia maneno yake, unaweza ukaamini kile anachokiongea ni sahihi. Lissu ni Mwanasheria mbobezi anajua jinsi ya kucheza na maneno na vifungu vya sheria kama ilivyo mahakamani ili kuweza kamshawishi hakimu akubaliane na hoja zake. Mbinu hiyo hiyo ndo anaitumia pia kuwashawishi watu huku nje wasiopenda kutafakari ili waamini anachoongea.

Nimesikiliza hoja za Lissu vizuri sana, kwanza anasema JPM hawakuwasilisha fomu za uteuzi siku iliyotakiwa kisheria. Lakini sote tulimuona JPM siku ile ya tarehe 25 ambayo ni ya uteuzi akiwa na fomu zake, sasa jiulize alienda kufanya nini pale Tume.

Lakini Hoja yake hii anaijenga pia kwenye uhakiki wa wadhamini, kwamba kwann wasimamizi wa uchaguzi ndo wahakiki wadhamini (membe pia wadhamini wake wamehakikiwa na hao wasimamizi wa Jimbo lakini cha ajabu hakumwekea pingamizi). Anarudi tena kusema kwamba tume ndo iliyotoa maelekezo kwa hao wasimamizi kuhakiki wadhamini katika kila jimbo lakini hapo hapo anasema maelekezo hayo yanapingana na sheria. Lakini hafafanui kwamba sheria hiyo ndo inairuhusu Tume kukasimu madaraka yake kwa kadri itakavyoona inafaa kwa wasimamizi wa uchaguzi bila kusema ni madaraka gani. Kwahiyo mpaka hapo utaona tume haikuvunja sheria. Lakini hata kama tume ingekua imevunja sheria kwa kuwapa mamlaka wasimamizi wa uchaguzi, unawezaje kumlaumu/kumuwekea pingamizi mgombea ambae alifuata maelekezo ya Tume.

Infact, Tundu Lissu aliweka mapingamizi siyo kwa maana ya mtego bali kwa kujihami kwasbb toka mwanzo alihisi atakatwa na Tume (Tweet ya mbowe siku moja kabla ya uchaguzi inathibitisha hili) . Baada ya kuona tume haikufanya hivyo, akajua CCM au chama kingine kinaweza kutumiwa kumuwekea pingamizi baada ya uteuzi. Kwsbb anajua zilikuepo sababu nyingi sana za kumuengua isipokua watu waliamua iwe fair play wamuache agombee na ili uchaguzi uende kwa amani.

Hata tukiutumia mtazamo huu, bado tume imejiweka pabaya. Watanzania hawana muda wa kusoma maelezo na vifungu kama ulivyofafanua. Ni kwa kutumia mwanya huo TL anaonekana bingwa kwasababu alifafanua kifungu kwa kifungu na wananchi wakamwelewa. Ili kujibu hoja hizi na kueleweka kwa umma Tume ilipaswa kutokukurupuka kujibu. Maana hata aliyeweka pingamizi alikuwa anajua fika kuwa pingamizi lake halitakubaliwa, lakini umma utabadirishwa fikra zao na katika hili kafanikiwa. Sasa ili fikra za umma zirudi ktk mstari, na kuifuta kabisa hoja hiyo ufafanuzi kama huo ulioutoa ilipaswa utolewe na tume. Hoja hujibiwa kwa hoja.
 
Hii ni aibu, tuna mgombea Urais anayedhani Tume ya Taifa ya Uchaguzi ni jengo lililopo Dodoma 😂😂
 
Ninachojiuliza hivi ni kwanini kila wakati tunasikia wameenguliwa wangombea wa upinzani tu?? Na au wapita bila kupingwa wagombea wa CCM tuu???
Bro iyo ni kama kwenye soccer, defender akimfanyia foul striker referee anatoa penalty lakini striker akimfanyia foul defender inakua tuu free kick..SASA ktk uchaguzi chama kinachokua madarakani mara nyingi kinakua ktk advantageous position (penalty box) kinashambulia na Wapinzani wanakaba, kosa kidogo tuu penalty inapigwa kwenda upinzani, na mara nyingi mechi inachezwaga nusu uwanja upande wa Wapinzani, so ni Ngumu penalty itokee sehemu mpira hausogei kabisa. Nadhani umenielewa.
 
