Uchaguzi 2020 NEC yatoa siku 2 kwa Vyama vilivyopata changamoto kutambulisha Wagombea wao baada ya Watu wasioteuliwa kuchukua fomu za Uteuzi

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema inafuatilia zoezi la kuchukua fomu za uteuzi na kubaini kuwa kuna changamoto ambazo zimejitokeza kutokana na vyama vya siasa kutokujipanga na kuweka utaratibu mzuri wa Wagombea wao kuchukua fomu za Utezi

Tume imesema kutokana na hilo watu ambao hawakuteuliwa na vyama vyao wamejitokeza na kwenda kuchukua fomu za uteuzi za kugombea Ubunge au Udiwani bila ridhaa ya vyama husika na kupelekea walioteuliwa kushindwa kuchukua fomu

Kwa mujibu wa Tume hiyo Majimbo yaliyoathirika ni Kibamba, Mbagala, Kilombero, na Kigamboni

Hivyo, Tume imetoa nafasi kwa vyama vya siasa kuwatambulisha Wagombea wao kwa Wasimamizi wa Uchaguzi ndani ya siku 2 kuanzia Agosti 20, 2020 kwa majimbo na Kata zilizo na changamoto


 
Kigamboni?Kwamba makonda amechukua fomu wakati hajateuliwa?
 
Tumewastukia, na jana janja yenu. Sio kweli hata kidogo mtu aje tu na mumpe form. Wasimamzi wa Chaguzi hizi wanataka tu kuonekana kwa Magufuli kuwa "wameipigania CCM"ili teuzi zijazo wasipitwe.
 
Barua wameandikiwa Chadema; so walioathirika ni Chadema hivyo hakukuwa na sababu barua kusema "... watu ambao hawakuteuliwa na vyama vyao ..." ilitakiwa iseme "... watu ambao hawakuteuliwa na chama chako ...". Chadema ni lulu!
 
Tume ya UCHAGUZI iongeze vipengele vya kuacha Picha, nakala ya kitambulisho na namba ya simu kwa Msimamizi wa Uchaguzi (DED's) kama kweli wanataka (NIA YA DHATI) kuwakamata hawo WAHUNI .

Pamoja na hayo, aongozane na kiongozi wa chama husika na wote wapigwe picha. Vyama vitakiwe kupeleka majina (pamoja na picha) za viongozi watakaoongozana na wagombea wake.

Amandla...
 
Hapana, unaamini wewe unaweza kwenda kwenye ofisi ukawaambia naomba fomu ya kugombea ubunge kisha ukapewa bila ya ushahidi wa chama chako! Hii sasa tumor ndani ya basi la kwenda Manyara ABIRIA CHUNGA MZIGO WAKO.
Kuna maajabu mengi sana. Form ilikuwa moja tu na imeishachukuliwa alafa inapatikana ya kumpa mgombea halali ndani ya masaa machache.
NEC must be serious on transparency.
 
Sidhani kwamba ni tatizo la vyama vya siasa kutojipanga Mh Dr Mahera. Najua umetumia maneno hayo ili kuwalinda hao wasimamizi. Tume fikirieni hao wasimamizi ikiwa bado wana uhalali wa kusimamia maeneo hayo. Sijui kama vyama husika na wapiga kura wake winawaona kwamba hawana upande - yaani impartial
 

Serikali ya CCM iliwang'ang'ania hawo WAKURUGENZI kwa maana hiyo kwani ni wateule wa rais hivyo hamtaweza kuwafanya chochote.

Mfano hai ni yule wa Kinondoni na tukio la kuuawa kwa RIP Aquiline.

Tume ya UCHAGUZI nayo KIMYA wote ni wateule wa rais.

Watendaji wakuu wa tume waombe kazi kwa TUME MAALUM YA VYAMA VYA SIASA.
 
Kuna maajabu mengi sana. Form ilikuwa moja tu na imeishachukuliwa alafa inapatikana ya kumpa mgombea halali ndani ya masaa machache.
NEC must be serious on transparency.
Hiyo nyingine ni kati ya zile za chini ya meza, jungu kuu halikosi ukoko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…