Uchaguzi 2020 NEC imemteua Dkt. John Pombe Magufuli kugombea Urais na Mama Samia Suluhu Umakamu wa Rais kupitia CCM

Uchaguzi 2020 NEC imemteua Dkt. John Pombe Magufuli kugombea Urais na Mama Samia Suluhu Umakamu wa Rais kupitia CCM

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli arejesha fomu za kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM katika Ofisi za Makao Makuu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Njedengwa Jijini Dodoma. Ameongozana na Mgombea Mwenza Mhe. Samia Suluhu Hassan.

M/kiti wa NEC, Jaji Mstaafu Semistolces Kaijage kwa mamlaka aliyopewa amemteua Dkt. John Pombe Magufuli kuwa mgombea wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mama Samia Suluhu kuwa mgombea wa kiti cha Makamu wa Rais kupitia CCM na kukabidhiwa seti za fomu na nyaraka muhimu kuwa kumbukumbu kwao.

Uchaguzi 2020 - Tundu Lissu awawekea pingamizi wagombea wawili wa nafasi ya Urais wa Tanzania. John Magufuli (CCM) na Prof. Ibrahim Lipumba(CUF)



MaguCCM.JPG
 
Hivi TBC ni Tv ya CCM au ya umma?

Hivi inakuwaje pesa za walipa kodi zinafanya mambo ya chama tawala tu inashindwa kufanya mambo ya vyama vingine...

Huu ndio uhuni anaousema Tundu Lissu Kila siku.

Pesa za umma kutumika pasipo ridhaa ya Wananchi.
 
Hivi TBC ni Tv ya CCM au ya umma?

Hivi inakuwaje pesa za walipa kodi zinafanya mambo ya chama tawala tu inashindwa kufanya mambo ya vyama vingine...

Huu ndio uhuni anaousema Tundu Lissu Kila siku.

Pesa za umma kutumika pasipo ridhaa ya Wananchi.


Rais wa JMTZ anabakia kuwa Rais wa JMTZ mpaka pale Rais mpya atakapoapishwa, hivyo Magufuli ni Rais wa nchi na huwezi kumlinganisha na wagombea wengine, hiyo ni Katiba yetu, ...
 
All the position is locked up and cant get on TV.........is democracy!!?

Acha uwongo.. munapenda kulalamika tu.

Upinzani wao banapenda Twitter.. baendelee.. ruzuku wamekula viongozi.. ofisi za kudumu za Chadema na wengine hawana.. hao sio watulivu.. ni wafanya fujo tu kushiba matumbo yao..

sera hawana.. hawavutii hata watu wa media.. wakitaka kusema ngonjera na mipasho.. ndiwo wanaita media na kuwaomba wafike.. walipo..

Tulia.. demokrasia.. sio kusingizia pande moja.. uwongo.. huku upinzani futi sita.. ni wao walivyo.. tena babaya sana.. matumbo mbele..
 
TBC walipaswa kuwa live kwa wagombea wrote, kitendo cha kubagua sio saws.rai yangu time wawateue wagombea wrote wenye sifa.Umma utaamua kwenye sanduku LA kura.
 
Back
Top Bottom