Members, Tundu Lissu makusudi ameitega tume ya uchaguzi nayo imetegeka na kujiweka mahali penye maswali magumu na utata.

Kitendo cha tume kuyatupilia mbali mapingamizi ya Tundu Lissu juu ya wagombea urais wa CCM na CUF ni mtego mzito sana ambao Tundu Lissu alifanya kusudi kuwatega Tume ya uchaguzi.

Lengo la Tundu Lissu amefanikiwa kwa asilimia 100 kwani ameshapata msingi wa kuwaambia wananchi Tume ina ndimi mbili na hawazingatii sheria ya uchaguzi pale itakapotokea wagombea walioenguliwa hawajarudishwa na Tume ya uchaguzi.

Hoja za Tundu Lissu alizozitoa ni hoja za kisheria ambazo Tume ya uchaguzi wamejibu kwa kutofuata sheria bali kwa utashi binafsi,

Kitendo cha Tume ya uchaguzi kujibu hoja za mapingamizi mazito kisheria sasa rasmi wanaleta utata mitaani wa kisheria.

Kuokoa jahazi hapa na kujiondoa kwenye mtego huu na vurugu Tume lazima iwarudishe wagombea wote wa ubunge na udiwani walioengulia kijanja kijanja kwa utashi binafsi.

Hakika hoja za Tundu lisu za kisheria ambazo ni sheria za Tume ya Uchaguzi kuhusu mapingamizi zimeizamisha Tume ya uchaguzi yenyewe kwani Tume hawajaainisha vipengele vya sheria ya uchaguzi katika majibu yao ili kupinga hoja za Lissu.

Kuondoa sintofahamu hii sasa Tume ya uchaguzi Tundu lisu amewatega na nyinyi mmetegeka na kuingia mazima.

Ili mueleweke kwa wananchi na kuondoa utata mliofanya kwa mtego wa Tundu Lissu inawalazimu kuwarudisha wagombea wote wa udiwani na ubunge walioenguliwa na wakurugenzi.

Hoja za kisheria hupingwa kwa hoja za kisheria na vifungu vya kisheria.

Sheria tulizotunga wenyewe sasa zinageuka na kuwa msumari wa moto kwa Tume yenyewe ya uchaguzi.

Je sheria hizi zilitungwa ili kumtega nani? Tundu Lissu ametoa hoja kwa kufuata sheria za uchaguzi lakini Tume imetoa hoja kupinga mapingamizi kwa kuikwepa sheria yenyewe.
Itakuwa ngoma ya kienyeji ambayo nec kuicheza wameona ni upumbavu
 
Mkuu nadhani humjui vizuri Tundu Lissu.Kama unavichukulia vitu juu juu na kwa jinsi anavyopangilia maneno yake, unaweza ukaamini kile anachokiongea ni sahihi. Lissu ni Mwanasheria mbobezi anajua jinsi ya kucheza na maneno na vifungu vya sheria kama ilivyo mahakamani ili kuweza kamshawishi hakimu akubaliane na hoja zake. Mbinu hiyo hiyo ndo anaitumia pia kuwashawishi watu huku nje wasiopenda kutafakari ili waamini anachoongea.

Nimesikiliza hoja za Lissu vizuri sana, kwanza anasema JPM hawakuwasilisha fomu za uteuzi siku iliyotakiwa kisheria. Lakini sote tulimuona JPM siku ile ya tarehe 25 ambayo ni ya uteuzi akiwa na fomu zake, sasa jiulize alienda kufanya nini pale Tume.

