NEC hivi kweli hamuoni yanayoendelea katika nchi hii kwenye huu uchaguzi na kampeni?
1. Mwiteni mgombea URais wa CCM Kamati ya Maadili ahojiwe na yeye.
Kama kweli NEC mmesheheni wanasheria, Kwanini Rais Magufuli anatoa ahadi na kutekeleza miradi ya serikali wakati akiwa kwenye kampeni na amevalia nguo za CCM? Kuna tofauti gani kati ya kampeni na ziara?
2. Mwiteni na kumuonya Waziri mkuu.
Waziri mkuu anafanya kampeni nchi nzima na kutoa ahadi kama nani na anatumia sheria ya nchi gani?
Mnataka kulipeleka wapi taifa hili? Kwanini mnaanzisha uonevu wa wazi wazi ninyi?
Sasa tunasubiri na hawa muwaandikie barua. Mkikaa kimya tutajua kua mnatumika na Rais hatutakubaliana na hii
double standard.
View attachment 1583749
[/QU
lazima utambue kwamba Mh.Kassimu Majaliwa kwasasa atembei kama Waziri Mkuu,bali yeye ni Mjumbe wa kamati kuu ya CCM.
Pia, Tufahamu kwamba kwamujibu wa kifungu cha 7(3) cha Kanuni ya Taifa ya Uchaguzi, Mgombea atakuwa na timu ya Kampeni kwa lengo la kumnadi na kumsaidia mgombea huyo katika kampeni za Uchaguzi . Mgombea huyu anapaswa kuwasilisha majina ya watu wanaounda timu yake ya kampeni siku mbili kabla ya kuanza kwa mchakato wa uteuzi au siku saba baada ya uteuzi.
Mgombea Urais anakuwa na timu ya kampeni yenye watu 50 waliorodheshwa na chama husika kisha orodha hiyo kuwasilishwa kwa Msajili wa vyama vya siasa (Kanuni ya Taifa ya Uchaguzi ,Kifungu cha 17(1)(a)); hivyo ndg Majaliwa ni miongoni mwa hao watu 50 wanaotambulika.
Hivyohivyo ,Mgombea kiti cha Ubunge kwa Tanzania Bara anapaswa kuwasilisha kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri husika timu yake ya kampeni yenye watu wasiozidi ishirini (20)(Kanuni ya Taifa ya Uchaguzi ,Kifungu cha 17(1)(b)).
Mgombea ubunge kwa Tanzania Zanzibar anapaswa kuwasilisha kwa Katibu Tawala wa Wilaya timu yake ya kampeni yenye watu wasiozidi ishirini (20). (Kanuni 17(1)(b));
,Mgombea kiti cha Udiwani anapaswa kuwasilisha kwa Afisa Mtendaji wa Kata husika timu yake ya kampeni yenye watu wasiozidi kumi(10)(Kanuni ya Taifa ya Uchaguzi ,Kifungu cha 17(1)(b)).
hivyo,tunaposikia tuu majukwaani turudi kwanza kwa utafiti kabla ya kuanza kulalamika na kuporomosha matusi.