Narudia tena, kwenye ushindani kuna kushinda na kushindwa na yote ni matokeo sahihi. Cha muhimu ushinde au ushindwe kihalali hilo ndio la msingi.
Matokeo yeyote kwenye uchaguzi huu bila kujali nani mshindi, yamewaka wazi kuwa nchi hii haiwezi kutawaliwa na ccm tena, kama chama pekee chenye nguvu kwa ridhaa ya wananchi walio wengi.
Ndani ya hii miaka mitano, Magufuli kwa ulevi na matumizi mabaya ya madaraka, yeye na wapambe wake walitaka tuamini kuwa upinzani umekufa, na ccm inakubalika sana. Na hata kama Magufuli alijiandaa kujiongezea madaraka zaidi ya miaka kumi, basi matumaini hayo yamefutika rasmi kwenye kampeni hizi. Na iwapo ccm haitatumia mbinu chafu ambazo ndio nguzo yake pekee inaweza kupoteza dola, na hata kama itashinda basi ni kwa ushindi mwembamba mno. Kwenye uchaguzi huu tuendelee kuomba wananchi wabaki na ukondoo wao, uliovikwa koti liitwalo amani, kinyume na hapo iwapo wapinzani watasimama mshindi halali atangazwe, basi katiba mpya na tume huru ya uchaguzi lazima ipatikane.