Uchaguzi 2020 NEC yatoa siku 2 kwa Vyama vilivyopata changamoto kutambulisha Wagombea wao baada ya Watu wasioteuliwa kuchukua fomu za Uteuzi

NEC yatoa siku 2 kwa Vyama vilivyopata changamoto kutambulisha Wagombea wao baada ya Watu wasioteuliwa kuchukua fomu za Uteuzi
August 21, 2020 .

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema inafuatilia zoezi la kuchukua fomu za uteuzi na kubaini kuwa kuna changamoto ambazo zimejitokeza kutokana na vyama vya siasa kutokujipanga na kuweka utaratibu mzuri wa Wagombea wao kuchukua fomu za Utezi

Tume imesema kutokana na hilo watu ambao hawakuteuliwa na vyama vyao wamejitokeza na kwenda kuchukua fomu za uteuzi za kugombea Ubunge au Udiwani bila ridhaa ya vyama husika na kupelekea walioteuliwa kushindwa kuchukua fomu

Kwa mujibu wa Tume hiyo Majimbo yaliyoathirika ni Kibamba, Mbagala, Kilombero, na Kigamboni

Hivyo, Tume imetoa nafasi kwa vyama vya siasa kuwatambulisha Wagombea wao kwa Wasimamizi wa Uchaguzi ndani ya siku 2 kuanzia Agosti 20, 2020 kwa majimbo na Kata zilizo na changamoto.

My take: Afadhali maana Hawa makada wenzetu walianza kumtafutia lawama Mh. Rais na CCM
 
Hata wakati wa zoezi la kumtangaza mshindi wa kiti cha ubunge/udiwani, iwapo hao makada na wakurugenzi wa hizo halmashauri wakiamua kwa makusudi kabisa kupindua matokeo na kusababisha uvunjifu wa amani, bado CCM na Mwenyekiti hawawezi kukwepa lawama!

Inakuaje umteue mwamuzi wa mchezo ambaye anaegemea/ni mlengo wa upande mmoja?
 
kwani nao awaogopi kuweka rehani familia zao hadi wajitoe ufahamu kihivo
 
NEC yatoa siku 2 kwa Vyama vilivyopata changamoto kutambulisha Wagombea wao baada ya Watu wasioteuliwa kuchukua fomu za Uteuzi
August 21, 2020 .

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema inafuatilia zoezi la kuchukua fomu za uteuzi na kubaini kuwa kuna changamoto ambazo zimejitokeza kutokana na vyama vya siasa kutokujipanga na kuweka utaratibu mzuri wa Wagombea wao kuchukua fomu za Utezi

Tume imesema kutokana na hilo watu ambao hawakuteuliwa na vyama vyao wamejitokeza na kwenda kuchukua fomu za uteuzi za kugombea Ubunge au Udiwani bila ridhaa ya vyama husika na kupelekea walioteuliwa kushindwa kuchukua fomu

Kwa mujibu wa Tume hiyo Majimbo yaliyoathirika ni Kibamba, Mbagala, Kilombero, na Kigamboni

Hivyo, Tume imetoa nafasi kwa vyama vya siasa kuwatambulisha Wagombea wao kwa Wasimamizi wa Uchaguzi ndani ya siku 2 kuanzia Agosti 20, 2020 kwa majimbo na Kata zilizo na changamoto.

My take: Afadhali maana Hawa makada wenzetu walianza kumtafutia lawama Mh. Rais na CCM
Naipongeza hii tume kwa mara ya kwanza toka nizaliwe
 
Tume huru ya Uchaguzi ni muhimu sana,
Kama kweli hamtaki tufikie ya Syria, tutafunane maini wenyewe kwa wenyewe.
Mimi nafsni mwangu, nimehapa kufa au kupona, Uchaguzi huu CHADEMA tukidhurumiwa hata udiwani nakula maini ya CCM yoyote yule.
 
Hivi kilombero kapitishwa nani?

