NEC yafafanua Upotoshaji kuhusu Karatasi za kupiga kura Uchaguzi Mkuu 2020


Kila kitu kipo wazi hapo unataka nini tena? Propaganda?
 
Kwangu attachment ilikuwa haionekani ila ndio naiona sasa.
Mkuu tindo mara kadhaa nimekushauri uwe makini kabla ya kujibu hoja au kujadili liloletwa JF. Tabia hiyo ni ya viongozi wa CJADEMA ambao hukurupuka hadharani kutoa taarifa za tuhuma au malalamiko bila kuthibitisha ukweli wake kwanza.

Wafuasi wa CHADEMA humu JF, usipokuwa makini kwa michango yao, unaweza ukaamini mko pamoja kumbe ni wafuasi watiifu wa Serikali. Huchokonoa ili wapumbavu na lofa wafunguke uongo wao, kama inavyoonekana kwenye mada hii. Mchangiaji makini angetafuta Sheria ya Manunuzi kujiridhisha.

Humu JF wanachama ni wengi hata watumishi wa mamlaka mbalimbali. Wote hawa wanajua ukweli wa kinachoendelea hata mchakato wa kununua vifaa vya Tume ya Uchaguzi. Hivyo wafuasi wa CHADEMA msijifanye ninyi ndio mnajua sana.

MJITATHMINI
 
Majibu hayo hapo.. endeleeni kutafuta kura. Wananchi wanataka viongozi wachapa kazi sio viongozi lialia....
Waendelee kutafuta kura kwa wafuasi wasiokua na vitambulisho vya kupiga kura😁😁😁
 
Chadema hawajijtambi hata kidog
Wakishapewa tetesi za uongo tu
Haooooo wanaitisha mkutano na vyombo vya habari
Sijui wametoa wPi habari za jamana printers
 

Uko sahihi sana, lakini kwa umakini huohuo unaotaka niamini unao, kuna ile mada kuhusu umeme wa maji na gas nimekuuliza, lakini sijaona ukijibu chochote. Au ndio unajipanga? Hayo ya sheria bora ukae kimya, kuwa na sheria ni jambo moja, na kutekeleza kama sheria inavyotaka ni jambo jingine. Usitake kunionyesha eti kuna umakini sana huko serikalini kwa sababu ya uwepo wa sheria, wakati tunaona hati chafu nyingi tu za taasisi za Serikali.
 
Chadema mbona mna vichwa maji wengi? Mbona kila kitu mnataka mtafsiriwe na mume wenu kigogo?
Watu kama wewe ndio mnaoharibu hili jukwaa. Kila kitu ni kutukana tu. Lakini ndio gharama ya mafanikio. Sasa hivi kila mtu mwenye uwezo wa kununua Tecno yumo humu na anajiona ni Great Thinker kutokana na uwezo wake wa kuwatukana watu asiowajua. Kukujibu ni kupoteza wakati.

Amandla...
 
Nakiri kuna mapungufu makubwa ya usimamizi wa sheria kwa sababu mbalimbali ambazo hata wewe Mkuu tindo unazifahamu.

Itoshe kusema matatizo na changamoto za utendaji ziko kila sekta, nchi na mataifa duniani kote na ndio maana kuwepo kwa sheria na marekebisho (amendments) yake mara kwa mara.

Kuhusu mada ya umeme wa maji na gesi nimekujibu. Swali lako pia linatokana na kupokea suala juu juu bila kupata ukweli, ukatoa mchango hasi, na lawama tele. POLE
 

Unakiri kuna mapungufu makubwa kwenye usimamizi wa sheria, huku ukisema hata mimi nazifahamu, ila unashangaa mimi kupokea taarifa na kuitolea mchango hasi! Kwanini usione mchango wangu hasi umeongozwa na mwenendo wa hayo mapungufu makubwa ya usimamizi wa sheria?

Nashukuru kwa kuniletea document kubwa ya gas masteplan, ila nilisoma ya wakati ule tunaimbishwa kuhusu uchumi wa gas, chini ya waziri aliyekuwa na majivuno mtaalamu wa miamba Prof Muhongo. Je hii ya sasa itakuwa ya kweli kuliko ile? Au hii ya sasa inaendana na matamanio ya utawala huu, ila ukija utawala mwingine mtaleta ya kuelezea ubora wa umeme wa uranium au makaa ya mawe, huku mkisema tatizo la umeme wa maji ni mabadiliko ya tabia, na utawala huu ulikuwa wa wapigaji?
 
Mwaka huu watapigwa kotekote, watapigwa kaskazini, kusini, pemba na unguja, kanda ya ziwa, nyanda za juu kusini, central... koooote hakibaki kitu
Polepole anakusalimia .
 

Kila kitu kipo wazi hapo unataka nini tena? Propaganda?

Kiko wazi vipi?
Kuna haja ya kuwa makini na majibu yetu. Tenda imefunguliwa tarehe 8 Aprili 2020, vyama vya siasa vimeandikiwa barua kuambiwa wapeleke majina ya kuunda Kamati ya kitaifa ya manunuzi zaidi ya miezi miwili baadae, tarehe 30 Juni 2020. Kamati hiyo imekaa kwa mara ya kwanza tarehe 8 Oktoba 2020, siku nne zilizopita lakini tunaambiwa imekuwa ikifanya kazi kwa muda mrefu sasa. Katika maelezo ya Mkurugenzi hakuna mahali ambapo amesema kuwa kampuni iliyoshinda tenda ndio imepewa tenda hiyo na kuwa kampuni inayoshutumiwa haihusiki katika uchapishaji wa makaratasi ya kura. Alichokisema ni kuwa haikuwemo katika mchakato ambayo siyo sawa na kusema haichapishi makaratasi hayo. Kwa vile haya ni mambo ambayo Mnyika ndio alioyahoji, ilikuwa ni rahisi kuyafanunua kwa kusema tu kuwa kampuni iliyoshinda tenda ndio imechapisha makaratasi hayo na hiyo inayozushiwa haihusiki katika uchapishaji huo. Hapo Mnyika angeonekana kuwa amekurupuka na kuufunga mjadala. Lakini kwa kujibu alivyojibu, amemuachia njia ya kutokea.

Amandla...
 
Mkuu sikiliza tenda na tarehe ilipotolewa pamoja na vielelezo. Mbona una haraka sana unakimbilia wapi? Usikurupuke!
 
Huyu mwanaccm kindakindaki aliyepo tume hana chochote..
Jibu hoja wewe bwege. Malalamiko FC kila mnachopanga kinabuma hili nalo limebuma tena! Eti mnamtegemea Kigogo mavi ndiyo mtoa taarifa wenu!
 
Huwezi kuelewa wewe kichwa chako kidogo sana!
 
Mkuu sikiliza tenda na tarehe ilipotolewa pamoja na vielelezo. Mbona una haraka sana unakimbilia wapi? Usikurupuke!
Nimesikiliza vizuri sana Mkuu. Hizo tarehe nilizozitaja nimezipata baada ya kusikiliza.

Amandla....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…