Uchaguzi 2020 NEC imepokea rufaa 557 za mapingamizi, na imeanza kuzifanyia kazi

Uchaguzi 2020 NEC imepokea rufaa 557 za mapingamizi, na imeanza kuzifanyia kazi

Tengeneza tatizo Kisha litatue[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Alikuwa anahutubia lkn watu wanamchunia tu haoni vigeregere wala makofi
Kwa hiyo Yale Mambo ya kumpa kazi Lissu alikuwa anajisemesha mwenyewe? Na je ni nani alimsimamisha? Police au wananchi wa Ikungi?
 
Katika Uteuzi wa wabunge na madiwani uliokamilika Agosti 26, 2020 wabunge kadhaa waliwekewa mapingamizi hali iliyofanya baadhi ya majimbo kuwa na wagombea wa chama kimoja tu

Agosti 28, Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilitangaza majimbo 18 ambayo wagombea wake wamepita bila kupingwa kutokana na sababu mbalimbali kwa kuzingatia Sheria ya Taifa ya Uchaguzi

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, NEC Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage amesema hadi sasa tume hiyo imepokea rufaa 557 za mapingamizi katika upande wa udiwani na ubunge

Rufaa hizo zimeanza kufanyiwa kazi kuanzia Septemba 01, 2020 kwa kuzingatia sheria na kanuni zilizopo

#JFLeo #JamiiForums #Uchaguzi2020 #TZ2020
Sindano za Kamanda Mbowe zimeanza kuwaingia.
 
Tuipe nafasi tume ifanya maamuzi ya hizo rufaa. NEC pigeni kazi pasipo hofu.
 
Nadhani Tume yetu itakua inashikilia Guinness World Records kwakuwa na maamuzi mabovu yaliyokatiwa rufani kwa wakati mmoja. Rufani 557 si kiashiria kizuri kwa taasisi inayotegemewa kufanya maamuzi yatakayotupatia viongozi wa nchi. Kwa rufani hizo, maamuzi ya hii tume ni yakutilia shaka sana kuliko jambo lingine lolote.
 
Kuna factor ya muda pia, tume inatakiwa kulitambuwa hilo.
 
Hii Tume ya Uchaguzi isijaribu kutuharibia uchaguzi asilani. Upendeleo wowote ule utasababisha tuingie barabarani ili dunia ifahamu UFEDHULI wao.
Waingiaji barabarani huwa awasemi,wanatenda tu.
kwanza barabara ipi mtakayoingia,ya mwendo kasi ama?
 
Kwa Mfano mlalamikaji.akishinda anaanza kupiga kampeni,ilhali.mwenzake,aliyetangazwa kupita bila.kupingwa akiendelea au inakuwa vipi?
 
🛑BREAKING NEWS:

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC ) Jaji Semistocles Kaijage, amesema Tume imepokea Rufaa (mapingamizi) katika ngazi ya Ubunge na Udiwani 557 hadi sasa , nakusema kuwa Tume inaanza kusikiliza na kuzishughulikia Rufaa hizo mara moja kuanzia leo hii https://t.co/AtjrVGdDG9

Kuna kipya gani ukichokiandika? Kwani huu Uzi unahusu nini? Tunahitaji comments, siyo kuurudia Uzi wa mwenzako.
 
Back
Top Bottom