Lakini Hoja yake hii anaijenga pia kwenye uhakiki wa wadhamini, kwamba kwann wasimamizi wa uchaguzi ndo wahakiki wadhamini (membe pia wadhamini wake wamehakikiwa na hao wasimamizi wa Jimbo lakini cha ajabu hakumwekea pingamizi). Anarudi tena kusema kwamba tume ndo iliyotoa maelekezo kwa hao wasimamizi kuhakiki wadhamini katika kila jimbo lakini hapo hapo anasema maelekezo hayo yanapingana na sheria. Lakini hafafanui kwamba sheria hiyo ndo inairuhusu Tume kukasimu madaraka yake kwa kadri itakavyoona inafaa kwa wasimamizi wa uchaguzi bila kusema ni madaraka gani. Kwahiyo mpaka hapo utaona tume haikuvunja sheria. Lakini hata kama tume ingekua imevunja sheria kwa kuwapa mamlaka wasimamizi wa uchaguzi, unawezaje kumlaumu/kumuwekea pingamizi mgombea ambae alifuata maelekezo ya Tume.

Infact, Tundu Lissu aliweka mapingamizi siyo kwa maana ya mtego bali kwa kujihami kwasbb toka mwanzo alihisi atakatwa na Tume (Tweet ya mbowe siku moja kabla ya uchaguzi inathibitisha hili) . Baada ya kuona tume haikufanya hivyo, akajua CCM au chama kingine kinaweza kutumiwa kumuwekea pingamizi baada ya uteuzi. Kwsbb anajua zilikuepo sababu nyingi sana za kumuengua isipokua watu waliamua iwe fair play wamuache agombee na ili uchaguzi uende kwa amani.
Mkuu unachosahau ni kuwa maelekezo ya tume hayatakiwi kukiuka sheria ya uchaguzi. So hoja yako ya utetezi ni dhaifu na haiko kwenye mizani za kisheria
 
Sheria ya Uchaguzi inaipa Mamlaka Tume kukasimu baadhi ya majukumu yake kwa Wasimamizi wa Uchaguzi. Sasa Sheria gani imekiukwa hapo
 
Nilishasema watendaji wa serikali ndio wanaosababisha matatizo kwa wananchi bali sio chama cha mapinduzi

Kwa style hii,Tume ilibidi watulie kwanza kabla ya kumjibu mtu huyo,Sasa wanaleta utata mpya kabisa kwenye uchaguzi huu

Sio kila jambo inabidi kulijibu,kuna mambo unachutama kwanza

Hawa watendaji wanakiharibia chama cha mapinduzi sana kwani wao hawako mstari wa mbele kwenye kutafuta kura

Kanuni za uchaguzi haziruhusiwi kwenda kinyume na Sheria mama ya uchaguzi haya si wanayajua Tume ya uchaguzi

Kitendo cha kumuweka Tundu lisu siku ile masaa zaidi ya saba nilitegemea haya yatajitokeza tu

Hivi Tume mngepokea fomu za jamaa haraka na kumuacha aondoke si mngekiweka chama chetu salama

Nina hakika huyu mtu hakuwaza kuja na mapingamizi bali kitendo cha kumuweka pale masaa kibao ndio madhara yake hayo

Mengi tunashauri hapa,Mfano tulishauri akija toka nje aachwe si aliachwa airport na hajatupunguzia kura na heshma kwa wananchi au nje

Mfano angesumbuliwa siku ile airport wangesema ni ccm imefanya na sio watendaji

Kwanini tunaharibu image ya chama?
Kuna mambo yanafanyika sio kwa maslahi ya chama hasa kwa watendaji
CCM haiwezi kukwepeshwa na wewe, CCM hutoa maelekezo nayo ni "nimekuteua mimi mshahara na mengineyo nakupa mimi, ole wako nikusikie umemtangaza upinzani kuwa ameshinda" halafu wewe unaitetea CCM!
 
Mkuu pole sana kwa kazi,Huu ni wakati wa uchaguzi

Ni wajibu wa kila mwanachama wa ccm kutafuta habari na kuzisoma kwa umakini na kushauri chama

Tafuta hoja za Tundu lisu youtube huko na zisikilize ,Hapa toa ushauri nini kifanyike

Achana na story za darasani kutaka kuandika reference na nani kasema

Ushauri hapa ni huu ufuatao
Tume ya uchaguzi kwa wale ambao wagombea wameondolewa kwa technical ground mfano picha,mwandiko yapasa kuwarudisha

Wagombea ambao kweli imethibitika ni wala rushwa waondolewe na Tume ya uchaguzi

Lengo hapa ni kuondoa chuki kwa wananchi,Tutashinda bali tutashinda kwa mbinu za kisasa

