Uchaguzi 2020 NEC yatoa siku 2 kwa Vyama vilivyopata changamoto kutambulisha Wagombea wao baada ya Watu wasioteuliwa kuchukua fomu za Uteuzi

Huu ni mtego hatari sana, haiwezekani tume itoe tu fomu kwa kila mtu bila kujiridhisha kwamba muombaji/mchukuaji fomu ameambatanisha vielelezo sahihi ama magumashi. Halafu tume itoe siku 2 tu, ili baadae iwe kisingizio kwamba chama flani hakitoweza kusimamisha mgombea kwa kutokukamilisha masharti/utaratibu wa tume. Uchaguzi wa mwaka huu utakuwa na hatari sana za kiusalama kama wenye mamlaka/dhamana wasipokuwa makini na kudhani kwamba kila uchaguzi utakuwa sawa na uliopita.
 
Hivi wafanyakazi wa NEC nao Wana haki ya kupiga kura kumchagua rais?​
Maana nao si ni moja ya watumishi wa umma.​
Katiba yetu imeelezaje kuhusu hawa watumishi?​
 
Hivi wafanyakazi wa NEC nao Wana haki ya kupiga kura kumchagua rais?​
Maana nao si ni moja ya watumishi wa umma.​
Katiba yetu imeelezaje kuhusu hawa watumishi?​
Kila raia katika nchi hii ana Haki ya kupiga kura.
 
Wamefanya hivi kwasababu wanahisi yanaweza tokea CCM pia,,, ila walishindwa nini kushughulikia kabla sisiemu hawajaanza..

Ila ni fresh as long as vyama vyote vinanufaika na mchongo
 
Bora hata umeweza kuona hilo kosa. Nahisi hata barua yenyewe ni fake. Ama ni barua imefanyiwa uhariri kutoka nakala mama, lakini uhariri umefanywa na mtu mwenye uwezo mdogo, huku mwenyekiti wa tume kama ni kweli, akiwa amesaini bila kusoma.
... Kiongozi, mwandishi hakuandika hivyo kwa bahati mbaya; lengo ni kuonesha sio Chadema tu walioathrika bali vyama vyote huku akijisahau kwamba anawaandikia Chadema na sio vyama vyote! Ajabu kweli kweli.
 
ASANTE NEC KWA KULIONA HILI
 
Tume ya UCHAGUZI iongeze vipengele vya kuacha Picha, nakala ya kitambulisho na namba ya simu kwa Msimamizi wa Uchaguzi (DED's) kama kweli wanataka (NIA YA DHATI) kuwakamata hawo WAHUNI .
Ni upuuzi ku-submit maombi ya kuomba kugombea ubunge bila kuambatanisha Picha, Photo ID, Proof of address na contact number.
 
Ukijua kunawia mbele sisi tunanawia nyuma. CHADEMA walivyoona wanadhulumiwa Kibamba na wao wakaenda Musoma kuchukua fomu za Udiwani kwa tiketi ya CCM, tume kuona hivyo ndo wanajifanya wema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…