Uchaguzi 2020 NEC yakiri haijapokea majina ya CHADEMA Viti Maalum. Hongera CHADEMA kwa msimamo

Ni jambo jema, Ile orodha iliandaliwa Ufipa ili kutest zali.

CHADEMA sasa pelekeni ile orodha ya mzee Mgaya ya wabunge waliofeli majimboni akina Mdee, Mwakagenda, Peneza, Bulaya Matiko Ruge, Pareso, Kiwanga nk nk!

Siasa siyo Uadui

Maendeleo hayana vyama!

Job alisema Wapinzani awatorudi Bungeni wanakwamisha maendeleo mbona hamtaki kusikia, tunataka kusiwepo na kisingizio cha ukwamisho wa maendeleo
 
Kama hamkuwataka majimboni why muwatake kilazima kwenye viti maalumu, wapeni wake za mapolisi, wakuu wa vyombo, mke wa Mahera ili column itimie.
Kwani bila upinzani bunge haliendi?
 
CHADEMA sasa pelekeni ile orodha ya mzee Mgaya ya wabunge waliofeli majimboni akina Mdee, Mwakagenda, Peneza, Bulaya Matiko Ruge, Pareso, Kiwanga nk nk!

Siasa siyo Uadui
Ni kweli kabisa, ila kwa Tz tena awamu hii siasa ni uadui mkubwa kabisa!
 
Unajibuje utapeleka wakati hutambui matokeo yaliyopelekea mpewe nafasi hizo?
Mbona unataka ligi kwa jambo lisilo mbele na nyuma? Kwanza hapa hatujadili kauli ya Mnyika tunajadili kauli ya Mahera. Hata hivyo Mahera kasema Mnyika atapeleka ENDAPO watakamilisha utaratibu wao unaujua ni upi na wataamua nini.
 
Demokrasia haimaanishi lazima kuwe na Wabunge wa Upinzani. Watanzania wameamua kuchagua Wabunge wa CCM. Maamuzi yao ndio demokrasia.

Siku wakitaka kuchagua wapinzani watawachagua.

CHADEMA kama hawataki kushiriki Bunge ni chaguo lao. Kwanza wananchi wameshawakataa kwa kiasi kikubwa, kwahiyo hakuna madhara yoyote wasipokuwepo.

Hujui madhara yake wewe dogo! Pale bungeni kuna kamati tatu zilikuwepo na zilikua na msaada kutoka kwa mabeberu takriban Trillion 2 kwa mwaka! Kamati zile zilitokana na uwepo wa upinzani, leo zimefutika na kwa maana hiyo Trillion 2 imeyeyuka! Usifurahie kila kitu, vingine jaribu ku-digest tu kidogo!!! Binafsi sio mwanasiasa, wala sina chama. Nawapenda wote wenye fikra pevu ambao hawafikirii kwa kutumia tumbo kama wewe! Jaribu kutumia akili zilizopo kichwani, it will sound good.
 
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imesema haijapokea orodha ya majina ya wabunge wa viti maalumu kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Akizungumza na Nipashe jana kwa njia ya simu, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Dk. Wilson Mahera, alisema tume bado haijapokea orodha hiyo kama ambavyo imekuwa ikisambazwa kwenye mitandao ya kijamii.

“Kuna orodha ya majina inayosambaa kwenye mitandao ikionyesha majina ya wabunge wa Viti Maalumu wa CHADEMA. Orodha hiyo si ya kweli kwani hadi sasa hatujapokea orodha ya majina ya walioteuliwa kwenye nafasi ya ubunge wa viti maalumu kutoka chama hicho,” alisema.

Mkurugenzi huyo alisema amesikitishwa na taarifa ya Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika, iliyodai kuwa orodha ya majina hayo ni ya tume.

“Tume tumesikitishwa sana kusikia Katibu wa CHADEMA, John Mnyika, akidai kuwa orodha ya majina ya wa bunge wa viti maalumu ni ya tume. Imetusikitisha sana kwa kuwa siyo kweli,” aliongeza.

Dk. Mahera alisema aliwasiliana na Mnyika kwa kumpigia simu na kumwandikia barua ya kuulizia orodha ya majina hayo na kumwambia asubiri mpaka atakapoyaleta yeye mwenyewe baada ya utaratibu wa chama kukamilika.

“Mnyika mwenyewe anafahamu kuwa bado hatujapokea majina na alisema atayaleta majina hayo yeye mwenye endapo watakamilisha utaratibu wao, hivyo mpaka sasa hivi, NEC hatujapokea majina kutoka CHADEMA ambayo yamesainiwa na Katibu Mkuu wa chama hicho,” alisema Mahera.

“Bado tunasubiri majina hayo ambayo yametiwa saini na kupigwa muhuri wa Katibu Mkuu wa chama kwa kuwa utaratibu ndio unaelekeza hivyo,” alisisitiza.

Kutokana na kuvuja kwa orodha hiyo, kuna taarifa kwamba Mnyika alimwandikia barua Dk. Mahera, kutaka kupewa ufafanuzi kama tume imeshatangaza na kuwasilisha bungeni majina 19 ya wabunge wa viti maalumu wa chama hicho.

Aidha, tangu kutoka kwa mijana hayo kwenye mitandao, kumekuwa na taharuki juu ya chanzo halisi cha majini hayo, huku wapinzani, wakiwamo CHADEMA, wakiirushia lawama NEC kuwa ndiyo imehusika.
 
Sasa kwa nini hadi sasa hawapeleki majina yao hadi sasa inamana Wana Susa maendeleo ifikie mahali waache ukada na kuunga mkono maendeleo.
 