Tulikuwa tayari tumewapiga 18 kwa sifuri sasa majibu ya Tume kwa lisu mmh hapa tuna kazi ya ziada

Tume wangepotezea tu kumjibu ,wangeacha wagombea wajibishane kupitia vyama vyao wenyewe ,Halafu wangepotezea mazima kampeni ziendelee bila kumuengua mtu yeyote
Broo unaakili yakuzaliwa lkn unakosea kitu kimoja tuu sijui kwanini umo ktk kundi la watekaje
 
Mkuu nadhani humjui vizuri Tundu Lissu.Kama unavichukulia vitu juu juu na kwa jinsi anavyopangilia maneno yake, unaweza ukaamini kile anachokiongea ni sahihi. Lissu ni Mwanasheria mbobezi anajua jinsi ya kucheza na maneno na vifungu vya sheria kama ilivyo mahakamani ili kuweza kamshawishi hakimu akubaliane na hoja zake. Mbinu hiyo hiyo ndo anaitumia pia kuwashawishi watu huku nje wasiopenda kutafakari ili waamini anachoongea.

Nimesikiliza hoja za Lissu vizuri sana, kwanza anasema JPM hawakuwasilisha fomu za uteuzi siku iliyotakiwa kisheria. Lakini sote tulimuona JPM siku ile ya tarehe 25 ambayo ni ya uteuzi akiwa na fomu zake, sasa jiulize alienda kufanya nini pale Tume.

Lakini Hoja yake hii anaijenga pia kwenye uhakiki wa wadhamini, kwamba kwann wasimamizi wa uchaguzi ndo wahakiki wadhamini (membe pia wadhamini wake wamehakikiwa na hao wasimamizi wa Jimbo lakini cha ajabu hakumwekea pingamizi). Anarudi tena kusema kwamba tume ndo iliyotoa maelekezo kwa hao wasimamizi kuhakiki wadhamini katika kila jimbo lakini hapo hapo anasema maelekezo hayo yanapingana na sheria. Lakini hafafanui kwamba sheria hiyo ndo inairuhusu Tume kukasimu madaraka yake kwa kadri itakavyoona inafaa kwa wasimamizi wa uchaguzi bila kusema ni madaraka gani. Kwahiyo mpaka hapo utaona tume haikuvunja sheria. Lakini hata kama tume ingekua imevunja sheria kwa kuwapa mamlaka wasimamizi wa uchaguzi, unawezaje kumlaumu/kumuwekea pingamizi mgombea ambae alifuata maelekezo ya Tume.

Infact, Tundu Lissu aliweka mapingamizi siyo kwa maana ya mtego bali kwa kujihami kwasbb toka mwanzo alihisi atakatwa na Tume (Tweet ya mbowe siku moja kabla ya uchaguzi inathibitisha hili) . Baada ya kuona tume haikufanya hivyo, akajua CCM au chama kingine kinaweza kutumiwa kumuwekea pingamizi baada ya uteuzi. Kwsbb anajua zilikuepo sababu nyingi sana za kumuengua isipokua watu waliamua iwe fair play wamuache agombee na ili uchaguzi uende kwa amani.

Kwa hiyo unasemaje?

Kwamba, wagombea udiwani na ubunge waliondolewa using the same ground wafanyweje?

Ni vyema wakarudishwa, right?

Yes. Kwa sbb kwa maelezo ya NEC na sababu za wasimamizi wa uchaguzi majimboni na katani kuwaengua baadhi ya wagombea ubunge na udiwani, obviously, hazisimami tena....

Mwisho, Tundu Lissu na wengine wote kina sisi huku we knew exactly kuwa, mgombea wa CCM Ndg John Pombe Magufuli hata kama angekuwa amevunja/kiuka sheria na kanuni za uchaguzi kwa kiwango gani, ASINGEWEZA KUHUKUMIWA KINYUME NA ILIVYOFANYIKA...!!

Lakini, kwa upande mwingine TL ame - achieve alichotaka kuki achieve...

Huu ni umahiri wa hali ya juu sana...
 
Back
Top Bottom