Ili kulimaliza suala hili, Mkurugenzi alitakiwa kuweka wazi kuwa aliyeshinda tenda ndio waliyeingia nae mkataba na ndie anayechapisha hayo makaratasi. Alitakiwa kusema wazi kuwa Jamana hahusiki katika uchapishaji wa hayo makaratasi.
Hoja ya Mnyika, kama nilimuelewa, ilikuwa kuwa aliyeshinda hakupewa tenda na anaezichapisha sasa hivi hakuwepo kwenye kuomba hiyo kazi. Aidha, kwa vile kila mdau ana haki ya kuhoji taratibu zilizotumika, Mkurugenzi angejikita kwenye kujibu hoja tu bila kuingiza mambo mengine ambayo yanamfanya aonekane hampendi mtoa hoja. Hii si vizuri.
Amandla...