Abubakary Assenga. Ndiye aliyenyang'anywa tonge na Lijualikali mwaka 2015 kwa msaada mkubwa wa Nguvu ya Umma na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa ujumla wake.

Mlimba nako Godwin Kunambi atajiuliza baada ya kugaragazwa na Suzan Kiwanga mwaka huo huo 2015! All in all, Wapiga kura wa Wilaya ya Kilombero kwa ujumla wake huwa hawatabiriki nyakati za uchaguzi.
 
Baada ya ile Barua ya kampuni ya Kisheria kutoka Amsterdam kuwahusisha NEC na figisu figisu za Uchaguzi ndio maana yote haya!
 
Abubakary Assenga. Ndiye aliyenyang'anywa tonge na Lijualikali mwaka 2015 kwa msaada mkubwa wa Nguvu ya Umma na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa ujumla wake.

Mlimba nako Godwin Kunambi atajiuliza baada ya kugaragazwa na Suzan Kiwanga mwaka huo huo 2015! All in all, Wapiga kura wa Wilaya ya Kilombero kwa ujumla wake huwa hawatabiriki nyakati za uchaguzi.
Atapambana na nani kutoka chadema? Maana kuna yule dogo nabii au siyo
 
Naipongeza sana , Sana Tume ya Taida ya Uchaguzi ikiongozwa Na Jaji Kaijage ! Kwa kweli MUNGU yupo pamoja na Tume hii . Safari hii kweli hofu ya MUNGU ipo kwa Wajumbe wa Tume hii safari hii ! Nakupongeza Sana Mheshimiwa Kaijage ( Mwenyekiti ) wa Tume .
 
Atapambana na nani kutoka chadema? Maana kuna yule dogo nabii au siyo

Bila shaka atakuwa ni huyo huyo anayejiita Nabii Shilla. Nawaombea Chadema kila la heri ingawa watatakiwa kupambana kweli kweli kutetea hayo majimbo.
Maana historia inaibeba zaidi Ccm. Nilikuwepo huko tangu enzi za akina Jaji Edward Mwesiumo (Rip), Abbas Gulamali (Rip), nk.
 
Sidhani hili ni swala la vyama vya siasa. Ni swala la Tume kuwa na taratibu dhaifu!!

Tume inapaswa kufanya kazi kama mahakama na ndio maana wenyeviti wake wanakuwa ni majaji au mahakimu. Ili dhamani itolewe kuna masharti ya utambulisho wa mtoa dhamana. Kwanini anayedhaminiwa na chama kuwa mgombea asiwe na utambulisho wake na wa kiongozi halali wa chama husika???

Lazima kuwe na sheria au utaratibu rasmi utakaotolewa na Tume, hili jambo si la ushauri!!
 
Wamechukua hatua gani kwa yule DED alokuwa anabwabwaja kama mlevi? Alizani fomu za kugombe ubunge ni sawa na kadi za CCM wanawezafanya mass distribution bila kujali wanayompa ni raia wa tz au siyo!
 
Huna lolote mbona umekuja na ID fake ufipa bwana[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji38][emoji38]
Tume huru ya Uchaguzi ni muhimu sana,
Kama kweli hamtaki tufikie ya Syria, tutafunane maini wenyewe kwa wenyewe.
Mimi nafsni mwangu, nimehapa kufa au kupona, Uchaguzi huu CHADEMA tukidhurumiwa hata udiwani nakula maini ya CCM yoyote yule.
 
Barua wameandikiwa Chadema; so walioathirika ni Chadema hivyo hakukuwa na sababu barua kusema "... watu ambao hawakuteuliwa na vyama vyao ..." ilitakiwa iseme "... watu ambao hawakuteuliwa na chama chako ...". Chadema ni lulu!

Bora hata umeweza kuona hilo kosa. Nahisi hata barua yenyewe ni fake. Ama ni barua imefanyiwa uhariri kutoka nakala mama, lakini uhariri umefanywa na mtu mwenye uwezo mdogo, huku mwenyekiti wa tume kama ni kweli, akiwa amesaini bila kusoma.
 
Back
Top Bottom