Uchaguzi 2020 NEC: Kila Chama cha Siasa kimeruhusiwa kuweka wakala kwenye kila kituo ili kulinda maslahi ya Chama na Wagombea

Umehitimisha vema, lakini pia njaa haihalalishi 'rushwa' kwa mnunuaji.
Ungepewa nafasi ya kuhakikisha hili tatizo linaisha ungeshuri nini kibadilike,hii hoja ya wanaosema wapige kura kisha wabaki vituoni kuzilinda,unaichukuliaje?
 
Siku ya tarehe 28 Oktober itumieni vzuri
 
Ungepewa nafasi ya kuhakikisha hili tatizo linaisha ungeshuri nini kibadilike,hii hoja ya wanaosema wapige kura kisha wabaki vituoni kuzilinda,unaichukuliaje?

Elimu kwa wapiga kura, mfumo wa kisasa wa upigaji kura.... huwezi kulinda masanduku ikiwa hayo hapo juu yamezingatiwa.
 
Siku ya uchaguzi msije mkasema ati kwamba nakala za matokeo ya kura hazitoshi hivyo hamtawapatia mawakala wa vyama!!
 
Elimu kwa wapiga kura, mfumo wa kisasa wa upigaji kura.... huwezi kulinda masanduku ikiwa hayo hapo juu yamezingatiwa.
🙏🙏, Siioni hoja ya kulinda kura Kama suluhisho,hiyo Ni sawa na kuboresha nyumba yenye msingi mbovu.Mabadiliko yanapaswa kuanzia kwenye mfumo wa kisiasa.Naungana na wewe.
 
Hivi ni kwanini kuna Chama cha Siasa kinapinga sana suala la kubaki kulinda kura mara baada ya kupiga kura? Sheria siinasema ubaki mita 200? Au hiyo Sheria mwaka huu haipo?
 
naskia mawakala hakuna kuingia na simu katika chumba cha kupigia na kuhesabia kura !!
 
Huyu mama yaweza kumkuta ya naibu katibu mkuu elimu.
 
Baada ya kupiga kura wanachama wataruhusiwa kulinda kura zao?
Kazi ya kulinda usalama wa shughuli zote za uchaguzi ni kazi ya polisi sio wanachama wa CHADEMA au chaumma,

Unakwama wapi mkuu?
 
Na asipoenda nyumbani? Mathlani akienda kanisani au msikitini? Kazini? Shambani? Kwa mpango wake wa kando? Kwenye kijiwe cha jirani? Akifanya vyote badala ya kwenda nyumbani atakuwa amekiuka kifungu kipi cha sheria ipi?

Amandla....

hatavucha kifungu cha sheria yoyote,ila akikaa hapo kwa nia ya kulinda kura,akikaa hapo kwa nia ya kucheza mpira,akikaa hapo kwa nia ya kufanya mnada atakuwa navunja sheria.
 
Shida sio kuruhusu au kutoruhusiwa kwa vyama kuweka mawakala wao, bali shida ni figisu na hujuma wanazokumbana nazo mitaani kwenye vituo vya kupigia kura! Kuna wengine huzuiwa kuapishwa kwa sababu tu za kubumba ili chama kikose wakala! Hata walioapishwa kuna sehemu nyingine wan atolewa nje wakati wa kuhesabu kura kwa visingizio vya uongo eti wanafanya fujo!
Tunashauri kama kweli NEC imejipanga kusimamia uchaguzi huu kwa haki na usawa, iandae pia mazingira ya kuhakikisha maazingira ya kuhujumu mawakala hawa hayapewi nafasi!
 
Mi nashauri NEC ingeruhusu mawakala wawepo jimboni tu,,kuweka wakala kila kituo ni gharama sana,bora pesa zinazobaki ziende kwenye mradi wa reli ya umeme,,
 
hatavucha kifungu cha sheria yoyote,ila akikaa hapo kwa nia ya kulinda kura,akikaa hapo kwa nia ya kucheza mpira,akikaa hapo kwa nia ya kufanya mnada atakuwa navunja sheria.
Sheria ipi inamzuia mtu kukaa karibu na kituo cha kupigia kura? Sheria ipi inasema ni activity zipi zimezuiwa kufanywa karibu na kituo cha kupigia kura? Ninavyojua mimi mtanzania ana haki ya kukaa bila kubughudhiwa katika maeneo yote ambayo ni "public" ili mradi hafanyi vitendo ambavyo vimekatazwa na sheria ( kuvuta bangi, kunywa gongo, kupigana n.k.). Mtu atachukuliwa hatua kwa vitendo anavyofanya na sio kwa kujikalia tu. Mtu kama hauna nia mbaya kwa nini uogope watu kushuhudia unachofanya? Mimi ningetegemea kuwa ungependa uwe na mashahidi wengi iwezekanavyo ili pasiwe na shaka juu ya weledi wako.

Amandla...
 
Tumeona hivi karibuni watu wakijitokeza kugombea kwa niaba ya chama ambacho hakijawateua. Na wasimamizi kukataa kata kata kusikiliza hoja za chama ambacho wanadai kimewateua. Haitakuwa ajabu kukuta mawakala wapo tayari wa vyama ambavyo havijawateua. Huu ndio wasiwasi wa wengi. Njia pekee ya kuwaondoa watu huu wasiwasi ni kufanya kila kitu kwa uwazi kabisa na kuvishirikisha vyama vyote kikamilifu katika hali ya usawa.

Amandla...
 
utatolewa kwa kufanya mkusanyiko usio na kibali.
Hahaha yaani kipindi hiki kumekuwa na makosa mengi mpaka shetani mwenyewe anatushangaa. Ukiingia kwenye mikono ya polisi tu hutoki salama
 
hao mawakala waapishwe mapema kuepusha habari za Akwilina
 
Mwakala wa vyama vingine 13 wakiungana dhidi ya wakala 1 kubadilisha matokeo ataweza kujitetea peke yake?
Kama umeshindwa kumwamini wakala wako atizame kura zako sasa umemweka wa Nini?
 
Kwa sababu wanaweza kuhongwa wakabadili matokeo au wakazidiwa nguvu na mawakala wengine wengi wa vyama tofauti lakini wenye mrengo mmoja.
 
Hili nalo linahitaji ruhusa...., au its a given na ni obvious...., Hii nchi unaweza kuambiwa siku moja kwamba tumekupa ruhusa ya kupumua.... na kuvuta oxygen
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…