Uchaguzi 2020 NEC imepokea rufaa 557 za mapingamizi, na imeanza kuzifanyia kazi

Uchaguzi 2020 NEC imepokea rufaa 557 za mapingamizi, na imeanza kuzifanyia kazi

Wamefeli sana, uwezo wao wa kuongoza hiyo tume ni mdogo
Akili za kuongoza wanazo ila sema wana kazi mbili ambazo zinakinzana. Ni sawa na daktari hospitalini ambaye amepewa kazi ya kutibu watu, lakini pia kapewa kazi na shetani ya kuua wagonjwa. Sasa kutibu na kuuwa ni shughuli ambazo zinakinzana.
 
Hio tume iache kupokea maelekezo kutoka juu ifiuate sheria na kanuni za chaguzi bila kuaegemea upande mwingine.Haki itendeke.
 
Hahahahahaa natamani wote warudishwe halafu uchaguzi ufanyike na Kabudi Mzee wa jalalani aangukie pua .Atakuwa katika kumbukumbu kuwa aliwahi kutangazwa na tume mshindi lakina baada ya siku chache kabla ya kuapishwa anatenguliwatena na tume HIyo hiyo ,Hiii itaonesha kweli jamaa ni kutoka jalalani
 
Katika Uteuzi wa wabunge na madiwani uliokamilika Agosti 26, 2020 wabunge kadhaa waliwekewa mapingamizi hali iliyofanya baadhi ya majimbo kuwa na wagombea wa chama kimoja tu

Agosti 28, Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilitangaza majimbo 18 ambayo wagombea wake wamepita bila kupingwa kutokana na sababu mbalimbali kwa kuzingatia Sheria ya Taifa ya Uchaguzi

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, NEC Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage amesema hadi sasa tume hiyo imepokea rufaa 557 za mapingamizi katika upande wa udiwani na ubunge

Rufaa hizo zimeanza kufanyiwa kazi kuanzia Septemba 01, 2020 kwa kuzingatia sheria na kanuni zilizopo

#JFLeo #JamiiForums #Uchaguzi2020 #TZ2020
CCM wanafanya kampeni bila shida wenzao wanahaingaika na rufaa
 
Back
Top Bottom