Uchaguzi 2020 NEC: Tulifanya uteuzi wa wabunge wa viti maalum baada ya orodha ya majina hayo kuwasilishwa na Katibu Mkuu wa CHADEMA 19 Novemba 2020

Uchaguzi 2020 NEC: Tulifanya uteuzi wa wabunge wa viti maalum baada ya orodha ya majina hayo kuwasilishwa na Katibu Mkuu wa CHADEMA 19 Novemba 2020

Majna yanawasilishwa kwa fomu , si barua. Kuna fomu zinajazwa, wanaapa, hakimu anasaini etc.... stupid Mahela
Kama hawakuapa kwa hakimu walikwendaje kuapa bungeni? Nyumbu unafikiri kutumia Nini?
 
Hata kama umenyofolewa ubongo basi hata kupapasa huwezi ? hivi Unajua kwamba Nusrat alitolewa gerezani tarehe 23 usiku na Mdee akishirikiana na mfumo ? ni wapi katibu mkuu wa Chadema alimsainisha fomu Nusrat aliyewekwa selo tangu july 2020 ? halafu hata kama kichwani umewekwa udongo tangu lini ccm na Ndugai wakawa watetezi wa wabunge wa Chadema ?
Malalamiko FC...
 
Wafungue kesi kwa mahakama ipi ambayo itatenda haki? hivi CHADEMA wateue mbunge wa viti maalum akatolewe gerezani usiku wa manane kuja kuapisha tena anashitakiwa na jamhuri?

Mdee amesema anashukuru chama chake kwa kumteua! sasa usipige kelele nyingi fukuza kama walienda kinyume
 
Ulitaka walishilughulikie vipi?

Mbona unataka kunitoa kwenye hoja?
Nimeweka bayana kabisa kwamba siasa ni zaidi ya ukahaba, hapo ndio hoja yangu imejikita.

Tufanye NEC wanatudanganya, Je, Mdee si mwanasiasa? Yuko wapi sasa hivi? Nani alitegemea angekua miongoni mwa walioapishwa? Unakumbuka slivyokana hizi tuhuma zilipovuja kutoka kwa Kigogo?

Hapo kinachosubiriwa ni kauli na maamuzi baada ya kikao.
 
Uteuzi tarehe 19.11.2020...Mteuliwa mmoja bado yuko mahabusu...lakini Chadema hawajali wanapeleka jina lake.

Then siku moja kabla ya kuapishwa DPP anaondoa mashtaka usiku. Halafu siku ya pili anaapishwa....

Sijui connection ikoje hapa?
CDM kama ndio wamefanya hivyo,watakuwa wana nguvu kubwa sana na ya pekee. Yaani mpaka mtu anafutiwa kesi usiku bila taratibu kufuatwa!!
 
Hii taarifa ingekuwa na uzito kama ingetolewa kabla ya kuwateua au mara baada ya kuwateua. Na kama barua ilikuwepo, Esther Matiko alipohojiwa angesema Katibu Mkuu wake, sio Mamlaka husika. Inafanya watu wakumbuke mambo yalivyokuwa Ubungo.

Amandla...
 
Tatizo lenu mnawaamini Sana viongozi wa chadema kana kwamba wao ni Malaika hapana

Sasa unataka tuwaamini hao wezi wa kura wasio hata na aibu hao hakuna mtu mwenye akili timamu anaweza kuamini taarifa ya kutoka kwenye hilo genge la wezi wa kura wasitupotezee muda na hizo farm walipopelekewa walijiuliza mtu aliye mahabusu aliwezaje kuapa mbele ya hakimu.

Wanadhania watanzania ni wajinga hivo tangu lini TISS ndo isafirishe watu kwenda kuapa hii nchi ni ya aibu sana ati wanalipwa kodi yetu kwa kufanya hayo mambo ya hovyo wanayofanya hata aibu hawana sisi wananchi tunawaangaliaa tunashangaa hivi wanatuonane
 
Nahisi vyama vyote vilituma majina ya wabunge wa viti maalum hata kabla ya uchaguzi, kulikuwa na mawasiliano hayo napia kujaza form, sasa baada ya uchaguzi kwenda ndivyo sivyo na speaker kuhitaji majina ya wabunge wa viti maallum bila mafanikio basi NEC ikawa imeteua na kumpatia speaker, so labda tuulize kuwa nani huteua wabunge wa viti maalum?

NEC kupitia orodha waliotumiwa au chama chenyewe? kama ni NEC basi uongozi wa chadema hauna kosa kwa sabu list ile ni muda kabla ya uchaguzi na walifanya vile kutimiza matakwa ya sheria za uchaguzi, bado chadema kama hawataki wangewaambia hao walioteuliwa kutokuapishwa na hata sasa inaweza kkuambia wajivue , sasa ni utashi wa mbunge husika kukubali au kukataa.
 
Ulitaka waambatanishe na barua ya Mnyika? Si uende NEC kama unataka kuhakiki mkuu?

Wao watasemaje walipokea barua ambayo haionekani hayo si maneno tu wanadanganya watanzania kwa kuzoea wizi na hata wabunge wa viti maalum wameamuwa kuwapata kwa wizi tu hakuna cha barua wala nini wizi tu umefanyika
 
Umesoma vizuri barua ya NEC hapo juu? Au umeanza kuchangia bila kusoma barua ya NEC? Wanasema walipokea barua tarehe 19/11/2020.
Msome vizuri. Ana maana alitegemea tume iseme ilipokea forms ikibidi ingeongeza tu kusema forms zilizoambatana na barua, hiyo tarehe 19/12/2020. Ndiyo maana anasisitiza kwamba majina yanapelekwa yakiwa yamejazwa kwenye forms. Tena kila mmoja kwa form yake. Ikiwa na maana wabunge 19 ni forms 19 zilipokelewa na tume kutoka CHADEMA. Barua inakua ni kitu cha ku support tu.
 
Back
Top Bottom