Tume hii ni very democratic. Inazingatia uhuru wa mawazo ya kila cham
Uhuru na Mawazo ya vyama vya uupinzani baada ya uchaguzi vitasaidia nini? Waendelee wenyewe huko Bungeni, lengo lao limetimia.
 
Ni jambo jema, Ile orodha iliandaliwa Ufipa ili kutest zali.

CHADEMA sasa pelekeni ile orodha ya mzee Mgaya ya Wabunge waliofeli majimboni akina Mdee, Mwakagenda, Peneza, Bulaya Matiko Ruge, Pareso, Kiwanga nk nk!

Siasa siyo Uadui

Maendeleo hayana vyama!
Wanapaswa kuunga juhudi za maendeleo waache fikra potofu.
 
Mlikuwa mnatamani Chadema ifutike na bado manabii wenu wakasema hakuna mbunge hata mmoja wa Chadema atakayerudi bungeni,kiufupi ni kwamba MNAWACHUKIA SANA CHADEMA. Sasa leo mbona mnawabembeleza wapeleke wabunge wa viti maalumu bungeni?
 
Sio tunawalazimisha bali ni kwamba tunawatoa kwenye fikra potofu
 
Spika kasema Kuna maneno uteuzi wa akina mama viti maalumu vyama vya upinzani kwa akina mama

Spika kaonya wabunge viti maalum upinzani wajihadhari na rushwa isiyoeleweka kuwa wataeuliwa huko vyama vyao wakijirahisisha kirushwa wasije kwenda kumshtakia wakikosa kuwa ohh Mimi Kuna Rushwa isiyoeleweka nilitoa na chama hakikuniteua

Kasema ndio maana Kuna ucheleweshaji kuwateua kwa visingizio vya kutunga Kuna maneno huko vyama vya upinzani

Quote
 
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imesema haijapokea orodha ya majina ya wabunge wa viti maalumu kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Akizungumza na Nipashe jana kwa njia ya simu, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Dk. Wilson Mahera, alisema tume bado haijapokea orodha hiyo kama ambavyo imekuwa ikisambazwa kwenye mitandao ya kijamii.

“Kuna orodha ya majina inayosambaa kwenye mitandao ikionyesha majina ya wabunge wa Viti Maalumu wa CHADEMA. Orodha hiyo si ya kweli kwani hadi sasa hatujapokea orodha ya majina ya walioteuliwa kwenye nafasi ya ubunge wa viti maalumu kutoka chama hicho,” alisema.

Mkurugenzi huyo alisema amesikitishwa na taarifa ya Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika, iliyodai kuwa orodha ya majina hayo ni ya tume.

“Tume tumesikitishwa sana kusikia Katibu wa CHADEMA, John Mnyika, akidai kuwa orodha ya majina ya wa bunge wa viti maalumu ni ya tume. Imetusikitisha sana kwa kuwa siyo kweli,” aliongeza.

Dk. Mahera alisema aliwasiliana na Mnyika kwa kumpigia simu na kumwandikia barua ya kuulizia orodha ya majina hayo na kumwambia asubiri mpaka atakapoyaleta yeye mwenyewe baada ya utaratibu wa chama kukamilika.

“Mnyika mwenyewe anafahamu kuwa bado hatujapokea majina na alisema atayaleta majina hayo yeye mwenye endapo watakamilisha utaratibu wao, hivyo mpaka sasa hivi, NEC hatujapokea majina kutoka CHADEMA ambayo yamesainiwa na Katibu Mkuu wa chama hicho,” alisema Mahera.

“Bado tunasubiri majina hayo ambayo yametiwa saini na kupigwa muhuri wa Katibu Mkuu wa chama kwa kuwa utaratibu ndio unaelekeza hivyo,” alisisitiza.

Kutokana na kuvuja kwa orodha hiyo, kuna taarifa kwamba Mnyika alimwandikia barua Dk. Mahera, kutaka kupewa ufafanuzi kama tume imeshatangaza na kuwasilisha bungeni majina 19 ya wabunge wa viti maalumu wa chama hicho.

Aidha, tangu kutoka kwa mijana hayo kwenye mitandao, kumekuwa na taharuki juu ya chanzo halisi cha majini hayo, huku wapinzani, wakiwamo CHADEMA, wakiirushia lawama NEC kuwa ndiyo imehusika.

Chanzo cha habari ni Gazeti la Nipashe
Kaogopa aibu ya pili..
 
Demokrasia haimaanishi lazima kuwe na Wabunge wa Upinzani. Watanzania wameamua kuchagua Wabunge wa CCM. Maamuzi yao ndio demokrasia.

Siku wakitaka kuchagua wapinzani watawachagua.

CHADEMA kama hawataki kushiriki Bunge ni chaguo lao. Kwanza wananchi wameshawakataa kwa kiasi kikubwa, kwahiyo hakuna madhara yoyote wasipokuwepo.
Yani nakubaliana na wewe, CHADEMA isipeleke wabunge viti maalum kwasababu wananchi wameisha ikataa, kwanini CCM inalazimisha?!

Viti maalum sio hitaji la watanzania hawakupigiwa kura, wale wa CCM wanatosha au waongeze hao 19 kutoka CCM ili kukoleza rangi Bungeni.

Hawa CHADEMA wanawachelewesha kuleta maendeleo sijui kwanini wawe ni hitaji tena la bunge hadi wasikitishwe kwa kutokuwepo.
 
Back
Top Bottom