The Palm Tree
JF-Expert Member
- Apr 13, 2013
- 7,951
- 12,541
Huyo katibu Mkuu aliyeandika hiyo barua kwanini hatajwi? Imesainiwa na katibu mkuu gani? Huyu huyu John Mnyika?Tatizo lenu mnawaamini Sana viongozi wa chadema kana kwamba wao ni Malaika hapana
Itakuwa ni ajabu sana kuwa Katibu Mkuu John Mnyika aandike barua NEC ikiwa imeambatanishwa na orodha ya majina ya hawa wanawake kisha huyo huyo tena atoke mbele ya vyombo vya habari na kukana kuandika barua na kuipeleka huko huku dunia nzima ikiona na kusikia...
On the other hand, wala hakuna anayesema wao ni malaika na kwamba hawatendi dhambi na kwamba hawajaribiwi na tamaa ya dhambi...
Kinachotakiwa uchunguzi ufanyike ikiwa kuna hatia ya kughushi ama kweli wameandika lakini wanakana tu...
Yote yanawezekana. Lakini lililo wazi na rahisi kufanyika ni dola kutumia mbinu zake zote ovu kulifanikisha hili...