Uchaguzi 2020 NEC yakiri haijapokea majina ya CHADEMA Viti Maalum. Hongera CHADEMA kwa msimamo

Uchaguzi 2020 NEC yakiri haijapokea majina ya CHADEMA Viti Maalum. Hongera CHADEMA kwa msimamo

Quinine

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
22,227
Reaction score
49,628
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imesema haijapokea orodha ya majina ya wabunge wa viti maalumu kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Akizungumza na Nipashe jana kwa njia ya simu, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Dk. Wilson Mahera, alisema tume bado haijapokea orodha hiyo kama ambavyo imekuwa ikisambazwa kwenye mitandao ya kijamii.

“Kuna orodha ya majina inayosambaa kwenye mitandao ikionyesha majina ya wabunge wa Viti Maalumu wa CHADEMA. Orodha hiyo si ya kweli kwani hadi sasa hatujapokea orodha ya majina ya walioteuliwa kwenye nafasi ya ubunge wa viti maalumu kutoka chama hicho,” alisema.

Mkurugenzi huyo alisema amesikitishwa na taarifa ya Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika, iliyodai kuwa orodha ya majina hayo ni ya tume.

“Tume tumesikitishwa sana kusikia Katibu wa CHADEMA, John Mnyika, akidai kuwa orodha ya majina ya wa bunge wa viti maalumu ni ya tume. Imetusikitisha sana kwa kuwa siyo kweli,” aliongeza.

Dk. Mahera alisema aliwasiliana na Mnyika kwa kumpigia simu na kumwandikia barua ya kuulizia orodha ya majina hayo na kumwambia asubiri mpaka atakapoyaleta yeye mwenyewe baada ya utaratibu wa chama kukamilika.

“Mnyika mwenyewe anafahamu kuwa bado hatujapokea majina na alisema atayaleta majina hayo yeye mwenye endapo watakamilisha utaratibu wao, hivyo mpaka sasa hivi, NEC hatujapokea majina kutoka CHADEMA ambayo yamesainiwa na Katibu Mkuu wa chama hicho,” alisema Mahera.

“Bado tunasubiri majina hayo ambayo yametiwa saini na kupigwa muhuri wa Katibu Mkuu wa chama kwa kuwa utaratibu ndio unaelekeza hivyo,” alisisitiza.

Kutokana na kuvuja kwa orodha hiyo, kuna taarifa kwamba Mnyika alimwandikia barua Dk. Mahera, kutaka kupewa ufafanuzi kama tume imeshatangaza na kuwasilisha bungeni majina 19 ya wabunge wa viti maalumu wa chama hicho.

Aidha, tangu kutoka kwa mijana hayo kwenye mitandao, kumekuwa na taharuki juu ya chanzo halisi cha majini hayo, huku wapinzani, wakiwamo CHADEMA, wakiirushia lawama NEC kuwa ndiyo imehusika.

Chanzo cha habari ni Gazeti la Nipashe
 
Ni jambo jema, Ile orodha iliandaliwa Ufipa ili kutest zali.

CHADEMA sasa pelekeni ile orodha ya mzee Mgaya ya Wabunge waliofeli majimboni akina Mdee, Mwakagenda, Peneza, Bulaya Matiko Ruge, Pareso, Kiwanga nk nk!

Siasa siyo Uadui

Maendeleo hayana vyama!
 
Demokrasia haimaanishi lazima kuwe na Wabunge wa Upinzani. Watanzania wameamua kuchagua Wabunge wa CCM. Maamuzi yao ndio demokrasia.

Siku wakitaka kuchagua wapinzani watawachagua.

CHADEMA kama hawataki kushiriki Bunge ni chaguo lao. Kwanza wananchi wameshawakataa kwa kiasi kikubwa, kwahiyo hakuna madhara yoyote wasipokuwepo.
 
Demokrasia haimaanishi lazima kuwe na wabunge wa upinzani. Watanzania wameamua kuchagua wabunge wa CCM. Maamuzi yao ndio demokrasia....
Ni wakati wa kuendelea na maisha hivyo acheni kulialia badala yake pigeni kazi!Hizi habari za CDM ninyi wa upande huo ndio mmekuwa mnazikuza sana kuhusu viti maalum!

Napendekeza hata hao walioko bungeni wajiunge na CCM ili kusiwe ns kisingizio cha maendeleo kuchelewa!
 
Demokrasia haimaanishi lazima kuwe na wabunge wa upinzani. Watanzania wameamua kuchagua wabunge wa CCM. Maamuzi yao ndio demokrasia.

Siku wakitaka kuchagua wapinzani watawachagua.

Chadema kama hawataki kushiriki Bunge ni chaguo lao. Kwanza wananchi wameshawakataa kwa kiasi kikubwa, kwahiyo hakuna madhara yoyote wasipokuwepo.
Sizitaki mbichi hizi.
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Na bahati nzuri wenye majina yao "wametulia"
Hivi yule Aida ndo katushinda?
 
Tume hii ni very democratic. Inazingatia uhuru wa mawazo ya kila chama.
 
Ni jambo jema

Ile orodha iliandaliwa Ufipa ili kutest zali...
CHADEMA sasa pelekeni ile orodha ya mzee Mgaya ya wabunge waliofeli majimboni akina Mdee, Mwakagenda, Peneza, Bulaya Matiko Ruge, Pareso, Kiwanga nk nk!

Siasa siyo Uadui

Maendeleo hayana vyama!
Tayari Spika anayo na kasema wasipohudhuria mikutano mitatu watajifukuzisha, sijui aliwaapisha lini.
 
Demokrasia haimaanishi lazima kuwe na wabunge wa upinzani. Watanzania wameamua kuchagua wabunge wa CCM. Maamuzi yao ndio demokrasia.

Siku wakitaka kuchagua wapinzani watawachagua.

Chadema kama hawataki kushiriki Bunge ni chaguo lao. Kwanza wananchi wameshawakataa kwa kiasi kikubwa, kwahiyo hakuna madhara yoyote wasipokuwepo.
Usikute umesoma hadi chuo kikuu.
 
Demokrasia haimaanishi lazima kuwe na wabunge wa upinzani. Watanzania wameamua kuchagua wabunge wa CCM. Maamuzi yao ndio demokrasia.

Siku wakitaka kuchagua wapinzani watawachagua.

Chadema kama hawataki kushiriki Bunge ni chaguo lao. Kwanza wananchi wameshawakataa kwa kiasi kikubwa, kwahiyo hakuna madhara yoyote wasipokuwepo.

Kukataa au kukubali vyote ni haki yao ya kidemokrasia😁
 
Demokrasia haimaanishi lazima kuwe na wabunge wa upinzani. Watanzania wameamua kuchagua wabunge wa CCM. Maamuzi yao ndio demokrasia...
Balozi wa nchi za Ulaya nchini Kenya, Simon Mordue atakutana na aliyewahi kuwa Mbunge wa Arusha mjini nchini Tanzania Godbless Lema siku ya Ijumaa tarehe 13/11/2020 jijini Nairobi.
 
Back
Top Bottom